Wazazi watakiwa kuvunja ukimya kwa watoto wao
NA FATMA HAMAD, PEMBA
WASAIDIZI
WA SHERIA wametakiwa kuielimisha jamii kuwa na utaratibu wa kukaa na watoto wao
na kuzungumza nao, waweze kujitambua, ili wajiepushe na vitendo vya
udhalilishaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mradi wa sauti ya mwanamke Hamisa
Bakari Hamad wakati akizungumza na wasaidizi wa Sheria wa wilaya ya Micheweni
katika mafunzo ya Usawa wa kijinsia yaliofanyika kituo cha Uwalimu Wingwi mkoa
wa Kaskazini Pemba.
Alisema katika ulimwengu wa leo wazazi waliowengi wamekosa
utamaduni wa kukaa na watoto wao na kuwafundisha umuhimu wa kujitunza,na kuwa
na khofu ya kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji.
‘’Kuna watoto wamekuwa wakifanyiwa udhalilishaji lakini
wanashindwa kutoa taarifa majumbani kwao, na wazazi wanashindwa kuwagudua
kutokana na kukosa usubutu wa kukaa nao kjenga nao ukaribu,’’alisems.
Alisema ili kuwalinda watoto na vitendo vya udhalilishaji,
ipo haja kwa wasaidizi wa Sheria kuendelea kuielimisha jamii kuvunja ukimya na
kukaa na watoto wao na kuzungumza nao, ili wawe na uthubutu wa kuripoti kwa
wazazi wao watakapoona viashiria vya vitendo hivyo.
Aidha kwa upande mwengine mkuu huyo aliwasisitiza wasaidizi
hao wa Sheria kuzidisha bidii ya kuisaidia jamii juu ya masuala ya kisheria,ili
kuona wanaondokana na kero zinazowakwaza.
Mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto wilaya ya
Micheweni Semeni Ali Khamis alisema sasahvi Dunia yote ipo kiganjani kutoka na mabadiliko
ya kiutandawazi, hivyo ni wakati kwa
wazazi kukaa na watoto wao na kuwafundisha jinsi ya kujitambua, kujiheshimu na kujitunza.
‘’Ulimwengu sasahivi umekua ni tofauti na zamani, hivyo ni
wambie wazazi wenzangu tuvunje ukimya wala tusione aibu tuwafundishe watoto
mbinu za kujiepusha na udhalilishaji,’’ alisema.
Nao wasaidizi hao wa Sheria walisema watahakikisha elimu
hiyo wanaifikisha katika jamii, ili kuona matendo ya udhalilishaji yanapungua.


Comments
Post a Comment