WANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO

 
 

 

                                        NA FATMA HAMAD,PEMBA

Wandishi wa habari wametakiwa kuandika habari ambazo zitaihamasisha Jamii kulipa kipaumbele suala la michezo kwa wanawake ili kuona nawao wanashiriki katika mashindano mbali mbali Nchini.

Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa mafunzo ya masuala mbali mbali ya Jinsia na michezo Hawra Shamte wakati akizungumza na wandishi wa habari huko Ukumbi wa  Tamwa Chake chak Pemba.

Alisema bado Jamii hawampi kipaombele mwanamke kushiriki katika masuala ya michezo kutokana na dhana iliyojengeka kwamba mwanamke anaeingia kwenye michezo ni muhuni.

‘’Tumegundua kwamba Michezo yote ya wanawake imekufa kutokana na mfumo dume ambao umetawala katika Jamii ya Wazanzibar kwani wanasema michezo kwa mtoto wa kike ni uhun’’alisema Mkufunzi.

Alisema Sekta ya Michezo inafursa mbali mbali ambazo zinapatikana, hivyo ni wakati muafaka kwa waandishi wa habari kuandika habari ambazo zitaielimisha jamii kulipa kipaumbele suala la michezo kwa mtoto wa kike ili na yeye aweze kunufaika na fursa mbali mbali mbali ambazo zinapatikana katika sekta ya michezo.

Alifahamisha kuwa michezo haisababishi uhuni bali humjenga mwanawake kua na Afya njema, pia huleta  Amani na Upendo, na hupatkana kwa ajira.

 Kwa upande wake Afisa programu kutoka Chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA) Khairat Haji alisema lengo la mafunzo hayo kwa wandishi wa hao ni kuhakikisha wanaibua kero zinazowakumba  wanawake kushindwa kushiriki michezo mbali mbali ili ziweze kujulikana na kupatiwa ufumbuzi.Aidha alisema matarajio yao ni kuona kwamba wanawake wengi wamehamasika na kujikita katika Sekta ya michezo na kushiriki kwenye mashindano  mbali mbali  ili waweze kujipatia kipato pamoja na fursa ambazo zinapatikana.
 
 
 Nao Wandishi wa habari waliopata mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yamewaonesha njia, huku wakiahidi kuyafanyia kazi ili lengo liweze kufikiwa.


 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO