RAHMA HAMAD IDDI : MWANAMKE JASIRI WA WETE ALIEVAA NGAO YA SIASA

 


NA FATMA HAMAD, PEMBA

NI SAA KUMI na moja  za jioni kijua kikiwa kimetulia, kwambaali nikasikia mdundo wa beni umeacha maji, nikanza kuufuatilia ili kujua kuna nini.

Nikanza kusogea kidogo kidogo, nilipofika nikawakuta watu wameroa kijacho wakiserebuka kwa beni, kumbe ilikua ni mkutano wa kampeni wa chama cha ADC.

Hapo ndipo nikamuona mgombea ubunge wa jimbo la Wete kupitia chama cha ADC Bi Rahma Hamad Iddi akiwa jukwaani akiwamwagia sera zake wananchi wa jimboni kwake.

Baada ya kumaliza kuhutubia nilimsogelea nikanza kumsalmia habar za saivi, nzuri hujambo, sjambo, nikamsifu nikamwambia ahongere kwa sera nzuri,nikanza kujitambulisha kwake nikamuomba nifanye nae mahojiano, kwa vile ni mwanamke mwenye kujiamini hakunikatalia.

Bi Rahma Hamad ni mzaliwa wa Mtambwe nyali ana umri wa miaka (32)anasema huu ni mwaka wa tatu tokea kuanza kujingiza harakati za kisiasa.

Anasema tokea akiwa mwananfunzi ndote zake nikutaka kuwa kiongozi, ili aisaidie jamii yake.

‘’Sijashawishiwa na mtu kuingia kwenye harakati hizi bali, ni vile nikiona kero kama vile za ukosefu wa maji vijijini, nilikua natamani kua kiongozi nije kuziondosha,’’anasema.

Anasema mwaka juzi 2023 akanza kujiingiza moja kwa moja katika harakati za kisiasa, na mwaka huu 2025 akajitoa na kujiingiza kwenye kinyan’ganyiro cha kulisaka jimbo la wete.

Anasema jimbo ambalo amegombea ni jimbo lenye mchuano mkali, ila anaaamini kwa asilimia 90 anaweza kushinda, wanawake wenzake wamemuahidi kumuunga mkono.

CHANGAMOTO AMBAZO AMEPAMBANA NAZO

Moja ya changamoto ambazo amekumbana nazo ni jamii kumchukulia vibaya kwamba ameshaingia katika dimbwi la uhuni.

‘’Naambiwa natakakua muhuni kwa vile nishajihusisha na mambo ya kisiaa, ingawa sikuyasikia ninaendelea na harakati zanguhadi ndoto zangu zikamilike,’’anasema.

Mbali ya hilo anasema amekua akidharauliwa na kuambiwa hawezi kushinda yeye mwanamke, kwani uongozi si fani ya mwanamke.

Asema licha ya changamoto hizo hakukata tamaa aliendelea na harakati zake, na ameamua kugombea, kwani anaamini kufanya hivyo ni haki yake ya kikatiba, na naamini siku moja ndoto zake zitatimia.

VIPAUMBELE VYAKE

Rahma anasema endapo atachaguliwa na kuwa kiongozi wa jimbo la Wete,  kuwa karibu na wanawake na kuanzisha kamati maalu za kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

‘’Wanawake na watoto ni makundi ambayo yanakumbana zaidi na udhalilishaji wa kijinsia, nikipata nafasi naahidi kuanzisha kamati maalumu, ambazo zitaepusha matendo hayo ndani ya jimbo langu,’’analeza.

Mbali ya hilo anasema ataanzisha miradi mbalimbali ambayo itawasaidia vijana na wananchi wote kupata ajira, na kuendesha maisha yao.

Pia anasema atawasaidia watoto mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu waweze kusoma elimu ya dunia na ya akhera, ili wajipambanue na hali ngumu za maisha yao.

FAMILIA YAKE INAVYOMUUNGA MKONO

Anasema familia yake imekua bega kwa bega na yeye,na kila anapokwenda kufanya mkutano wanakua wanamfuata, na humsaidi fedha wakati anapohitaji.

‘’Nashukuru familia yangu tuko kitu kimoja, hapa unaponiona kwenye mkutano nipo na baangu, mamaangu ndugu zangu na hata majirani zangu wananifuata,’’anasema.

Anasema pia hatokua mwingi wa fadhila kutoa shukurani kwa mume wake kwani hata usafiri anaotumia kwenda shughuli zake za kampeni ni wa mume wake.

MUME WAKE.

Muhine Ahmed Kombo ni mume wa bi rahma anasema mke wake alipomshauri kutaka kujiunga na harakati za siasa hakumzuia, bali alikua anampa mashirikiano, ili akamilishe ndoto zake za kua kiongozi.

‘’Sijamzuia mke wangu kujiungana harakati hizi za kisiasa, naamini jambo hilo analolifanya ni jema kwani linaweza kuja kuleta maendeleo kwa familia yetu na hata wanajimbo hili la Wete,’’anasema.

KIONGOZI WA CHAMA CHAKE

Katibu Mkuu wa chama cha Alliance for  Democratic  Change ADC  Mwalim Hamad Aziz anasema katika kuhakikisha wanawake wanatimiza malengo yao ya kuwa viongozi, wanawawezesha kwa kuwapa mafunzo mbalimbali wawe na uthubutu wa kuingia majimboni na kuwania uongozi.

Anasema katika chama chao suala la ubaguzi halipo, bali kumekuepo na nafasi sawa kati ya wanaume na wanawake.

Takwimu

Kwa mujibu wa Chama cha Wandishi wa Habari WAnawake Tanzania Tamwa Zanzibar kupitia ripoti iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanziba mwaka 2020, kupitia nafasi ya Uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar wanawake waliojitokeza ni 61 walioshinda ni 8 na wabunge wanawake waliowakilisha Zanziba ni wane.

Takwimu kutoka Tume huru ya Uchaguzi Tanzania kwa upande wa wabunge walikua 141 walioshinda wanawake ni wanne tu.

Kwa Uchaguzi wa mwaka huu 2025, unaweka historia mpya, kwani ni mara ya kwanza wanawake kujitokeza kwa wingi

kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Kwa vile suasa la uchaguzi ni haki ya kila mtu kama katiba Katiba yetu mama ya nchi ya mwaka 1984 inavyoeleza katika kifungu cha 21,(2) kinaeleza mzanzibari yoyote anahaki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia maamuzijuu ya mambo yanayo muhusu yeye, maisha yake au yanayohusu Taifa lake.

Hata Mikataba ya kimataifa ya haki za kiraia na haki za kisiasa ya mwaka 1966 kifungu cha 25, kila raia ana haki ya kupiga kura na kuchaguliwa katika uchaguzi wa kweli, wa haki na wa mara kwa mara, uliofanywa kwa kura ya siri na kuhakikisha uhuru wa wapiga kura.

Ripoti za vyombo vya habari na mashirika ya jinsia zinaripoti ongezeko la wanawake wanaogombea mwaka 2025 ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.

 Zanzibar pia imeona wanawake wakichukua nafasi kubwa katika kuingia kwenye nafasi za juu za uongozi,ikiwa ni sehemu ya mwelekeo wa kitaifa wa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika siasa.

Hata kwa upande wa Bunge, ziko taratibu za viti maalum za wanawake na hii imekuwa moja ya njia za kuimarisha uwakilishi wa kijinsia, ingawa juhudi za kuongezeka kwa wagombea wa kiti cha uwakilishi wa moja kwa moja zinaendelea.

MWISHO

 

 

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI