WANDISHI WA HABARI IELIMISHENI JAMII MATUMIZI YA MITANDAO

 

NA FATMA HAMAD,PEMBA

MTAALAMU WA Masuwala ya Mitandao ua Kijamii kisiwani Pemba Mustafa Mohd Abdul Rabi Moyo amewataka Wandishi wa Habari kuendelea kuielimisha jaamii  hususani  ya wanawake, kufuata  miko na maadili ya mitandao, ili kuepuka kufanyiwa udhalilishaji  mitandaoni.

Mtaalamu huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Chakechake Pemba, alisema imeonekana jamii haina elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao, hivyo ipo haja wandishi wa habari kutoa elimu, ili kuepuka udhalilishaji huo.

Alisema kutokana na kuzuka kwa wimbi la udhalilishaji katika mitandao ya kijamii kwa wanawake, ni budi jamii kuelimika na kufahamu madhara ya udhalilishaji mtandaoni.

Alisema kwa sasa udhalilishaji ambao unatumika zaidi  katika mitandao ni wa mashambulizi ya matusi, na huu unakuja pale mwanamke anapotuma  picha za maungo yake  yakiwa utupu.

‘’Niwambie tu dada zangu, licha kua mnatangaza biashara zenu ila ni vyema mkavaa nguo za stara,  zenye heshima, msiweke picha ambazo zitawapa wahalifu fursa ya kuwadhalilisha,’’alisema.

 Akitaja moja ya athari ambayo anaweza kuipata mwanamke wakati asipotumia vizuri mitandao ya kijamii ni kujiondolea heshima na kupelekea kukosa fursa za maendeleo katika jamii.

 ‘’Inawezekana siku moja mwanamke akajakugombea nafasi ya uongozi hivyo kama atakua hatumii mitandao vizuri inaweza kuja kuwa sababu akakosa nafasi, kwani watu wanaweza kuangalia historia yako na ikaonekana huna historia nzuri,’’alieleza.

 Alisema Teknolojia mpya ya Akili bandia (AI)  inaweza ikatoa mwanya kwa wahalifu kupata fursa ya kuwadhalilisha wengine, hivyo wanawake wahakikishe wanatumia mitandao ya kijamii kwa uwangalifu na uwadilifu wa hali juu.

 Alisema asilimia 70 ya wananchi wa Pemba wanatumia mitandao ya kijamii kwa shughuli zao mbalimbali, hivyo ipo haja kuendelea kuitumia mitandao kwa uwangalifu, ili kuendelea kunufaika na  fursa zilizomo mitandaoni.

 Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi Out Gromic Abock ambae ni mkuu wa Polisi jamii Kaskazini ali sema ipo haja Jamii kuzingatia matumizi sahihi ya mtandao, kwa kuepuka kuangalia maudhui yaliokinyume na kanuni na Sheria za Nchi.

 Aidha alisema ni jamii kujifunza Sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, ili kuepuka kufanya vitendo vinavyokwenda kinyume na Sheria hiyo.

 Mwanaharakati  kutoka Jumuia ya Wasaidiz wa Sheria wilaya ya Micheweni Saleh Hamad Juma, alisema Ili kudhibiti vitendo hivyo, ni vyema kukaimarishwa  kwa sheria za kukabiliana na unyanyasaji mtandaoni, kuongeza elimu ya matumizi salama ya mitandao ya kijamii na kuwawajibisha wanaowadhalilisha wengine.

 Sheria ya Maudhui ya Mtandaoni ya 2020: Inakataza kurusha picha, video za utupu, au kutumia lugha za matusi na kejeli zinazodhalilisha utu.

 MWISHO.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

WANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA UCHAMBUZI

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO