‘’TUTAHAKIKISHA TUNAULINDA UTAMADUNI WA ZANZIBAR’’ANASEMA HEMED
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itahakikisha inafanya juhudi mbalimbali kuona utamaduni wa mzanzibari unadumu, ili uweze kuinua uchumi wa vijana wa kizanzibari.
Hayo yalisemwa na Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemedi Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Ali Hassan Mwinyi, wakati akizindua Tamasha la 31 la Utamaduni wa Mzanzibar, huko Gombani wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema Utamaduni wa kizanzibar ni moja ya jambo linalochangia uchumi wa Nchi, hiivyo ipo haja kuendeleza Utamaduni huo ili kuleta ajira kwa vijana wa Zanzibar.
‘’Tutahakikisha tunaulinda utamaduni wetu uweze kudumu, na kuwa kivutio kwa wageni wanaoingia Zanzibar,'alisema.
Alisema Serikali imeshetenga Bilioni 40 kwaajili ya kujenga kijiji cha utamaduni ili wazanzibari wakuze bidhaa zao za kiutamaduni kamavile mapishi ya asili, ikiwemo Vitobwesha, Mkate wa gae, Ugali wa muhogo pamoja na Msambwija ( muhogo wa ndizi).
Aidha Hemed aliwataka Wajasiriamali na Wasanii kuzitumia fursa zilizomo katika Afcon 2027 waweze kujiajiri na kujipatia kipato kitakachoinua Uchumi wao.
Sambamba na hilo aliiagiza Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo kushirikiana na Wizara ya Elimu,na kujifunza mbinu zitakazosaidia kuibua vipaji vya kisanii vitakavyosaidia kulinda Utamaduni huo.
Kwa upande wake Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Riziki Pembe Juma alisema serikali itahakikisha inashirikiana na wadau mbalimbali kuona wanauenzi na kuudumisha utamaduni wa kizanzibari, ili uendelee kubaki kwa wenyewe Wazanzibari.
Nae Katibu Mkuu wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo Mattar Zahor Massoud alisema Serikali itahakikisha inapiga vita vitendo viovu ambambavyo haviendani na maadili ya kizanzibari
"Tutahakikisha tunapinga vitendo viovu vya mporomoko wa maadili, vinavyoenda kinyume na tamaduni zetu alisema,'
Alisema Tamasha hilo la 31 litatoa fursa kubwa kwa wajasiriamali na wasanii pamoja na vijana wa kizanzibari.
Kauli mbiyu ya Tamasha la mwaa huu Utamaduni wetu urithi kwa vizazi vyetu, tumia fursa za Utamaduni kwenye Afcon 2027.
MWISHO
Comments
Post a Comment