TIMU ZA WANAWAKE ZA PEMBA ZAOMBA KUSHIRIKISHWA KWENYE MASHINDANO YA KITAIFA

 

                       NA FATMA HAMAD-PEMBA

Kukosekana kwa uwanzishwaji wa ligi maalumu kwa wachezaji wanawake,  imekua ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha Timu ya Mpira wa pete iliyopo Mchangamdogo  Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Hayo yamesemwa na Amina Kudra Ali Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Wete wakati wakizungumza na wandishi wa habari ikiwa ni ufuatiliaji wa tathmini ya mafanikio wa mradi wa michezo kwa maendeleo uliokua ukitekelezwa na Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA), Chama cha wanasheria wanawake (ZAFELA)   na CYD.

Anasema anahamu ya kua mchezaji mkubwa duniani, lakini anarudinyuma kwasababu tangu walipoanzisha timu hiyo hawajashirikishwapo mashindano  ya ligi za aina yoyote na kuweza kukuza vipaji vyao.

‘’Huu ni mwaka wa tano tokea kuanzisha timu yetu hii ya mpira wa pete pamoja na Netball, lakini tunakata tama hatujashirikiswapo hata siku moja bonanza lolote ambalo limeandaliwa na Serikali,’’anasema.

Anasema michezo ni moja ya fursa inayomfanya mtu kujipatia ajira, hivyo  ni vyema kwa Serikali pamoja na wadau wengine kuziunga mkono timu za wanawake zilizopo Pemba ili ziweze kufika mbali kimichezo.

Kwa upande wake mchezaji Zainab Rashid Said amesema tokea alipojiunga na timu hiyo alibahatika kupata safari mara moja ya kuenda kisiwani unguja  kwa ajili ya kushiriki mashindano ya ligi kuu.

‘’Tumekua tukishuhudia wanawake wakisafiri na kuenda nchi za nje  kwa ajili ya michezo, hivyo Tunatamani ufike wakati viongozi wawekeze kwenye timu zetu, ili na sisi vijana wa kike wa Pemba  tuweze  kutambulika duniani kupitia  michezo,’alieleza.

Katibu wa timu hiyo Bimkubwa Maulid Othman amesema baada ya kupatiwa mafunzo  juu ya umuhimu wa mwanamke kushiriki kwenye michezo, kutoka kwa Chama cha wandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA  Zanzibar  waliamua  kuanzisha timu ya mpira wa pete,  ili kuona wanawake wa pemba nawao wananufaika na fursa zitokanao na sekta ya michezo.

‘’Tumeamua kuanzisha mchezo huu kwa ajili ya kujenga afya zetu pamoja na kuonesha vipaji vyetu sisi kama wanawake,’’ameeleza.

Akitaja changamoto zinazowakabili katika timu yao ni kukosekana kwa uwezeshwaji pamoja na vitendea kazi.

Anasema wamekua wakichangishana wenyewe kwa wenyewe pamoja na viongozi wao wa majimbo na kuanzisha mabonanza ya shehia ili waweze kutoa hamasa kwa jamii juu ya umuhimu wa michezo kwa mwanamke na mtoto wa kike.

‘’Tumekua tukiwaomba viongozi wetu wa majimbo waweze kutuandalia  japo ligi  ndogondogo, ili tuweze kuonesha vipaji vyetu,’’ameeleza.

Amesema  jamii imekua akiwachukulia kama ni wahuni kwa vile wamejiingiza kwenye michezo, hivyo  ameiomba Serikali ya Mapinduzi kuangalia kwa jicho la pili ili kuona wanaungwa mkono  na kuweza  kujiajiri  kupitia  sekta hiyo.


Makamo mwenyekiti  wa  chama cha mpira wa netball Chaniza Wilaya ya Wete  alikiri kutokuwepo kwa ligi maalumu  pamoja na uwezeshwaji  kwa timu za wanawake  kisiwani Pemba.

‘’kama  hakutokua na uwezeshwaji wowote  tutakuja  kukosa timu  hata  moja  za wanawake  na kuweza kushiririki mashindano mbalimbali endapo yatatokezea,’’amesema.

Afisa mawasiliano kutoka  Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar  Khairat Ali amesema wamekua wakitoa elimu kwa jamii ili kuona wanawapa fursa wanawake waweze kushiriki michezo.

‘’Wanawake nawao wanahaki ya kushiriki michezo kama wanavyoshiriki watoto wa kiume, hivyo niwakati  jamii kuamka na kuwaruhusu ili nawao waweze kupata ajira kupitia michezo,’’ameeleza.

Amesema  kama TAMWA wataendelea kuwapa moyo wachezaji hao, waweze  kuwa wachezaji wazuri, huku akiomba na wadau wengine  wajitokeze  kuwasaidia ili waweze  kutimiza ndoto zao.


 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO