ZSSF yawataka Masheha kuwaripoti wanachama waliofariki




                               NA FATMA HAMAD – PEMBA

MASHEHA WA MKOA WA KUSINI Pemba wametakiwa kutoa taarifa    katika  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) endapo kutatokea  kifo cha mwanachama wa mfuko huo katika shehia zao, ili kupunguza udanganyifu hasa katika malipo ya fedha za Serikali.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mafao kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF Zanzibar Mussa Yussuf wakati akiwasilisha mada ya dhima ya Masheha katika utoaji wa huduma za ZSSF katika kikao kazi kilichofanyika Tibirinzi Chakechake Pemba.

Alisema kumekuwepo na baadhi ya watu wamekua wakipeleka taairifa za vifo vya jamaa zao  katika mfuko huo ambazo si za ukweli, hivyo endapo watapeleka taarifa wataepusha kutokea kwa udanganyifu  huo, sambamba na kuokoa fedha za Serikali.

‘’Wamekua wakitujia watu na taarifa za jamaa zao kufariki na kudai mafao yao, lakini tukifanya uchunguzi tunagundua kwamba sio ukweli ni uzushi,’’alisema.

Aliendelea  kusema kuwa endapo Masheha watatoa taarifa na kupeleka vielelezo  sahihi vya marehemu watasaidia warithi wake kupata mafao yao kwa haraka na kwa wakati.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hamad Omar Bakar kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid aliwataka  Masheha  hao kuwa na mashirikiano ya hali ya juu  na mfuko  wa Hifadhi ya Jamii, ili kufanikisha azma na malengo ya mfuko huo.

‘’Ndugu masheha nyinyi mnadhima kubwa katika Jamii, hivyo ni vyema mkaweka mashirikiano na ZSSF ili kuona  kila mwanachama anapata mafao yake,’’alisisitiza.


Nao baadhi ya masheha walioshiriki mkutano huo walisema watahakikisha wanalifanyia kazi agizo hilo la kuripoti matukio ya vifo yanapotokezea shehiani mwao, ili kuepusha malalamiko kati ya wananchi na ZSSF.

‘’Tunalichkua na Tutahakikisha mabuku  tuliopewa kwa ajili ya kuripoti matukio ya vifo  tunayatumia na tunaripoti Kwanu nyinyi  ZSSF,  kwani kutamfanya kila mwanachama aweze kupata stahiki zake,’’alieleza.

Aidha kwa upande mwengine masheha hao waliutaka Mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii ZSSF kuwaingiza  katika mfuko wa Pencheni ya wazee ili nawao waweze kufaidika na matunda ya Serikali yao.




Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’