Posts

Jamii yatakiwa kuwacha tabia ya kuwaficha wadhalilishaji

Image
                                             NA FATMA HAMAD,PEMBA Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya ameitaka Jamii kuwa mstari wa mbele kutoa mashirikiano kwa   vyombo vya Sheria wakati kunapotokea vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia Vijijini mwao. Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akifungua kongamano maalumu la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto, ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Sauti ya Vijana [Youth   Voice Oganization] lililofanyika Tumbe Mashariki wilaya ya Micheweni Pemba. Amesema suala la udhalilishaji bado ni tatizo ambalo linaendelea kuiathiri Jamii, hivyo ni wakati kwa jamii kuacha muhali na kuvunja ukimwa kusimama kidete kutoa ushahidi ili kuona wahalifu wanaotenda makosa hayo wanatiwa hatiani jambo ambalo litao...

JAMII YATAKIWA KUWACHA TABIA YA KUWAFICHA WADHALILISHAJI

Image
                              NA FATMA HAMAD,PEMBA Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya ameitaka Jamii kuwa mstari wa mbele kutoa mashirikiano kwa   vyombo vya Sheria wakati kunapotokea vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia Vijijini mwao. Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akifungua kongamano maalumu la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto, ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Sauti ya Vijana [Youth   Voice Oganization] lililofanyika Tumbe Mashariki wilaya ya Micheweni Pemba. Amesema suala la udhalilishaji bado ni tatizo ambalo linaendelea kuiathiri Jamii, hivyo ni wakati kwa jamii kuacha muhali na kuvunja ukimwa kusimama kidete kutoa ushahidi ili kuona wahalifu wanaotenda makosa hayo wanatiwa hatiani jambo ambalo litaondosha vitendo hivyo viovu ndani ya jamii. ‘’Nashangaa sana eti unamuonea huru...

WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI WALIA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI.

Image
                                                NA FATMA HAMAD, PEMBA Jamii imetakiwa kuwafichuwa wahalifu wanaowafanyia vitendo vya udhalilishaji watu wenye ulemavu wa akili ili kuona wanatiwa hatiani. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Chake chake Mratibu wa Jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili kisiwani Pemba Khalfan Amour Mohd amesema wapo watu wamekuwa wakimaliza matamanio yao kwa kuwafanyia udhalilishaji watu wenye ulemavu wa akil. Alisema ni vyema jamii kuwafichua watendaji wa matendo hayo ili kuona wanatiwa hatiani jambo ambalo litapunguza udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu wa akili. ‘’Wapo watu wamekua wakiwadhalilisha wenye ulemavu wa akili na badala yake kukimbia, wakijidai hawawezi kukamatwa kwa vile wanaowafanyia h...

WATU WENYE ULEMAVU WAIOMBA SERIKALI KUONDOSHA VIKWAZO KWENYE MIKOPO.

Image
                                            NA FATMA HAMAD,PEMBA VIKUNDI vya Ushirika vya Watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba vimeiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwaondeshea vikwazo kwenye suala la upatikanaji wa Mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi ili kuona watu wenye ulemavu nawao wananufaika na fursa hiyo. Hayo yamesemwa na Omar Kombo Hamad kutoka kikundi cha Twamshukuru Allah kilichopo   mbuzini na Fatma Salim Hamud wa kikundi cha Nia njema   kutoka Ole kianga cha watu wenye ulemavu mara baada ya kumaliza mafunzo ya ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo Mafuta ya mgando ya mwani, mafuta ya mkaratusi pamoja na Jiki huko Ole mihogoni Chake chake Pemba.   Walisema ili kuona watu wenye ulemavu wananufaika na fursa mbali mbali zilizomo kwenye Serikali, nivyema   kupatiwa mkopo   kwa mtu mmoja mmoja   na isi...

SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA HOSPITALI, KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA

Image
                                              NA ZUHURA JUMA, PEMBA   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kujenga hospitali na vituo vya afya vyenye vifaa vya kisasa ili kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.   Akizungumza wakati akifungua hospitali ya Wilaya iliyopo Kinyasini Wilaya ya Wete, Dk. Mwinyi alisema tayari zimeshajengwa hospitali  za Wilaya kwa unguja na Pemba huku Serikali ikiendelea kujenga hospitali za mikoa, rufaa na mwanzo (dispensaries na vituo vya afya) ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila ya usumbufu.   Alisema kuwa, ujenzi wa hospitali hizo na vituo vya afya vitawapunguzia wananchi kwenda masafa marefu kuifuata huduma hiyo, sambamba ya kupata huduma bora kutokana na vifaa vya kisasa vilivyowekwa.   "Tutahakikisha tu...

Dk. Mwinyi ataka usafi kwenye miji uimarike

Image
NA ZUHURA JUMA, PEMBA RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amezitaka Halmashauri, Mabaraza ya Miji na Manispaa kudumisha usafi katika miji, ili kuiweka katika mazingira bora na haiba ya kuvutia.   kizungumza wakati akifungua kituo cha wajasiriamali Kifumbikai Wete pamoja na stendi ya Kinowe Konde Dk. Mwinyi aliziagiza taasisi hizo mambo matano, ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika miji, kujenga masoko, vituo vya ujasiriamali, maegesho na viwanja vya kufurahishia watoto ambayo hayo yatasaidia kuweka mazingira bora na mazuri.   Alisema kuwa, usafi ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, hivyo ni wajibu wao kudumisha katika maeneo ya miji, kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri na ya kuvutia.   "Tumebadilisha ugatuzi ili taasisi hizi ziweze kufanya kazi zake vizuri ikiwa ni pamoja na suala la kuimarisha usafi katika miji yetu, hivyo mna wajibu wa kuyatekeleza kwa vitendo ili kuimarisha maisha ya wananchi," alisema Rais Mwinyi. ...