WAVUVI WATAKIWA KUTUMIA ZANA MBADALA KULINDA RASILIMALI BAHARI

NA FATMA HAMAD, PEMBA 

 AFISA MRADI wa Kuimarisha Uvuvi endelevu na usimamizi wa Mazao ya Bahari TASFAM Salma Sururu Juma amewataka wananchi wanaofanya shughuli za  Uvuvi kuhakikisha wanafanya shughuli hizo wanatumia zana za kisasa ambazo zinaruhusiwa kisheria, ili kulindavrasilimali za Bahari na kuona zinakua endelevu. Wito huo meutoa wakati akizungumza na Maafis Uvuvi na wadau wanaosimamia shughuli za Uvuvi, katika mkutano wa kuutanbulisha Mardi huo wa kuimarisha Uvuvi endelevu na usimamizi wa Mazao ya Baharini TASFAM huko ukumbi wa wizara ya Fedh Gombani Chakechake Kusini Pemba.

 Alisema bila kutumia  zana za kisasa na zinazokubalika kisheria, sio rahisi rasilimali Bahari zikaweza kuhifadhika na kua endelevu. Alisema lengo la Mardi huo ni kuhivadhi Mazao ya Bahari, hivyo ipo haja kwa maafisa Uvuvi kusimamia ipasavyo kuona wavuvi na wanaofanya shughuli za abaharini kuwa na zana zinazokubalika, ili lengo liweze kulengo lifikiwe na kuona serikali inaingiza kipato kupitia Mazao ya Baharini.

 “Kama hatutotumia zana zilizombadala hatutopata kitu na hatutoweza kujiingizia kipato,”alisema.

 Shafii Khamis Sudi kutoka Uchumi wa Buluu na Uvuvi Idara ya Maedeleo na Uvuvi alisema Mradi wa TASFAM utawaezesha wavuvi pamoja wakulima wa Mwani wanaotumia kina kidogo cha Maji, na wafikie kina kikubwa, ili wazalishe Mazao kwa Wingi,''alisema

''Tunaimani kwamba MRadi huu utakua chanzo Cha mabadiliko na kujiinua kiuchumi kwa wavuvi pamoja na wale wote wanaofanya shughuli za uhifadhi wa Mazao ya Bahari,’alisema

. Shaaban Ngwabila kutoka Shirika linaloshughulikia Mazao ya Baharini, alisema watahakikisha wanashirikiana na Mradi huo na kuondosha baadhi ya changamoto zinazowakaza wavuvi ikiwemo kuwapata Maboti ya kisasa kwa ajili ya Uvuvi. 

 ‘’Mradi huu utasaidia wavuvi kupata zana za kisasa pamoja na Boti za uokozi pindi itakapotokezea dharura wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi,’’alisema. 

 Nao Maafisa hao walisema watahakikisha wanasimamia ipasavyo, ili kuona rasilimali Bahari zinatunzwa na zinabakia katika uhalisia wake. 

 Nae Afisa Mdhamini wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi DK Salim Mohamed Hamza aliwataka aliwataka Maafisa hao kuhakikisha wanatoa ushirikiano bega kwa bega na Mradi huo, kuona unatekelezeka ipavyo na rasilimali bahari zinabakia salama. 

 Mradi huo ambayo  unatekelezwa na  Wizara ya Uchumi wa buluu Zanzibar, wizara yaMifugo na Uvuvi MLF Tanzania, na Dee Sea Fishing, Authority  DSFA Tanzani. 

 Ambapo atatekeleswa kuanzia 2025 hadi 2030 kwa ufadhili wa benk ya dunia. Unaolenga kuongeza uzalishaji wa thamani ya mazao ya baharini pamoja na kuimarisha upatikanaji wa masoko na uhifadhi wa rasilimali hizokwa manufaa wa kizazi cha sasa na kijacho.

 MWISHO..



Comments

Popular posts from this blog

WANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA UCHAMBUZI

NAJIVUNIA KUONA WANANCHI WA MJINI KIUYU WAKIKANYAGA BARABARA YA LAMI

HOFU YA UDHALILISHAJI MTANDAONI INAVYOWANYAMAZISHA WANAWAKE