Wanawake wawagaragaza wanaume, katika kamati za uhifadhi mazingira za shehia
Na Fatma Hamad- Pemba
Rais Samia Suluh Hassan wa Tanzania, mara baada ya kula kiapo Machi 19,
2021, alitaja moja ya vipaumbele vyake, ni kuyashirikisha makundi mbali mbali
wakiwemo wanawake.
Na ndio maana wapo mawaziri kadhaa wanawake wanaoongoza Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiwemo waziri wa Afya Jenister Mhagama, na mwenzake Ashatu Kijaji anashikilia wizara ya Mifugo na
uvuvi.
Lakini hata wizara ya Fedha na mipango, inashikiliwa na mwanadada Natu Elmaamry Mwamba kwa nafasi ya Katibu
Mkuu wa wizara hiyo.
Eneo jingine ni uwepo wa sera ya taifa ya Jinsia na maendeleo ya mwaka
2023/2033 ambayo nayo imehimiza, uzingatiaji wa haki na usawa wa kiuchumi kwa
wanawake na wanaume.
Kwa Zanzibar katiba ya mwaka
1984, kifungu cha 10 (e) kimeleza kila raia atakuwa na haki sawa, majukumu na
fursa sawa kwa mujibu wa sheria.
Ndani ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Wwatoto Zanzibar ya mwaka 2024/2025 ikaubua kuwa, tafiti
zinaonesha kuwa nchi zinazozingatia usawa wa kijinsia zimeweza kuimarika
kiuchumi kwa kasi kuliko, ambazo
hazizingatii usawa huo.
Kimataifa ripoti ya ‘UN Women’ na ECOSOC ya Septemba 2023, inatoa wito wa ufadhili
kwenye programu za kuhamasisha usawa wa jinsia.
Kwa kuzingatia hilo, wenzetu
wa Jumuia ya uhifadhi wa misitu Pemba ‘CFP’ wakishirikiana na wenzao wa
kimataifa ‘CFI’ kwa ushirikiano na Chama cha wandishi wa habari wanawake
(TAMWA) Zanzibar, katika mradi wa
uhifadhi mazingira, wakalenga zaidi
wanawake, ili kutekeleza azma ya usawa.
UZINGATIAJI
USAWA WA JINSI KAMATI ZA HIFADHI YA MAZNGIRA
Kamati za shehia nne za
wilaya ya Wete Pemba, ambapo mradi wa
mabadiliko tabianchi, umebisha hodi, utafiti unaonesha utekelezaji wa sera ya
jinsia kwa vitendo.
Maana ndani ya kamati hizo,
ambazo zinatekeleza mradi huo, zimefanikiwa kutekeleza sera kwa vitendao, kwani kati ya wajumbe wote 110 wanaounda kamati
hizo, wanawake ni 68 sawa na asilimia 0.68 ya wajumbe wote.
Kwenye shehi hizo za Kambini
kichokochwe, Mchanga mdogo, Chwale na Mjini kiuyu, mradi huo, ulilazimisha
kuanzishwa kwa kamati hizo.
Jambo zuri kwenye kamati hizo
zenye lengo la kukabiliana na mabadiliko tabia nchi, sambamba na kujiongezea
kipato, wanawake wapo 68 na wanaume na wanaume 33.
Hili ni jambo jema, kwa jamii na wanaouendesha mradi huo ambao ni Jumuia ya uhifadhi wa misitu Pemba ‘CFP’ wakishirikiana na wenzao wa kimataifa ‘CFI’ kwa ushirikiano wa karibu na TAMWA Zanzibar kwa ufadhili wa Serikali ya Canada, na kuridhiwa na Serikali ya Mapinduzi.
HAYA
YALIKUJAJE KWA WANAWAKE KUWA WINGI
Bakar Hamad katibu wa kamati
ya upandaji wa mikoko ya Kambini kichokochwe, anasema kamati yake inawajumbe
55, wanawake 31 na wanaume 24.
Anasema wanawake ndio wahanga
wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi, hivyo unapomuelimisha na kumpa nyenzo yuko
tayari kuhakikisha anayatunza mazingira, ili awe salama.
‘’Yanapotokea mafuriko
wanawake hua ndo wahanga wakubwa, na ndiomaana mradi ukalenga kwa wanawake zaidi,’’anaeleza.
Fatma Shaaban Mohamed ni kiongozi wa kamati ya kilimo msito Shehia ya Mjini kiuyu, anasema katika kamati yake ana wajumbe 25 wanawake 20 wanaume watano sawa na asilimia 0.05.
Anasema anampango wa kuongeza
tena wajumbe wanawake kwani,
alishaona kilimo msitu
kitawasaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
‘’Ukilima kilimo mseto, katikashamba hilo moja, utavuna mazao
utakula, utauza, utapata kuni, na utaepusha mmon’gonyoko wa ardhi,’’anaeleza.
Anu Omar Juma ni kiongozi wa Kamati ya uhifadhi wa mazingira, inayojishughulisha na kilimo mseto ya Mchanga mdogo, ina wajumbe sita (6) wote ni wanawake.
Anasema hajashirikisha
wanaume, kwani anahisi athari za
mabadiliko ya tabianchi, wathirika zaidi ni wanawake.
‘’Wanawake ndio wanaohangaika
kutafuta kuni,hivyo wakilima kilimo msitu wataepuka kukata miti kiholela, itakua wanazipata
katika mashambayao,’’anaeleza.
Ali Juma Mbarouk kiongozi kutoka Chwale anasema kamati yake ya kilimo msitu, ina wajumbe 15 kati ya hao, wanawake ni 11 na wanaume ni wanne (4).
Anasema ameamua
kuwashirikisha wanawake wengi, kwasababu wao ndio wanahitaji zaidi elimu ya
mabadiliko ya tabianchi.
‘’Elimu ya mabadiliko ya
tabia nchi inaweza kuinua kipato cha wanawake, kwani wanaweza kulima kilimo cha
biashara na kujingizia kipato,’’anasema.
Asya Abeid Said mwanakamati wa Mjini kiuyu, anasema siku zote
panapokuwepo na kiongozi mwanamke ni rahisi kufanikiwa.
‘’ Kwa vile mradi huu umempa
fursa kubwa mwanamke, naamini athari zitokanazo na uharibifu wa kimazingira
zitapungua kwa kiasi kikubwa,’’anafafanua.
Bakar Amour nae ni mwanakamti
ya Mchanga mdogo anasema, mradi wa mabadiko ya tabianchi, utawajenga wanawake,
kua na uthubutu wa kushiriki katika nafasi yeyote ya uongozi.
‘’Walipoelimishwa na
wakafahamu sababu za uharibifu wa mazingira, nasubutu kusema kumeundwa kamati
hakuna anayeweza kukata mikoko,’’anasimulia.
Maryam Khamis Bakari
mwenyeulemavu wa uziwi mwanakamati Mchangamdogo, anasema anapokuepo kiongozi
mwanamke, hupatikana mabadiliko.
‘’Kunapotokezea tetemeko la
ardhi, mafuriko na mimi yananikumba, ndio wakanishirikisha kwenye kamati yake
ili niweze kufahamu mabadiliko ya hali ya hewa,’’anasema.
Mafunda Haji Khatib kutoka
shehia ya Chwale anasema wameona faida ya kuwa na kiongozi mwanamke, kwani
wengi shehiani mwao wamekua na mwamko wa kulima kilimo msitu.
‘’Tunashuru mwanamke mwenzetu
kwa kutupa elimu ya utunzaji wa mazingira, na sasa tunapanda miti, ili tuweze
kukabiliana nayo,’’anasema.
JAMII
Maryam Abdala Hamad mkaazi
wa Chwale amesema, kiongozi mwanamke ni
bora, kwani mara nyingi ndio yuko karibu na jamii yake.
Kombo Khatib Bakar mkaazi wa
Mjinikiuyu, anafahamisha kuwa, mwanamke ni mpenda mabadiliko, hivyo unampompa
nyenzo anaweza kufanikiwa.
‘’Walipatiwa elimu ya
utunzaji mazingira wanawake wachache, ila niseme wengi wao sasa hivi wametafuta
mashamba wanalima kilimo mchanganyiko,’’anafafanua.
WANAHARAKATI
Hafidh Abdi Said kutoka jumuiya ya utetezi wa kimazingira na jinsia Pemba ‘’PEGAO ’’ anasema kwa baadhi ya tasisi tayari wamekuwa na
uwelewa wa kuitekeleza Sera ya jinsia, kwani wanawashirikisha wanawake katika miradi
ya kimaendeleo.
Nairat Abdullah Ali, kutoka Chama cha
wandishi wa habari wanawake (TAMWA) Zanzibar, anasema mradi huo wa uhifadhi mazingira, utainua kiapato cha
wanawake sambamba na kuepukana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mbarouk Mussa Omar Mkurugenzi
wa Jumuiya ya uhifadhi wa misitu Pemba (CFP), anasema kupitia mradi huo wamewekeza zaidi kwa wanawake, kwani athari ya
mabadiliko ya tabianchi inawaumiza zaidi.
‘’Tunataka kila penye watu
100 basi 80 iwe wanawake ambao wanafahamu athari za mabadiliko ya tabianchi na
jinsi kukuabiliana nayo,’’anafahamisha.
VIONGOZI
WA DINI
Sheikh Said Ahmed Mohamed
kutoka Ofisi ya Mufti Pemba anasema, uislamu umemruhusu mwanamke
kushiriki katika fursa yoyote ya kimaendeleo, anayoiweza kwa mujibu wa dini.
Mchungaji Yohana Ali Mfundo
wa Machomane Chake chake, amefahamisha kuwa katika dini yao hakuzuiwa mwanamke asishiriki kwenye miradi ya
kimaendeleo.
NINI
KIFANYIKE.
Sheha wa Kambini kichokochwe,
Ali Omar Ali anasema, ni vyema na miradi
mengine ya maendeleo inayokuja kuiga
mfano huo, kuhakikisha wanazingatia
usawa.
Si jambo geni wanawake kuonekana wengi katika kamati hizo za
uhifadhi mazingira, kwani hata Sensa ya
watu na makizi ya mwaka 2022 Zanzibar
imeonekana kua na wanawake wengi dhidi ya wanaume
Lakini hata kwa shehia ya Mchangamdogo yenyewe inayo wanawake 2385
huku, wanaume wakiwa 2207 kamailivyo shehia ya Kambini
kichokochwe inayowanawake, 2067 na wanaume 1938.
Comments
Post a Comment