‘’Wandishi endeleeni kuipigia debe Sheria ya habari, ili irekebishwe’’
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Wandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuipigia kelele Sheria ya habari, kuona imefanyiwa marekebesho na kuondoshwa vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari na vyombo vya habar.
Alisema wandishi wa habari ndio wahanga wakubwa ambao wanaathirika kutokana na kuepo kwa Sheria inayominya uhuru wao kwani inapelekea kukosa baadhi ya tarifa.
Akizungumza na wandishi wa habari katika mkutano wa tathmini wa mradi wa kudai uhuru wa habari, Afisa miradi na tathmini kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Mohd Khatib Mohd, alisema kukosekana na sheria rafiki hakuathiri wandishi wa habari pekeyao bali hata jamii kiujumla.
Hivyo Afisa huyo alisema kuepo kwa hilo, ipohaja kuendelea kuandika habari zinazoshawishi kufanyiwa marekebisho na kupatikana kwa Sheria mpya Zanzibar.
Mapema akiwasilisha ripoti ya mapitio a Sheria za Habari Afisa programu kutoka Tamwa, Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, alisema licha ya juhudi mbalimbali zinazochukuliwa kupiga kelele kupatikana kwa Sheria mpya za habari, bado halijafanyiwa kazi ipaswavyo, ingawa Baraza la Wawakilishi limeahidi kuifanyia kazi kwa mwaka ujao.
Alisema wamewajengea uwezo wandishi wa habari kuvifahamu vifungu vinavyokandamiza uhuru wao, waweze kuvifahamu na kuvisemea virekebishwe, na kuwekwa vingene vipya ambavyo vinaendana na muda.
Alisema jumla ya makala na vipindi 237 zimeandikwa na wandishi wa habari kwa muda wa mwaka mmoja, ambazo zimekua zikishawishi serikali kuona umuhimu wa kupatikana kwa sharia mpya ya habari Zanzibar.
"Miongoni mwa matokeo ya mradi huu ni pamoja na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuzitambua Sheria za Habari kuona mapungufu yaliyomo katika Sheria hizo, kutoa mapendekezo ili ziweze kufanyiwa marekebisho" alisema
Comments
Post a Comment