ADAIWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MIWILI
KIJANA
SHAAME Ali Hamad anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka (38) mkaazi wa Mchangamdogo
wilaya ya Wete Pemba, ashikiliwa na adaiwa za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye
umri wa miaka miwili na miezi mitatu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwake, mama wa mtoto huyo alisema mtoto
wake alifanyiwa tukio hilo la kinyama akiwa nyumbani kwa jirani yake ambae ni mtuhumiwa.
Alisema,
siku ya Ijumaa ya tarehe 26/06/2026 akiwa nyumbani kwake akifanya shughuli zake,
mtoto wake alikuwa hajamuona muda mrefu, ndipo aliponza kumtafuta na kumuita
kwa jina ingawa hakubahatika kumuona kwa wakati huo.
‘’Nilirudi
nyumbani kuendelea kufua lakini nilifanya wasiwasi na nikaamua kwenda kumtafuta
tena, ndipo nikamkuta amekaa nje ya mlango wa nyumba ya Shaame, akiwa na hali
ya huzuni,’’ alisema.
Alisema,
alimwambia asimame ili waondoke lakini mtoto huyo hakuweza kusimama na akambeba
na kwenda nyumbani kwao na kumueka huku yeye akiendelea na shughuli zake.
Alisema,
baada ya muda mfupi alimuona amelala kifudifudi huku suruali yake aliyokuwa
amevaa ikiwa na uchafu.
‘’Hapo nilishtuka, nikaanza kumuangalia vizuri
na nikaona sehemu zake za siri za nyuma haziko sawa, kwani zinatoka
uchafu,’’alisema.
Mama
huyo alieleza kuwa, baada ya kuona hali hiyo walikwenda kituo cha afya
Kinyikani, na madaktari wakawapa barua ya kwenda kituo cha Polisi Mchangamdogo,
na hapo wakapewa Pf 3 na kwenda hospitali ya wilaya Kinyasini Wete kwa ajili ya
kufanyiwa uchunguzi.
‘’Tulipofika
Kinyasini alifanyiwa uchughuzi na tukaambiwa
kwamba mtoto wetu alishafanyiwa
kitendo cha udhalilishaji,’’ alifafanua mama huyo.
Baba
mzazi wa mtoto alisema, tangu siku ya Ijumaa alipofanyiwa unyama huo, mtoto
wake amekua akitokwa na uchafu, kinyesi bila kuzuilika, na kulazimika
kuvalishwa pempasi muda wote.
‘’Kwakweli
tokea alipopatwa na tukio hilo amekua choo chake hakizuiliki, ilibidi muda wote
tuvalishe pempasi kutokana na athari aliyoipata,’’alisimulia.
Alisema,
licha ya tukio hilo la kinyama bali kuna watu wamekua wakimuendea na kumtaka
wafanye suluhu, ili kesi isiende kwenye vyombo vya Sheria.
‘’Wanakuja watu wasiopenda nguvu za wenzao na
kunipa vitisho nikubali suluhu, ila kwa unyama aliofanyiwa mtoto wangu hilo silikubali,
kama ni ujirani alishaupoteza yeye,’’alisema.
Hivyo
aliiomba Serikali na wanaharakati kusimama imara kuhakikisha hatua kali za
kisheria zinachukuliwa dhidi ya muhalifu huyo, na kuona haki inatendeka.
Sheha
wa Mchangamdogo Assaa Makame Said alikiri kuepo kwa tukio hilo katika shehia
yake na kusema, amelipokea kwa huzuni, huku akiwataka wazazi wa mtoto huyo
kutosikiliza maneno ya jamii kwa ajili ya kuifanyia suluhu kesi hiyo.
Mratibu
wa wanawake na watoto shehia ya Mchangamdogo Mbeu Makame Bakar alisema,
amefurahishwa na kitendo cha wazazi wa mtoto huyo kuwa na mwamko wa kulipeleka
katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
Suleiman
Hamoud Salim ambae daktari kutoka Spitali ya Kinyasini Wete alisema, siku ya
ijumaa aliletewa mtoto huyo aliedaiwa kulawitiwa, na baada ya kumfanyia
uchunguzi aligundua kwamba tupu yake ya nyuma haikua katika hali ya kawaida kwani
alikuta michubuko na alikua akitoka kinyesi na uchafu.
‘’Baada
ya kumfanyia uchunguzi nilikuta michubuko katika tupu yake ya nyuma na huku
akiwa anatoka kinyesi,’’alisema.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) William Mwampagale alisema kuwa, hajapokea taarifa za tukio hilo ingawa
wanapopokea taarifa za matukio kama hayo wanafanya uchunguzi na kuyachukulia
hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuyafikisha mahakamni kwa ajili ya
kuendelea na taratibu.
"Baada ya kupokea taarifa ya tukio, huwa tunaliangalia ikiwa ni muhimu kujulikana kwenye jamii kwa faida yao, basi tunaita vyombo vya habari na kulitolea ufafanuzi lakini ikiwa kwenye umma hakuna umuhimu wa kulitoa kwa maslahi ya jamii, basi tunachukua tu hatua za kisheria tu na sio kutoa kwenye vyombo vya habari," alisema Kamanda huyo.
MWISHO.

Comments
Post a Comment