Jeshi la Polisi lawataka wahisani kuisaidia familia ya wototo wenye ulemavu

 



                              NA FATMA HAMAD – PEMBA

Jeshi la  Polisi  Mkoa wa Kusini Pemba limewataka  Wadau  pamoja na wahisani mbali mbali  kujitokeza kuisaidia  familia ya Mohamed Mussa yenye watoto  wawili wenye ulemavu wa viungo, iliyopo  Matele wilaya ya Mkoani Pemba mahitaji muhimu ikiwemo  makaazi pamoja na viti mwendo.

Wito  huo umetolewa na Mratibu  wa  Polisi  jamii wa mkoa wa Kusini Pemba Makame Nasibu Silima kwa niaba ya Kamanda wa Polisi  wa  Mkoa huo,  Abdla Hussein Mussa,  mara  baada ya kukabidhi msaaada wa vyakula na godoro,  ikiwa ni shamra shamra ya kuelekea madhimisho ya siku  16  za  kupinga  ukatili  wa kijinsia.

Alisema mazingira ya familia hiyo ni duni, hivyo ni vyema wadau pamoja na wahisani kujitokeza kuisaidia familia hiyo ili iweze kuishi katika hali ya furaha kama binadamu wengine.

‘’Kutokana na halingumu ya kimaisha inayoikumba familia hiyo, tumeamua kuwapa  msaada wa vyakula  pamoja na magodoro ili vieze kuwasaidia,’’alisema


Mapema mkuu wa  mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Kusini Pemba (TPF NET ) Habiba Ali Said amesema baada ya kuona tarifa ya familia hiyo  ambayo inakukumbwa na ugumu wa maisha kupitia kwenye mitandao ya kijamii, wameamua kuja kuifariji familia hiyo.

‘’Baada ya kuona tarifa hiyo imetugusa na tumeamua kujakuifariji familia hiyo kwa kidogo chetu mungu alichotujaalia,’’alisema.

Alisema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wamekua wakitoa misaada mbali mbali kwa familia zinazoishi katika mazingira magumu, waliopatwa na maafa pamoja waliopatwa na udhalilishaji.


Kwa upande wake baba mzazi wa watoto hao wenye ulemavu Muhammed Mussa, alisema  wanashindwa kusoma Skuli kutokana na kukosa Vigari vya maringimawili kwa ajili ya kutembelea.

‘’Hawasomi Skuli wala Mdrasa, kwani  ni mbali hawana vigari, na mimi sina uwezo wa kununua,’’alisema baba mzazi.

Wakitoa shukrani zao mara baada ya kupokea msaadahuo wanafamilia hao,  wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwapatia msaada, huku wakiwataka na wengine wenye nia ya kutoa kuekeza sadaka yao kwa  familia hiyo, ili waweze kupata mahitaji muhimu ambayo yatawasaidia   watoto hao.




 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO