UBAKAJI BADO WAENDELEA KUWATESA WATOTO
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Familia moja Micheweni Pemba yakumbwa na huzuni kufuatia mtoto wao wa miaka mitano (5) kufanyiwa kitendo cha kuingiliwa kinyume na maumbile.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama mzazi wa mtoto huyo huko nyumbani kwake alisema mtoto wake huyo alifanyiwa kitendo hicho wakati alipokua shambani akiinga mtama.
Alisema baada ya kurudi nyumbani kwao mtoto alikua anatetemeka na kumuambia mama yake kuwa kuna mtu alimchukuwa na kumfanyia kitendo kiovu.
‘’Nilipo muhoji alinimbia kuna mtu kanichukua kaningiza kwenye boma na kunivua nguo na kunifanyia udhalilishaji,alisema’’mama mtoto.
Alisema baada ya hapo walikwenda Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi hatimae alionekana tayari ameshaathirika.
Kwa upande wake baba mzazi wa mtoto huyo alisema kitendo hicho cha kinyama alichofanyiwa mtoto wake kimemsikitisha kutokana na mtoto wake ni mdogo, hivyo ameliomba jeshi la Polisi kumsaidia ili kuona haki imetendeka.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Wiliam Mwampagale alisema tukio hilo limetokea mwanzoni mwa mwezi huu, ambapo mtuhumiwa wa tukio hilo hawajafanikiwa kumkamata.
‘’Tuliungana na kamati ya usalama ya Wilaya pamoja na kamati ya Sheha ila hatukufanikiwa kumpata mtuhumiwa, inaonesha alishasafari na kwenda kisiwa chengine,alisema’’.
Aidha kamanda huyo aliwataka wananchi kuwacha muhali na badala yake washirikiane na vyombo vya sheria ili kuwadhibiti wahalifu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutiwa hatiani.

Comments
Post a Comment