MARADI WA MALEZI,MAKUZI YA AWALI YA MTOTO ULIVOBADILISHA MITAZAMO KWA WAZAZI PEMBA

 


NA FATMA HAMAD, PEMBA

WAZAZI NA WALEZI kisiwani Pemba wamesema uwepo wa Mradi wa Malezi,Mkuzi na Maendeleo ya  awali ya mtoto umewasaidia, kwani wameelewa umuhumu wa kukaa karibu na watoto wao na kucheza nao.

Walisema mradi umewazesha kujua  kipindi cha siku 1000 ndicho kipindi pekee mtoto anachohitaji uangalizi zaidi na kuwandaliwa kuwa mtoto bora wa baadae.

Akizungumza katika kikao cha tathmini juu ya mradi huo mzazi Asha kutoka N’gambwa Chake, alisema baada ya kupata elimu ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto amejenga ukaribu na watoto wake na wamekua na uthubutu wa kuiga baadhi ya mambo ambayo wanamuona akiyafanya.

‘’Kwa mfano wakati nikiwa jikoni nikipika nilikua mtoto namuweka mbali kwani nahisi ananikera, ila kwa sasa napika nae na nikimenya mbatata yeye anamenya vitunguu,’’alisema.

Kwa upande wake mzazi Kassim Masoud Hamad kutoka Piki Wete alisema zamani ilikua watoto wake hawakua na ukaribu  nawala hawakisubutu kumueleza shida zao, bali  wakimwambia  mama yao.

‘’Nashkuru elimu hii ya malezi ya makuzi na maendeleo ya mtoto yametubadilisha kwani kwa sasa ninakawaida ya kuwaita watoto wangu na wameondokana na woga wananieleza kila wanachokihitaji bila ya hofu,’’alisema.

Zulekha Othman Omar muhudumu wa afya ngazi ya Jamii kutoka Shungi Chakechake alisema mradi wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto umeleta mapinduzim makubwa katika jamii, kwani wengi wameona ile thamani ya kuwa na ukaribu na watoto wao.

‘’Nilipokenda kwa mzazi Amina Ali (sio jina lake halisi) kwa mara ya kwanza mwenye mtoto wa miezi sita aliniambia hana tabia ya kukaa na kuzungumza wala kucheza nae yule mtoto wake kwani anahisi ni mchanga hafahamu chochote,’’alisema.

Alisema mara baada ya kurudi tena kwa ajili ya kujua maendeleo yao, alisema baada ya kupata elimu amekua akicheza ,nae na amemgundua kwamba anasikia, anafahamu na anafurahia kitendo hicho cha kucheza na mamayake.

Mapema Mratibu wa Madrasa Early childhildhood Programme Zanzibar upande wa Pemba Haji Ali Hamad alisema  kwa mujibu wa Sayansi ya ECD katika kipindi cha awali cha siku 1000 ndicho kipindi muhimu ambacho mtoto anahitajika kupata huduma hizo, kwani ndipo akili ya mtoto  inachukua  mambo kwa haraka.

 ‘’Wazazi niwambie kipindi hichi ndicho cha kuwekeza zaid, kwani akili yake haija beba mambo mengine utakachomfundisha anakishika, kuliko kupiga kelele na wa miaka 16,’’alisema.

Alisema ili mtoto akue akiwa vizuri kiakili anahitaji uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wazazi wake, hivyo ipo haja wazazi kuwakaribu na watoto wao, licha ya pirika za maisha walizonazo.

Mtaalamu kutoka wizara ya Afya Pemba Fadhila Abdulla Abdi alisema mtoto anahitaji kuzungumzishwa kuanzia tokea  akiwa tumboni kwa mama yake.

Alisema kiutaalamu mtoto alietumboni anasikia kila kitu kinachozungumzwa, hivyo ni vyema mama anapokua na ujauzito kuepuka migogoro na kuwa na mawazo mabaya, ili kuzaa mtoto mwenye akili timamu na mwenye afya bora.

‘’ Wazazi wenzangu tuzungumze na watoto wetu kuanzia wakiwa tumboni, na pia mama anapokua na ujauzito anahitajika uangalifu wa hali ya juu (STIRES),’’alisema.

Mradi huo wa Vroom unatekelezwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa kwa Pemba ni wilaya ya Wete na Chakechake, unafadhiliwa na Shirika la Bezos Familiy Fondation, lengo lake ni kutoa uwelewa kwa wazazi na Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii, juu ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto.

Mradi huo ulianza mwakajana na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.



MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA UCHAMBUZI

HOFU YA UDHALILISHAJI MTANDAONI INAVYOWANYAMAZISHA WANAWAKE

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI