Dawa za kulevya zamsababishia kwenda Jelamiaka 7
NA FATMA HAMAD,PEMBA
Ridhwan Mkongwe Sharif mwenyeumri wa miaka 38 mkaazi wa Kipange Konde Pemba,ameanza maisha mapya katika chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka saba, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na misokoto 50 ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 210.5.
Mapema Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Wete Zuwena Mohamed Abdulkadir alisema, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kuona kwamba hauna chembe ya shaka, mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo.
‘’Kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wetu tumejirisha na kuona ushahidi uliotolewa ni wa ukweli hivyo mahkama imekukuta na hatia mshitakiwa,’’ alisema.
Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP Mohamed Ali Juma aliiambia Mahkama hiyo kuwa, kwa vile mshtakiwa ameonekana na hatia ni vyema kupewa adhabu kali ili iwesomo kwake na wengine.
Alisema dawa za kulevya ni changamoto inayodumaza maendeleo ya vijana nahataTaifa.
‘’Kwa kweli sasahivi masuala ya dawa za kulevya imekua ni mtihani mkubwa kwa vijana wetu mitaani, hivyo tunaomba apewe adhabu inayomstahiki kupewa mshtakiwa huyo ili na wengine wenye tabia kama yake waogope,’’ alisema.
Kabla ya kutolewa hukumu mshtakiwa Ridhwan aliiomba Mahkama impatie adhabu ndogo kwa vile ni marayake ya kwanza kufanya kosahilo.
Hakimu Zuwena alifafanua kuwa,kwa mujibuwa kifungu cha 23 cha sherianambari 8 yamwaka 2021 sheria ya Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawaza kulevya sheria ya Zanzibar, adhabu yake ni Faini ya shilingi Milioni 50 au kifungo cha miaka 30.
Ingawa Hakimu huyo alijiegemeza katika kifungu cha 299 cha sherianamba 7 yamwaka 2018 sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na kumuamuru mshtakiwa huyo atumikie chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka 7 au kulipafaini ya shilingimilio 50.
Sambamba na adhabu hiyo pia alitoa amri ya kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali Vespa ya mshtakiwa huyo ambayo ilitumika kama ni kilelezo cha ushahidi pamoja na kuharibiwa kwa bangi iliyokamatwa.
Mshtakiwa huyoalitenda kosahilo Disemba 31 mwaka jana majira ya saa 12:00 jioni kijiji cha Kipange Konde wilaya ya Micheweni Pemba, bila ya halali alipatikana naMisokoto 50 ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 2010.5 kwa ajili ya matumizi binafsi, jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 23 (1) (a) (2) (3) sheria na mbari 8 yamwaka 2021 sheria ya Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment