Huuhapa mkakati wa vyama vya siasa, kuwandaa wanawake kuelekea uchaguzi wa 2025.

 

                                   Na Fatma Hamad – Pemba

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotolewa azimio  Octoba 31 mwaka 2000 limesema kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi inazidisha demokrasia ya nchi, uchumi, amani na utulivu.

Eneo jengine ni katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 21 (1) kinaeleza  kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke  na taifa lake.

Hata Sera ya Chama cha Mapinduzi  kwenye mkakati wake, ni kuongoza umma wa watanzania katika ujenzi wa uchumi wa kisiasa,  utakaoleta  maisha bora ya wananchi kwa kuwawezesha  kiuchumi.

  Kwa mujibu wa  Mkataba wa Kikanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika,  uliotiwa saini mwaka 2008 kupitia kifungu nambari 13 cha mkataba huo,  kinaelezea  kuwekwa  mikakati  madhubuti ya kuwawezesha wanawake kimafunzo na kuwashajiisha katika nyanja mbalimbali za siasa.

Kimataifa, ni asilimia 26.7 tu wanawake kote ulimwenguni ambao ni wabunge, huku asilimia 35.5 wakiwa katika nafasi za serikalini.Huku  asilimia 28.2 tu ya wanawake wanaoshika nafasi za kiutawala mahali pa kazi.

Emma Rubagumya mbunge na mwanakamati wa Kamati ya masuala ya jinsia katika Bunge la Rwanda,anayewakilisha  nchi yake katika Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW,katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York,anasema ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya ngazi zote imewaweka mahali pazuri!

Bi Emma Rubagumya akizungumza nje ya mkutano huo anasema wanawake wanapokuwa wengi katika ngazi za  maamuzi,  inakuwa rahisi kujua matatizo hasa  yanayowakabili wanawake.

 

Kwa mujibu wa takwimu za hivi sasa nchi za Rwanda, Cuba na Bolivia, zinaongoza kwa kuwa na wawakilishi wanawake zikiwa na zaidi ya asilimia 50.


 Hivyo basi ili kuona Zanziba nayo wanawake waupiga mwingi, katika nafasi za maamuzi, vyama vya siasa kisiwani Pemba vimekuja na mkakakti  maalum wa kuwandaa wanawake katika vyama vyao, ili wawe na uthubutu  wa kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA.

Hassan Khamis mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba anasema mkakati wao ni kuhakikisha wanawake wa chama chao wamekua na uthubutu wa kuingia majimboni na kugombea nafasi za uongozi.

‘’Kwasasa  tunawapa  mafunzo  wanawake ambayo yanajikita zaidi kujiamini na kujitambua, ili waweze kuondokana na woga,’’ anaeleza.

Khamis anasema furaha yao ni kuona wanawake wameingia kwa wingi majimboni, na  kujichukulia nafasi mbalimbali za uongozi.


Abass Mohamed Khatib  Mratibu wa Chama cha Demokrasia Makini (DP) kisiwani Pemba, anasema  wanawapa elimu ya uongozi wanawake wa Chama chao, ili waweze kujiamini na kuweza kugombea nafasi nje na ndani ya chama.

‘’Tunawapatia mafunzo  ya uongozi wanawke, ili kuona na wao uchaguzi mkuu wa mwakani wanaingia kwa wingi majimboni na kujichukulia nafasi mbalimbali za uongozi,’’anasema Abass

Kumbe mkakati hauko kwa CCM  pekee bali hata kwa upande wa  Chama cha ACT WAZALENDO nako kunaunguruma, kwani kumeanzishwa miradi maalum,  kwa ajili ya kuwasaidia wanawake kujipatia kipato.

Saleh Nassor  Juma ni Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO Mkoa wa Kusini Pemba kichama, anaeleza  kwa  sasa  mkakati  wao mkubwa wameweka miradi maalumu  ambayoitawapitia kipato, ili wamudu kuendesha shughuli zao za uongozi.

‘’Tumeanzisha miradi midogo midogo ambayo itawasaidia wanawake kujiandaa na shughuli za uchaguzi wa mwakani,’’ anasema katibu.

JEE HILI LINA UKWELI WOWOTE/WANAWAKE WENYEWE

 Rukia Abubakar Mohamed  mkaazi wa Machomane, Aligombea nafasi ya uwakilishi Jimbo la ChakeChake, anasema  Chama chao kimekua kikiwajengea uwezo kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ya uongozi.

 ‘’Kama si chama ambacho  kinatuandaa na kutufanya tuwe na uthubutu, basi wengine wangeshindwa kuingia majimboni na kuwania nafasi na wanaume’’,alisimulia Rukia.

Anasema Chama chao kimekuwa kikiwapika vya kutosha na ndio maana yeye amekua na uthubutu wa kuingia kwenye mchakato na kugombea.

‘’Tumekua tukipatiwa mafunzo mbalimbali ya uongozi, na ndio maana wengine tukaweza kuingia majimboni kuwania nafasi za uongozi na wanaume,’’anasimulia Rukia.

Mpaji Abass mkaazi wa Chakechake, mwanachama kutoka Chama cha ACT WAZALENDO, anasema chama chao kimekua kikiwapa mafunzo ya kuwa na uthubutu na kujiamini, ili waweze kugombea.

‘’Nimejiunga kwenye chama huu ni zaidi ya mwaka wa 18, nimejengwa vya kutosha na  kwavile tayari nishakua na uwezo, uchaguzi wa mwakani naingia jimboni kugombea ubunge jimbo la Chakechake,’’anasema.

JAMII

Bimize Othman Ali, 42 mkaazi  wa Wilaya ya Micheweni Sizini  anasema mwanamke ana umuhimu mkubwa katika ngazi za maamuzi, kwani ndo anaejua  zaidi kero na shida zinazowakumba wanawake wenzake.‘’Tukiwa tumebakiwa na siku chake  za kuingia mwaka wa 2025, nivyema viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanawajenga wanawake, waondokana na hofu, jambo litalowasaidia kuingia kwa wingi majimboni “ anasema.

WANAHARAKATI

Wanaharakati wa masuala ya jinsia na utawala bora wako mstari wa mbele katika kuwasaidia wanawake kwenye masuala ya wanawake na uongozi,Hafidh Abdi Saidi kutoka Jumuiya ya Utetezi wa Kimazingira na Jinsia ‘’PEGAO ’’ anasema licha ya kuwa wanawake wamekua na mwamko  juu ya uongozi,  lakini bado  ipo  haja kwa  wanasiasa  kuongeza  nguvu  ya kuwaelimisha  wanawake,  ili  wawe  na uthubu wa kuingia  majimboni kwa wingi.

‘’Ni wakati kwa wanasiasa kuongeza bidii ya kuwajenga uwezo wanawake, ili kuona uchaguzi wa mwakani idadi ya wanawake kwenye majimbo imeongezeka,’’anafahamisha.


Afisa Mkuu wa mahusiano kutoka Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar -TAMWA Sophia Ngalaphi, anasema vyama vya saisa viweke mkakati malaum wa kuwasuka na kuwapika wanawake ambao wanania  ya  kugombea , ili  wasivunjike  moyo  na badalayake  waingie jimboni na kugombea.

‘’Furaha  yetu  kama  wanaharakati  ni  kuona  wanawake wameingia  kwa  wingi  majimboni,  ili  kupata  idadi  kubwa ya wanawake  katinga  ngazi  za uongozi,’’anasema  Sofia.

NINI KIFANYIKE

Ili kuhakikisha wanawake wameingia kwa wingi majimboni nakugombea nafasi za uongozi na wanaume, katika Uchaguzi wa 2025 ni vyema kwa vyama vya siasa,  kuwandaa mpango mkakati wa kuwapika wanawake waondokane na khofu, amedai Juma Kombo mwananchi kutoka Wingwi kisiwani Pemba anaeleza.

Kwa mujibu wa Sensa  ya  watu  na  makazi  ya  mwaka  2022  Zanzibar  inawanawake wengi  ambao  ni  974,281  sawa  na  asilimia  51.6  kuliko  wanaume, ikiwa  wao  ni  915,492  sawa na  48.4  ambapo  licha  ya  uwingi  huo bado  idadi  kwenye  ngazi  za  maamuzi  ni  kidogo.

Kati ya hao, ni asilimia 21.14 tu kwa wanawake 71 waliojitokeza kugombea udiwani.

Kwa nafasi ya uwakilishi wanawake waliogombea ni 251, wakiwemo wanaume 190 na wanawake 61, ambapo walishinda wanaume 42 na wanawake nane (8) sawa na asilimia 16, wabunge walioshinda wanawake ni wanne sawa na asilimia 8,

Takwimu za uongozi za vyama vya siasa zilizokusanywa mwaka 2024 na afisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania ,kwani, zimeonesha hadisasa kunavyama vitatu tu ambavyo wenyeviti wanawake ambavyoni CCM, ACT_ wazalendo na SAU.

Aidha kwa nafasi za Makatibu Wakuu pia nivyama vitatu (3 ) tu ndio vyenye Makatibu Wakuu wanawake ambavyo ni CCK, UNDP na NCCR_Mageuzi.

Kwa  Pemba ambako kuna Wilaya nne na Mikoa miwili, ni  vyama  vinne (4) tu,  ndivyo vinamakatibu  wanawake  wa  mikoa,  ambavyo ni, TLP,  NRA,  NLD,  na  CHAUMA  .

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO