Posts

‘’Wandishi endeleeni kuipigia debe Sheria ya habari, ili irekebishwe’’

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA Wandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuipigia kelele Sheria ya habari, kuona imefanyiwa marekebesho na  kuondoshwa vifungu vinavyokwaza  uhuru wa habari na vyombo vya habar. Alisema wandishi wa habari ndio wahanga wakubwa ambao wanaathirika kutokana na kuepo  kwa Sheria inayominya uhuru wao kwani inapelekea kukosa baadhi ya tarifa. Akizungumza na wandishi wa habari katika mkutano wa tathmini wa mradi wa  kudai uhuru wa habari, Afisa miradi na tathmini kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Mohd Khatib Mohd, alisema kukosekana na sheria rafiki hakuathiri wandishi wa habari pekeyao bali hata jamii kiujumla.  Hivyo Afisa huyo alisema  kuepo kwa hilo, ipohaja kuendelea kuandika habari zinazoshawishi  kufanyiwa marekebisho na kupatikana kwa Sheria mpya Zanzibar. Mapema akiwasilisha ripoti ya mapitio a Sheria za Habari  Afisa programu kutoka Tamwa, Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, alisema licha ya juhudi mbalimb...

Wandishi wa habari watakiwa kuielimisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi

Image
                      NA FATMA HAMAD, PEMBA AFISA ELIMU kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Pemba Nassor Ali Salim, amesema endapo kama, hakutochukuliwa hatua za makusudi za kukabiliana na athari zinazotokana na  Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya miaka 100 kisiwa cha Pemba kitabakia historia, kutokana na maji ya bahari kuingia Nchi kavu. Alisema kufuatia tatizo hilo la Majichumvi kuingia katika Nchikavu,  kunauwezekano mkubwa wa kupoteza Kilomita za mraba 286, sawa na asilimia 28 ya eneo lote la Pemba. Alisema watu wanaongezeka na Ardhi inaendelea kupungua, hivyo endapo kama hakutochukuliwa jitihada za ziada, juu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kisiwa cha Pemba kitakua kiko hatarini zaid, na watu wanaweza kuja kukosa maeneo ya kuishi. Alisema yapo maeneo yasiyopungua  123 yakiwemo  makaazi ya watu pamoja na mashamba yanayotumika kwa ajili ya kilimo, yameathirika kutokana na uingiaji wa majichumvi. ‘’Tuna ...

SHERIA RAFIKI NI NGUZO MUHIMU KWA WAANDISHI KUFANYA KAZI KWA UFANISI

Image
  Na Mwandishi wetu Kupatikana kwa sheria mpya na rafiki ya habari visiwani Zanzibar kutasaidia kuweka mazingira bora ya kazi kwa waandishi wa habari, kwa kuhakikisha ulinzi na ushiriki wao unapatikana kikamilifu hususan katika kipindi cha uchaguzi. Akizungumza katika mkutano maalum ulioandaliwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) huko Tunguu, Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ, Dkt. Mzuri Issa, amesema kuwa ni haki ya waandishi wa habari kuwekewa mazingira bora ya kazi. Alisisitiza kuwa kuwepo kwa sheria rafiki ya habari kutawawezesha waandishi kufanya kazi kwa uhuru, ufanisi, na kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao. Amesema kuwa kwa sasa teknolojia ya habari imekuwa kwa kasi, na idadi ya vyombo vya habari, hususan vya binafsi, imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, licha ya maendeleo hayo, waandishi wa habari bado wanalazimika kufanya kazi kwa kutumia sheria zilizotungwa tangu mwaka 1988, ambazo hazina mlingano na mahitaji y...

Unyanyapaa ulimsukuma Maryam kujifungulia nyumbani

Image
  Ilikuwa chanzo kumuambukiza mtoto wake VVU Sasa anao watutu wakiwa salama, kama alivyo muume wake NA FATMA HAMAD, PEMBA MIMBA yangu ya kwanza nilijifungulia nyumbani kwani nilikua nanyayapaliwa, na ndio chanzo cha kumuambukiza mtoto wangu VIRUSI vya Ukimwi. Hayo ni maneno ya Maryam Said mkaazi wa Chake chake mwenye umri wa miaka 38 ambae anaishi na virusi vya ukimwi kwa muda wa miaka 18 sasa. Anasema alimuambukiza mtoto wake wa mwanzo mambukizi ya virusi vya UKIMWI  Mimba yake ya kwanza, alijifungulia nyumbani, kwa hofu ya kwenda Hospital kwa kuogopa kunyanyapaliwa. ‘’Hadi leo najilaumu, na najutia nafsi yangu, kwa kitendo cha kutokimbilia hospitali kwa ajili ya kwenda kujifungua nikidhani kwamba nyumbani ni salama,’’anasimulia.  Kwa sasa  ameshajifungua watoto  wengine watatu, ambao wako salama hawana   maambukizo  ya  VVU , baada ya kusikiliza na kutekeleza kwa vitendo ushauri wa watalamu wa afya.  aligundulika na Virusi Vinavyosabab...

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

Image
                 NA FATMA HAMAD, PEMBA UTELEKEZAJI ni ile hali ya wazazi kukwepa majukumu yao ya kutoa matunzo kwa familia zao. Wengi wa wananchi wanadai kwamba, sababu kubwa inayopelekea utelekezaji ni baadhi ya akinababa wanapoamua kuoa mke zaidi ya mmoja, maranyi huwa hawatimizi wajibu wao. Ingawa wapo wengine, hudai kukumbwa na sababu, ya kutafuta maisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, mfano wa wavuvi au wafanyabiashara. Hayo yakifanyika, mafundisho ya dini yanafundisha kuwa, mzazi wa kiume ndio mwenye jukumu kubwa la kutoa matunzo kwa familia yake. Lakini ulimwengu wetu wa leo, kumeibuka wimbi kubwa la baadhi ya wanaume kukwepa majukumu  yao na kuwabebesha mzigo wa malezi wanawake peke yao. Hali hiyo ya wanaume kutokushughulikia familia zao, inasababisha watoto kuishi kwa simanzi na huzuni, kana kwamba wamefiwa na wazazi wao na kukosa familia ya kuwatunza. Kiongozi wa Kanisa Katoliki lililopo Mkungu Malofa Chakechake, Robert Mig...

Mfahamu Joahari, binti mwenye ndoto ya kua kiongozi

Image
                     NA FATMA HAMAD- PEMBA Kuwapa nafasi wasichana katika mijadala ya kisiasa, vikundi vya uongozi shuleni na vyuoni, , kunawajengea ujasiri wa kushiriki kwenye michakato ya kisiasa mapema na wakiwa na taarifa sahihi. Hili linasaidia kuvunja mila na desturi zinazoweza kuzuia wanawake kushiriki nafasi za uongozi  kwa   kiwango kikubwa. Kwa  kuanzisha  ushiriki  wao  mapema, tunaunda  kizazi  cha  wanawake wenye ujasiri na maarifa, ambao  watakuwa  tayari  kuwania  nafasi za  uongozi  na  kushiriki  kikamilifu  katika  kufanya maamuzi kwa maslahi ya jamii nzima. Hii pia inaongeza uwezekano wa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kisera kuhusu masuala yanayohusu wanawake na vijana. Makala hii imezungumza na Johari Ibrahim Mbarouk ambae ni Rais wa Skuli ya Msingi Kiungoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambae ana ndot...