Wanawake wenye ulemavu ambao waligombea na kukosa waomba kuangaliwa

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

WANAWAKE Wenye Ulemavu kisiwani Pemba ambao waliingia kwenye kinyan’ganyiro kugombea, katika  Uchaguzi mkuu 2025, wamemtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Ali Mwinyi kuwangalia kwa jichola huruma kwa kuwapa nafasi mbalimbali, ili walete mabadiliko kwa Taifa na kwa wenzao wenye Ulemavu.

Akizungumza na mwandishi wa habari  hizi huko nyumbani kwao Katija Mbarouk Ali mwenye Ulemavu wa Viungo ambae aligombea Uwakilishi Jimbo la Kojani ingawa hakufanikiwa, alisema wamekua wakiingia kwenye kinyan’ganyiro ili kuona nawao wanaingia kwenye maamuzi.

Alisema wakati kunapokuepo na nafasi za uteuzi kuwapa kipaombele wale ambao walijitokeza kugombea, ili kuwatia hamasa na moyo wa kuingia kwenye kinyan’ganyiro kwa wanawake hao wenye Ulemavu.

‘’Tumejitoa tumedharauliwa kwa sababbu tunapambana na watu wenye pesa na vyeo vyao, hivyo ipo haja Rais utuone, ili kufuta nguvu zetu ambazo tumezipoteza,’’alisema.

Alisema watuWenye Ulemavu maranyingi wamekua wakisahauliwa katika fursa mabalimbali ambazo zimekua zikitokezea, hivyo ipo haja serikali kuwaona ili wafaidike na fursa hizo ambazo zimo katika serikali yao.

Halima Suleiman Ali mkazi wa Mtambile aliejitosa kuania udiwani Wadi ya Mtambile alisema wakati wa wanawake wenye ulemavu kuwekwa nyuma katika fursa za maamuzi  umepitwa na muda, hivyo ni wakati kupewa nafasi, hivyo ni vyema kupewa nafasi ili kuonesha uthubutu na uwezo walionao wa kutumikia taifa lao.

‘’Wanawake wenyeulemavu hatutaki tena kuekwa nyuma, tunaomba tuangaliwe hususani wale ambao tumeonesha uthubutu wetu tokea kwenye Uchaguzi Mkuu,’’alisema.

 Nasra Fakih Hassan mwenye ulemavu wa viungo  mzaliwa wa Kangagani Wete Pemba , ambaye alijitosa kugombea nafasi ya uwakilishi viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi  (CCM) alisema katika nafasi za wanawake za Wilaya na za mkoa kuhakikisha watu wenyeulemavu wanazipata nafasi hizo.

‘’Makundi yote ikiwemo Vijana, Wanawake kila mkoa na wilaya zinakua ni mbili mbli, iweje kundi la watu wenye ulemavu iwe ni nafasi moja mkoa mzima ama Pemba mzima, tunaomba tuangaliwe tuwemo kila sehemu,’alisema.

 Mratib wa Jumuia ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Pemba Juma Kombo Hija, aliema katika Uchaguzi wa 2025, Wanawake Wenye Ulemavu walihamasika kuingia kwa wingi majimboni kuania uongozi ikiwa walikua ni 12, kwa Pemba pee ambapo haijawahi kutokea kwa chaguzi zilizopita.

Alisema ni vyema serikali kuwatupia jichowanawake hao ambao walionesha uthubutu wao kwa kuwapatia nafasi waweze kufikisha mchango wao katika serikali yao, sambamba na kutoa hamasa kwa wanawake wenzao wenyeulemavu wa kushiriki harakati za kimaendele, zilizomo katika Taifa lao.

Kaimu Mratibu wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanziba  Ofisi ya Pemba Amina Ahmed Mohamed alisema wamekua wakifanya jitihada  mbali mbali, kuona wanawake wenyeulemavu wanaingia katika nafasi za maamuzi.

‘’Huu ni mwaka wa mabadiliko tumechoka kuona wanawake wenye ulemavu wakitazamwa kama wakulima, tunatamani kuona wanaigia kila sehemu,’’alisema.

Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa akiwemo Hamad Rashid Mohamed wa chama cha Alliance for  Democratic  Change (ADC)  Maryam Saleh Juma kutoka  chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma) walisema wanawake wenye ulemavu wanamchango mkubw, hivyo ipo haja kupewa kipaombele na kuona wanashiriki kwa wingi katika nafasi mbali mbali za maamuzi.

Sheria ya watu enye ulemavu namba 8 ya mwaka 2022, kifungu cha 29 kinaeleza, umuhimu wa watu wenye ulemavu kufikia miundombinu pamoja na taarifa, mawasiliano na haki zote za kibinadamu.

Katika programu za uchumi nchini Tanzania, hata pale ambapo watu wenye ulemavu wanashirikishwa, mara nyingi katika harakati za kijamii, bado nafasi za uongozi ni chache.


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO