Posts

Hemedi alitwisha mzigo shirika la Nyumba la Zanzibar

Image
                           Na Fatma Hamad- Pemba Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar   Hemed  Suleiman Abdulla ameliagiza Shirika la Nyumba  kuendelea kujenga majengo ya kisasa katika mji wa Chakechake, ili uweze kuendena na mazingira ya sasa. Makamo huyo ameyasema hayo wakati akifungua Nyumba za biashara na maakazi huko Mkungumalofa Chakechake   Mkoa wa   Kusini   Pemba. Amesema   Serikali   ya   awamu ya nane, imedhamiria kujenga   majengo ya kisasa   katika   miji   yote   ya Zanzibar, ili kuona wananchi wake wanaishi katika majumba zenye hadhi na zenye kuvutia. ‘’Chakechake   ndio mji mkuu wa Pemba, nikuombe waziri wa Ardhi   kuhakikisha Chakechake   imebadilika, nakua mji wa kisasa,’’ameagiza. Amesema majengo hayo ya kisasa yatawanufaisha wananchi kupata makaazi bora, pamoja   na wafanyabiashara wote, hivyo ni budi ...

Mitazamo finyu ya jamii inavyowakosesha fursa za uongozi, wanawake

Image
                               Na Fatma Hamad-Pemba Kwa mujibu wa Sensa   ya   watu   na   makazi   ya   mwaka   2022   Zanzibar   inawanawake wengi   ambao   ni   974,281   sawa   na   asilimia   51.6   kuliko   wanaume, ikiwa   wao   ni   915,492   sawa na   48.4   ambapo   licha   ya   uwingi   huo bado   idadi   kwenye   ngazi   za   maamuzi   ni   kidogo.   licha ya uwingi huo bado idadi ya wanawake wanaojitokeza na kugombea   Kati ya hao, ni asilimia 21.14 tu kwa wanawake 71 waliojitokeza kugombea udiwani. Kwa nafasi ya uwakilishi wanawake waliogombea ni 251, wakiwemo wanaume 190 na wanawake 61, ambapo walishinda wanaume 42 na wanawake nane (8) sawa na asilimia 16 , wabunge walioshinda wanawake ni wanne sawa na asi...

Jamii yatahadharishwa kuachwa nyuma wanawake wenye ulemavu mradi mabadiliko tabia nchi

Image
                                   Na Fatma Hamad- Pemba …...hana mguu, hana mkono, haoni, atawezaje kutunza mazingira……. HAYO NI MANENO ya ALi   Juma Mbarouk   kiongozi wa kamati ya uhifadhi mazingira Chwale anasema wanawake wenye ulemavu ni vigumu kuingizwa kwenye kamati za utunzaji mazingira. Anasema kamati yake, ina wajumbe 15, kati ya hao hamna hata mjumbe mmoja mwanamke mwenye ulemavu. Anasema hajamshirikisha   mwanamke yeyote mwenye ulemavu, kwani anadhani hawezi kufanya shughuli hizo za uhifadhi kutokana na hali zao. ‘’Mtu aliekua hana mguu, hana mkono, wala haoni atawezaje kupambana na mabadiliko ya tabianchi hasa kwa kuwemo ndani ya kamati,’’anasema. VIONGOZI/WAJUMBE WA KAMATI Fatma Shaaban Mohamed ni kiongozi wa kamati ya kilimo msitu shehia ya Mjini kiuyu, anasema katika kamati yake anao wajumbe 25 mtu mwenye ulemavu hana hata mmoja. Anasema hajawahi kum...

Huuhapa mkakati wa vyama vya siasa, kuwandaa wanawake kuelekea uchaguzi wa 2025.

Image
                                     Na Fatma Hamad – Pemba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotolewa azimio   Octoba 31 mwaka 2000 limesema kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi inazidisha demokrasia ya nchi, uchumi, amani na utulivu. Eneo jengine ni katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 21 (1) kinaeleza   kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke   na taifa lake. Hata Sera ya Chama cha Mapinduzi   kwenye mkakati wake, ni kuongoza umma wa watanzania katika ujenzi wa uchumi wa kisiasa,   utakaoleta   maisha bora ya wananchi kwa kuwawezesha   kiuchumi.   Kwa mujibu wa   Mkataba wa Kikanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika,   uliotiwa saini mwaka 2008 kupitia kifungu nambari 13 cha mkataba huo,   kinaelezea   kuwekwa   mik...

Wanawake wawagaragaza wanaume, katika kamati za uhifadhi mazingira za shehia

Image
                          Na Fatma Hamad- Pemba Rais Samia Suluh Hassan wa Tanzania, mara baada ya kula kiapo Machi 19, 2021, alitaja moja ya vipaumbele vyake, ni kuyashirikisha makundi mbali mbali wakiwemo wanawake. Na ndio maana wapo mawaziri kadhaa wanawake wanaoongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo waziri wa Afya Jenister Mhagama, na mwenzake   Ashatu Kijaji anashikilia wizara ya Mifugo na uvuvi. Lakini hata wizara ya Fedha na mipango, inashikiliwa na mwanadada   Natu Elmaamry Mwamba kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Eneo jingine ni uwepo wa sera ya taifa ya Jinsia na maendeleo ya mwaka 2023/2033 ambayo nayo imehimiza, uzingatiaji wa haki na usawa wa kiuchumi kwa   wanaume. Kwa Zanzibar katiba ya mwaka 1984, kifungu cha 10 (e) kimeleza kila raia atakuwa na haki sawa, majukumu na fursa sawa kwa mujibu wa sheria.   Ndani ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jins...