Mitazamo finyu ya jamii inavyowakosesha fursa za uongozi, wanawake

 


                             Na Fatma Hamad-Pemba

Kwa mujibu wa Sensa  ya  watu  na  makazi  ya  mwaka  2022  Zanzibar  inawanawake wengi  ambao  ni  974,281  sawa  na  asilimia  51.6  kuliko  wanaume, ikiwa  wao  ni  915,492  sawa na  48.4  ambapo  licha  ya  uwingi  huo bado  idadi  kwenye  ngazi  za  maamuzi  ni  kidogo.

 licha ya uwingi huo bado idadi ya wanawake wanaojitokeza na kugombea  Kati ya hao, ni asilimia 21.14 tu kwa wanawake 71 waliojitokeza kugombea udiwani.

Kwa nafasi ya uwakilishi wanawake waliogombea ni 251, wakiwemo wanaume 190 na wanawake 61, ambapo walishinda wanaume 42 na wanawake nane (8) sawa na asilimia 16, wabunge walioshinda wanawake ni wanne sawa na asilimia 8,

Hata katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 21 (1) kinaeleza  kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke  na Taifa lake. 

Hata  Sera  na  Sheria  mbalimbali  za  Zanzibar  zimeelekeza  kutambua  haki  ya  mwanamke  kushiriki  katika  demokrasia  na  uongozi.

Ijapokua  wanawake wamepewa fursa ya kugombea na kushika nafasi mbalimbali za mamuzi, lakini bado Jamii inaonekana haikotayari  kuwachagua  viongozi  wanawake, na hii ni kutokana na mitazamo finyu inayojengeka kwa wananchi.

 Hivyo  basi  Makala  hii  imezungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali  kisiwani  Pemba na kutaka kufahamu, ni kwanini  Jamii  haikotayari  kuwachagua  viongozi  wanawake.

SABABU  ZINAZOPELEKEA  JAMII  KUTOKUWACHAGUA VIONGOZI  WANAWAKE

   JAMII  

Fatma Mohamed Shaaban mkazi wa Penjewani wilaya ya Wete Pemba,  anasema jamii iko tayari kuwachagua viongozi wanawake, ila kinachowatia hofu kuwachagua, ni kwamba wengi wanaogombea hawana sifa.

Anasema wanawake wengi hawana utayari, na wengi wao hawashiriki kwenye vikao vya vyama.

‘’Wale  wanawake wenye sifa hasa na wenye uthubutu wa kusimama mbele za watu na kuweza kutetea mambo ya kimaendeleo, hawajitokezi kusimama majimboni na kugombea’’, anaeleza.

Juma Kombo Hija mkaazi wa Micheweni anasema jamii haikotayari kuwachagua viongozi wanawake, kwa sababu waliowengi hawataki kuongozwa na wanawake.

‘’Hadi leo wapo baadhi ya watu wanamawazo finyu,  hawapendi  mwanamke ashike nafasi ya juu, wanataka sikuzote wawe ni watu wa kukaa mkiani,’’anaelza.

Fatma Rashid mkaazi wa Sizini wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba anasema Jamii hawako tayari kuwachagua viongozi wanawake,  kwa  sababu bado hao wanawake wenyewe  wanasuasua, hawajakua kitu kimoja juu ya masuala ya uongozi.

‘’Tulitarajia anaposimama mwanamke mwenzetu  jimboni ashinde, kwa sisi  wanawake tuko wengi ni , lakini chakushangaza hata sisi  wenzake tunamsaliti, tunawafanya  wanaume kilan siku kua mbele wao,’’anasema.

   VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Maryam Saleh Juma  ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama cha Ukombozi wa Umma  (CHAUMA) anasema jamii  wanaogopa kuwachagua  wanawake,  wanadai kua hata wakiwachagua hawapati  nafasi.

‘’Hata mwanamke akashinda anapigwa vita alimradi asipite, wanaume bado hawajawakubali wanawake kushika uongozi,’’anaeleza.

Abass Mohamed Khatib Mratib wa Chama cha Demokrasia Makini (DP)  anasema  jamii haikotayari  kuwachagua viongozi wanawake  kwa  sababu wengi wanaogombea hawana uwezo wa kusimamambele  za  watu  na  kuzungumza.

Anasema wengi wa wanawake hawashuki chini kwenye matawi na kufanya shughuli za chama na kuweza kujijengea uzoefu.

‘’Wengi wa  wanawake wanajificha wanasubiri kipindi  cha uchaguzi ndo wanakuja majimboni  kwa  kujaza   fomu  tu  za kugombea, hawana ule uzoefu wa kuzungumza na watu,’’anafafanua.

Anasema jamii inahitaji mtu ambae ataweza kusimama na kuwatetea shida zao, na sio kuchagua  kiongozi  kwa kua ni mwanamke  mwisho wa siku akaishia mpiga kofi kwenye meza.

WANASHERIA

Khalfan Amour Mohamed mwanasheria wa kujitegemea kutoka wilaya ya  Chakechake  Mkoa wa Kusini Pemba, anasema wanchi hawakotayari kuwachagua viongozi wanawake, kwani wengi wa wanawake wanaogombea hawana sifa za kugombea, hawashiriki ipasavyo shughuli za chama.

Anasema wanawake walio na sifa za kugombea hawajitokezi matawini na kushiriki harakati za kwenye vyama wakaweza kuonekana.

‘’Kiukweli  hasa  wale wanawake  wasomi  wenye  uthubutu hawajitokezi  kwenye  shughuli  za  vyama, wanajificha, wanawahamasisha wengine kugombea ambao hawanasifa, jee wananchi watawachagua, anasema khalfan.

Anasema ipo haja kuwekwa mifumo mbadala kwenye siasa ili kuona wanawake walio na elimu wanajitokeza kwenyeshughuli za vyama bila ya khofu, jambo litalopelekea kupata nafasinyingi za uongozi kwa wingi.

Saleh  Hamad  Juma  ni  kaimu  Mkurugenzi  wa  Jumuia ya wasaidizi  wa  Sheria  wilaya  ya  Micheweni  Mkoa  wa  Kaskazini  Pemba,  anasema  yeye  anaona  kiongozi  mwanamke ni  bora  kwani sikuzote  anaejua utungu wa  mwana  ni  mama.

‘’Tukiangalia  hata  Raisi  wetu  wa  mungano ni  mwanamke,  na tunamuona  anvyofanya  vizuri  licha ya uwanawake wake maendeleo  yanapatikana,’’amefafanaua.

WANAHARAKATI

Semeni Ali Khamis mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto Wilaya ya Micheweni  anasema,  ili kufikiwa  lengo la  hamsini  kwa  hamsini  ya  uongozi. ipo haja kwa wanawake kukaakitu kimoja na kuungana mkono,  kuhakikisha wanaingia kwa wingi majimboni  katika  Uchaguzi  mkuu  wa  2025.

Amina Ahmed Mohamed ni kaimu Mratibu wa Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar  (TAMWA ) Ofisi ya Pemba,  anasema  wamekua wakitoa  elimu  siku hadi siku  kwa  wanawake  juu ya masuala ya uongozi, ili kuona wanakua kitu kimoja,  na  kuona wanajichukulia nafasi mbalimbali za maamuzi.

WACHAMBUZI WA MASUALA YA HABARI

Bakar Mussa Juma ni mwenyekiti wa Jumuia ya wandishi wa habari kisiwani Pemba anasema kiongozi mwanamke ni bora kwani, maranyingi yeye ndo anakua karibu zaidi na Jamii.

‘’Mara nyingi mwanamke yeye ndo anakua karibu na wananchi, inakua ni rahisi kuzifahamu shida zinazowamkubwa,’’anafahamisha.

 

 

 

 

 

 

 

 


Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI