WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI WALIA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI.
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Jamii imetakiwa kuwafichuwa wahalifu wanaowafanyia vitendo vya udhalilishaji watu wenye ulemavu wa akili ili kuona wanatiwa hatiani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Chake chake Mratibu wa Jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili kisiwani Pemba Khalfan Amour Mohd amesema wapo watu wamekuwa wakimaliza matamanio yao kwa kuwafanyia udhalilishaji watu wenye ulemavu wa akil.
Alisema ni vyema jamii kuwafichua watendaji wa matendo hayo ili kuona wanatiwa hatiani jambo ambalo litapunguza udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu wa akili.
‘’Wapo watu wamekua wakiwadhalilisha wenye ulemavu wa akili na badala yake kukimbia, wakijidai hawawezi kukamatwa kwa vile wanaowafanyia hawana kumbu kumbu, alisema.
Alisema kwa mwezi wa Novemba hadi Desemba 3 mwaka huu katika ofisi yao wamepokea jumla ya matukio manne [4] ya udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu wa Akili ndani ya wilaya ya moja ya Chake chake, ambapo matukio matatu yapo mahakamani na moja lipo Polisi linaendelea na upelelezi .
Kwa upande wake Hidaya Mjaka Ali kutoka Jumuia ya Umoja wa watu wenye ulemavu Ofisi kuu Pemba alisema licha ya juhudi zinazochukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo, lakini bado watu wenye ulemavu hususan wa akili wamekuwa wakiathirika zaidi na udhalilishaji.
‘’Jami imekuwa akiwachukulia wenye ulemavu wa akili kama ni watu wasio na faida yoyote katika taifa hili,hata akidhalilishwa hakotayari kutoa mashirikianouna juu ya kesi hizo,alisema.
Alisema unapomdhalilisha mwenye ulemavu wa akili unazidi kumuathiri kutokana na hali zao walizo nazo, kwani wao wanakua hawawezi kujieleza wenyewe ja kupelekea kukosa haki zao.
Walisema kuwepo kwa siku 16 za kupinga udhalilishaji ni jambo la msingi kwani kunawafanya wenye ulemavu kutoa changamoto zao mbali mbali zinazo wa kwaza,katika maisha yao.

.jpg)
Comments
Post a Comment