ZAFELA YAWATAKA WAZAZI KUWARUHUSU WATOTO WAO WA KIKE KUSHIRIKI MICHEZO
NA MARYAM SALUM,PEMBA
JUMUIA ya Wanasheria Wanawake Zanzibar ZAFELA imesema imejipanga kuendeleza mapambano dhidi ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwenye makundi ya michezo.
Hayo yalisemwa na Rufea Juma kutoka Chama cha Wanasheri wanawake ‘’ZAFELA’’ Zanzibar wakati akizungumza na asasi za kiraia pamoja na tasisi za Serikali katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya umuhimu wa michezo kwa mwanamke na mtoto wa kike yaliofanyika Gombani Chake chake Pemba.
Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuona kunakuwepo na usawa wa kijinsia kwa jamii katika suala zima la michezo.
Alisema kuwa ingawa kumekuwa na dhana nyingi potofu kutoka kwa baadhi ya watu kudhani michezo kwa mtoto wa kike na mwanamke ni uhuni.
‘’Jamii imekua na dhana mtoto wa kike akishiriki michezo atakua muhuni, hali inayopelekea kukosa fursa za kimaendeleo zilizomo katika jamii,alisema’’.
Alieleza kuwa suala la udhalilishaji halipo kwenye michezo pekee bali hata majumbani lipo na linafanywa siku hadi siku bila mtu mwenyewe kujua.
Alisema kwa vile changamoto hiyo haipo tu kwenye jamii ipo hadi kwenye maeneo mengine kama vilekatika michezo, ni vyema jamii kushirikiana na wadau wengine kupambana na tatizo hilo kwenye makundi mengine kama vile michezo.
Kwa upande wake Riziki Hamadi Ali,msaidizi wa sheria Chake Chake alisema kuwa ili waweze kupambana na tatizo hilo kuna haja sasa kufika hadi kwenye maeneo ya michezo kwani kumekuwa na baadhi ya watu wanafanya udhalilishaji iwe kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya.
Hivyo kama wasaidizi wa sheria tuungane kwa pamoja kuona tunafika kwenye makundi ya michezo kuelimisha, lengo ni kuondosha udhalilishaji, ili kuweka usawa wa kijinsia kwenye michezo.
Walifahamisha kuwa ili usawa wa kijinsia uweze ni vyema kuwepo na mazingira salamakwenye michezo .


.jpg)


Comments
Post a Comment