Wanawake wenye ulemavu ambao waligombea na kukosa waomba kuangaliwa
NA FATMA HAMAD, PEMBA WANAWAKE Wenye Ulemavu kisiwani Pemba ambao waliingia kwenye kinyan’ganyiro kugombea, katika Uchaguzi mkuu 2025, wamemtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Ali Mwinyi kuwangalia kwa jichola huruma kwa kuwapa nafasi mbalimbali, ili walete mabadiliko kwa Taifa na kwa wenzao wenye Ulemavu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwao Katija Mbarouk Ali mwenye Ulemavu wa Viungo ambae aligombea Uwakilishi Jimbo la Kojani ingawa hakufanikiwa, alisema wamekua wakiingia kwenye kinyan’ganyiro ili kuona nawao wanaingia kwenye maamuzi. Alisema wakati kunapokuepo na nafasi za uteuzi kuwapa kipaombele wale ambao walijitokeza kugombea, ili kuwatia hamasa na moyo wa kuingia kwenye kinyan’ganyiro kwa wanawake hao wenye Ulemavu. ‘’Tumejitoa tumedharauliwa kwa sababbu tunapambana na watu wenye pesa na vyeo vyao, hivyo ipo haja Rais utuone, ili kufuta nguvu zetu ambazo tumezipoteza,’’alisema. Alisema watuWeny...