“Uchumi, unavyofifiza Ndoto za Wanawake Wenye Ulemavu kufikia uongoz’’
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2025, Tanzania imeshuhudia wimbi jipya la wanawake wenye ulemavu wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi kutoka udiwani, ubunge hadi uwakilishi wa majimbo.
Ingawa nyuma ya safari
hiyo ya kisiasa, kuna simulizi ya
kiuchumi, unavyosababisha wanawake hao
kufikia malengo yao ya kisiasa.
Makala hii inachambua jinsi uchumi wa wanawake wenye ulemavu
unavyoathiri ushiriki wao katika maamuzi, nafasi zao za uongozi, na sauti yao
katika jamii ya Tanzania, hususan Zanzibar, kwa kuzingatia takwimu, sheria, na
mikataba ya kimataifa.
Utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wa mwaka 2022,
unaonesha zaidi ya asilimia 73 ya watu wenye ulemavu nchini, wanafanya kazi
katika sekta zisizo rasmi hususan kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo.
Maranyingi, wanawake
wenye ulemavu wanabaki nyuma zaidi kwa sababu ya changamoto hiyo ya uchimi, mitajina
ukosefu wa fursa za kifedha, hali hii huwafanya kushindwa kugharamia kampeni za
kisiasa au kushiriki ipasavyo katika uongozi.
Katika uchaguzi wa mwaka 2025, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
ilisajili wagombea 1,735 wa ubunge, kati yao wanawake walikuwa 558 (sawa na
32%), hata hivyo, ni wagombea 27 tu waliokuwa na ulemavu wakiwemo wanawake,
chini ya asilimia 2 ya jumla ya wagombea wote.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), ilithibitisha wapiga kura 717,557, ambapo wanawake walikuwa
asilimia 53.
Hata hivyo, uwiano huu
haukuakisi kwenye orodha ya wagombea wenye ulemavu, ambapo wachache sana
waliweza kufikia hatua za mwisho za uteuzi au ushindi.
Baadhi ya wanawake wenye ulemavu walijitokeza kugombea kupitia
vyamavya siasa, ingawa walikosa rasilimali fedha na kupelekea wenye pesa zao
kujichiukulia majimbo, kutokana na mfumo wa uchaguzi ulivyo.
Halima Suleiman Ali mkazi wa Mtambile mwenye
ulemavu wa uoni hafifu, amejitosa kuwania udiwani Wadi ya Mtambile, ingawa
hakufanikiwa, anasema suala la uchaguzilinahitaji gharama.
“Uchumi wetu ni dhaifu, na si rahisi kugombea bila fedha, wengi
wetu tunabaki kuwa wafuasi badala ya viongozi,” anasema.
Anasema fomu moja pekee ya udiwani ni shilingi 50,000, ukipita
kuna pesa za kampeni ambapo unatakiwa ufanye mkutano kila shehia, napo hapo
fedha huhitajika.
Mwingine ni Katija Mbarouk Ali mwenye ulemavu wa viungo mkaazi
wa Kiuyu Minungwini wilaya ya Wete, aliyegombea Uwakilishi jimbo la Kojani,
anasema uchumi ni moja ya kikwazo kinachowakosesha kuingia kwenye maamuzi.
Anasema ameshagombea marambili na wala hawajawahi kufanikiwa,
ingawa mwaka 2020 aligombea nafasi hiyo kupitia viti maalumu.
Anasema ambacho amekigundua kushindwa yeye kuingia kwenye
maamuzi ni kukosa pesa, kama wanavyofanya wingine.
‘’Fomu tu ya uwakilishi ya kugombea ni shilingi 500,000 hujapata
pesa za kuchapisha mabango, vipeperushi na hata kufanya mikutano ya kampeni,
hicho ni kikwazo kinachorudisha nyuma,’’anasema.
Marahii aliamua kugombea jimboni, kwani alihisi angeweza kupata
unafuu wa gharama, ila anasema mambo ni magumu kwake kwa pande zote, kutokana
na uchumi wake.
Bi Amina Abdala Said mwenye ulemavu wa viungo mteule wa udiwani viti maalum, kupitia Chama cha ACT WAZALENDO wadi ya Changaaweni Mkoani, anasema kulingana na mifumo ya harakati za uchaguzi ilivyo, wanawake wenye ulemavu ni vigumu kupata nafasi.
‘’Kwakweli sasahivi uongozi ni biashara, hivyo kama huna pesa
huwezi kulikamata jimbo, hivyo sisi wenye ulemavu ni vigumu, kushika nafasi, na
badalayake huzichukua watu wenye pesa zao,’’anaeleza.
Tumu Mwalim Massoud wa Wingwi Micheweni, ambae amegombea
uwakilishi Jimbo la Wingwi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu
wa 2020, anahamu ya kuwa kiongozi, ingawa akikumbuka gharama zilizomtoka, hatamani
tena kugombea.
Anasema mbali na gharama ya fomu ya Uwakilishi ya shilingi 500,000
pia unahitajika ufanye mikutano wastani mitano kwenye jimbo, usafiri, vipaza
sauti na vyote hivyo vinahitaji uvigharamikie mwenyeo.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kushindwa, alianza kuuza gari
yake ya kutembelea, N’gombe wa mamake ili apate fedha ya kulipa madeni.
‘’Kwa sasa najifikiria kugombea tena kwa sababu nakumbuka maumivu
ya kulipa madeni, ingawa natamani niingie tena kwani ndoto yangu ya kuwa
kiongozi haijakamilika,’’anasema.
Anasema kwa mujibu wa utaratibu ulivyo, anaetaka kugombea
uwakilishi, anatakiwa alipie chamani shilingi 100,000 kwa kuchukua fomu.
Pia anatakiwa kulipa Tume ya uchaguzi shilingi 500,000, wakati huo
huo ukitakiwa kuchukua fomu, kwa ajili ya kuendelea na harakati nyingine.
JAMII
Hadia Omar Ali mkaazi wa Sizini anasema, ikiwa serikali
haitokipatia ufumbuzi kilio hicho, siku zote wanawake wenye ulemavu wataendelea
kushika mkia tu kwenye chombo cha mamuzi.
Mohamed Hassan Ali mkaazi wa Wete, anasemawanawake wenye ulemavu
hawawezi kumudu gharama za chaguzi, kwani uchumi wao uko chini.
JUMUIA ZA WATU
WENYE ULEMAVU
Hidaya Mjaka Ali kutok Jumuia ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA),
anasema uchumi bado kikwazo kinachopelekea wanawake wenye ulemavu kushindwa,
kuonekana kwenye maamuzi.
Anasema bila ya kuwepo uwezeshwaji kwa wanawake hao, wengi wao
hawana kipato kikubwa ambacho kianawezesha kumudu shughuli za uchaguzi.
‘’Chaguzi za sikuhizi, zimekua ni biashara, kama huna pesa huwezi
kufanikiwa, na ndiomaana sisi wenye ulemavu hatupati nafasi, kwani uchumi wetu
ni wa kipato cha chini,’’anaeleza.
Mashavu Juma Mabrouk ni Mratibu wa Baraza la watu wenye Ulemavu
kisiwani Pemba, anasema wanawake wenye ulemavu, wamepata hamasa ya kuingia
kwenye harakati za maamuzi, ingawa bado wanashindwa kumudu gharama.
Anasema wingi wa wanawake wenye ulemavu ni masikini wa kipato, hawamiliki
hata mahitaji ya nyumbani kwake, seuze ya uchaguzi.
WANAHARAKATI
Tatu Abdalla Mselem ni mwanaharakati wa masiuala ya utetezi kwa
wanawake, watoto, mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu(TUJIPE) nasema
katika zama za sasa pesa ndio kigenzo kikubwa kinachosababisha watu kushika
nafasi za uongozi.
Anasema Wanawake Wenye Ulemavu sio rahisi kufanikiwa kuyakamata
majimbo, kwani uchumi wao ni mdogo, gharama za chaguzi zimekua kubwa hawawezi
kuzimudu.
‘’Kutokana na gharama za Chaguzi zilivyopanda, napata kusema
Wanawake Wenye Ulemavu ni vikugumu kuyakamata majimbo na kuingia kwenye maamuzi
kwani hali zao wenyewe ni duni,’anasema.
Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-
Zanzibar (TAMWA)Dk. Mzuri Issa Ali anasema wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu, ushawishi
wa sera, na kuwajengea wanawake wenye ulemavu.
NINI ATHARI YAKE
Ikiwa vyama vya siasa pamoja na serikali havikukaa chini na
kutafakari mifumo ya uchaguzi iliyopo sasa, basi Wanawake Wenye Ulemavu na hata
wasio na ulemavu itakua ni nadra kushika uongozi,’’wanasema wananchi.
NINI KIFANYIKE?
Ili kuona Wanawake Wenye Ulemavu na wao wanashiriki kwenye
harakati za uchaguzi na kuingia kwa wingi katika maamuzi, ipo haja kwa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuweka ruzuku maalum, mafunzo pamoja na mitaji ambayo
itawasaidia wagombea hususan wanawake wenye ulemavu.
MIKATABA
Tanzania imeridhia Mkataba
wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD), wa mwaka
2006 kinahimiza serikali, kuhakikisha
ushiriki sawa wa watu wenye ulemavu katika siasa na maamuzi.
Hata Mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na haki za
kisiasa ya mwaka 1966 ibara ya 25, kila raia ana haki ya kupiga kura na
kuchaguliwa, katika uchaguzi wa kisiasa.
Katiba ya Zanzibar ya 1984,kifungu chake cha 21(1) nacho kinatambua haki ya kila raia,
kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi bila ubaguzi.
Kifungu kidogo cha (3) kinaeleza kwamba, kila mzanzibari anayohaki
ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyoko chini ya mamlaka ya
Zanzibar.
Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka
2018 inaweka
mazingira ya upatikanaji wa haki sawa, kwa wagombea wote, wakiwemo wenye
ulemavu, lakini utekelezaji wake bado unahitaji nguvu zaidi.
Sheria ya watu enye ulemavu namba 8 ya mwaka 2022, kifungu cha
29 kinaeleza, umuhimu wa watu wenye ulemavu kufikia miundombinu pamoja na
taarifa, mawasiliano na haki zote za kibinadamu.
Katika programu za uchumi nchini Tanzania, hata pale ambapo watu
wenye ulemavu wanashirikishwa, mara nyingi katika harakati za kijamii, bado
nafasi za uongozi ni chache.
China, takwimu zinaonyesha kwamba kipato cha wanawake wenye
ulemavu ni sawa na asilimia 42.5 ya kipato cha wastani kwa mtu bila ulemavu.
Ripoti ya Women’s World Banking inaonyesha kampeni ya taasisi ya
wanawake wenye ulemavu nchini Indonesia ambayo imetoa mafunzo ya ujuzi wa fedha
za kidijitali, na hivyo kuongeza fursa zao za kiuchumi.

Comments
Post a Comment