Hemedi alitwisha mzigo shirika la Nyumba la Zanzibar

 


                         Na Fatma Hamad- Pemba

Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar  Hemed  Suleiman Abdulla ameliagiza Shirika la Nyumba  kuendelea kujenga majengo ya kisasa katika mji wa Chakechake, ili uweze kuendena na mazingira ya sasa.

Makamo huyo ameyasema hayo wakati akifungua Nyumba za biashara na maakazi huko Mkungumalofa Chakechake  Mkoa wa  Kusini  Pemba.

Amesema  Serikali  ya  awamu ya nane, imedhamiria kujenga  majengo ya kisasa  katika  miji  yote  ya Zanzibar, ili kuona wananchi wake wanaishi katika majumba zenye hadhi na zenye kuvutia.

‘’Chakechake  ndio mji mkuu wa Pemba, nikuombe waziri wa Ardhi  kuhakikisha Chakechake  imebadilika, nakua mji wa kisasa,’’ameagiza.

Amesema majengo hayo ya kisasa yatawanufaisha wananchi kupata makaazi bora, pamoja  na wafanyabiashara wote, hivyo ni budi jamii kutoa mashirikiano na Serikali ili kuona majengo hayo yamesimama.


Aidha amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu, ili Nchi izidi kupiga hatua kimaendele.


 Mapema  waziri wa  Ardhi  nyumba na makaazi Zanzibar  Rahma Kassim Ali amesema,  wataendelea  kujenga majengo ya kisasa,  kili kuona miji  yote  ya  Zanzibar  inakua na hadhi.

 Akitoa tarifa ya kitaalamu Katibu mkuu wizara  ya Ardhi na maakazi Zanzibar  Khadija  Khamis  Rjab  amesema,  Jumla  ya  shilingi  Bilioni  moja  ishirini na sita zimetumika  kwa  ajili  ya ujenzi  huo, ikiwa ni  pamoja na kulipwa  mjenzi  na mshauri elekezi.

Amesema nyumba hiyo  yenye  Gorofa  nne inanyumba nane za maakazi  zenye  vyumba  vitatu,  Maduka 20  ilijengwa na Mkandarasi  wa  kampuni  ya  Zanzibar  Hause Coporation kwa kupitia  mshauri  elekezi  wakala  wa  majengo  Zanzibar  ZBS.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid amesema   Mkoa  wake  utaendelea  kuunga  mkono jitihada za Rais wa Zanzibar,  ili kuhakikisha  amani na maendeleo  yanaendelea  kupatikana  Mkoani  humo.







Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO