UCHUMI WA BULUU YAJA NA MRADI WA KUIMARISHA UVUVI ENDELEVU



Sekta ya uvuvi, ufugaji wa samaki na kilimo cha mwani iznaendelea kuwa nguzo muhimu ya ajira na kipato kwa wananchi wa Zanzibar huku Serikali na taasisi binafsi ikiweka mkazo katika matumizi ya rasilimali za baharini kama fursa ya biashara na uwekezaji. 

 Hayo yalisemwa na Afisa Mdhamini wizara ya Uchumi wa Buluu DK Salim Mohamed Hamza wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Mradi wa Kuimarisha Uvuvi Endelevu na Ufugaji wa Mazao ya Baharini Tanzania, TASFAM, huko katika ukumbi wa ZRA Gombani Chakechake Kusini Pemba.

 Alisemesema ushirikiano wa wadau ni muhimu katika kuongeza uzalishaji, ajira na kipato kwa wananchi. ALisema kwa Sasa serikali imeelekeza zaidi katika sekta ya Bahari, hivyo imeamua kuleta Mardi huo wa kuimarisha usimamizi endelevu wa uvuvi na ufugaji wa mazao baharini, ili wadau waunge mkono Mradi huo na lile lengo la serikali liweze kutimia la kujipatia kipato kupitia Bahari.

 "Nyinyi wadau mnaoshughulika na masuala ya Bahari mnamchango makubwa, hivyo tumeamua kuwaita muweze kufanya kazi na sisi, ili Mardi uweze kufanikiwa na Kupatikana kwa maedeleo yanayohitajika,"alisema. 

 Alisema lengo hasa la mkutano huo ni kuutanbulisha Mardi huo, uweze kufahamika na kuona Kila mdau anaelekeza nguvu zake, ili Kupatikana kwa matunda ambayo yataifadisha jamii na serikali kiujumla.

 Kwa upande wake Mratibu wa Mardi wa TASFAM, Mohammed Said Khamis, alisema mradi huo utatowa fursa mbalimba zinazotokana na rasilimali za baharini ambazo zitawanufaisha wananchi,

 "Niseme kwanba Mardi huu utakuza zaidi uchumi wa wananchi wanaoishi katika maeneo ya ukanda wa pembezoni mwa Bahari,"alieleza. 

 Aidha alifahamisha kwamba Mardi huo pia utasaidia uimarishwaji wa kukabiliana na kupambana na masuala ya mabadilikotabia nchi, jambo ambalo kimekua liikiathiri jamii. 

 Akiwasilisha mada katika mkutano huo afisa tathmini kutoka mradi huo Daudi Haji Pandu alisema TASFAM inalenga kuwasaidia wananchi kutumia rasilimali za baharini kama chanzo cha ajira, biashara na uwekezaji husasani kwa wakaazi wa maeneyo ya ukanda wa bahari.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar, Mussa Ramadhan Said alisema, Mardi huo utahakikisha unamnufaisha kila mtu awe kijana, mzee,mwanamke ama mwanamke.

 "Kwakweli Mardi wetu huu utakuza ni chachu ya mabadiliko kwa watu wote, utahakikisha haumuachi mtu nyuma,'alieleza.

 Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano huo walisema ni vyema jamii iendelee kupewa elimu zaidi juu ya dhana ya Uchumi wa buluu iweze kufahamu, na kuweza kuchangamkia fursa zitokanazo na sekta hiyo.

 Sambamba na hilo walisema ni vyema kuzingatia sera ya Jinsia katika utekelezaji wa Mardi huo, ili Kila mwananchi anufaike na fursa hiyo. Mradi huo ambayo unatekelezwa na Wizara ya Uchumi wa buluu Zanzibar, wizara yaMifugo na Uvuvi MLF Tanzania, na Dee Sea Fishing, Authority DSFA Tanzani.

 Ambapo atatekeleswa kuanzia 2025 hadi 2030 kwa ufadhili wa benk ya dunia. Unaolenga kuongeza uzalishaji wa thamani ya mazao ya baharini pamoja na kuimarisha upatikanaji wa masoko na uhifadhi wa rasilimali hizokwa manufaa wa kizazi cha sasa na kijacho.

 …MWISHO..




Comments

Popular posts from this blog

WANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA UCHAMBUZI

NAJIVUNIA KUONA WANANCHI WA MJINI KIUYU WAKIKANYAGA BARABARA YA LAMI

HOFU YA UDHALILISHAJI MTANDAONI INAVYOWANYAMAZISHA WANAWAKE