KUKOSEKANA KWA MTANDAO KWA SABABISHA HASARA KWA WAFANYA BIASHARA


 


NA NIHIFADHI ABDULLAH UNGUJA

 Kukosekana kwa mtandao kumesababisha hasara ya kutoingiza kipato kwa watu ambao shughuli zao zinategemea huduma hiyo kwa kiasi kikubwa

 Wakizungumza na kati fm kwa nyakati tofauti wafanyakazi wanaotoa huduma ya intanet na waandishi wa habari wa mitandao wamesema hali hiyo imewarejesha nyuma kwani walishindwa kufanya kazi.

 Waandishi wa habari Hassan Mselem  na Amina Masoud wamesema kutokana na dunia ilipo kuzimwa au kukosekana huduma ya inteneti  inapelekea hasara sio tu kwao bali hata kwa wananchi kutopata habari kwa wakati muafaka

 Nae Juma Marijani amesema ameamua kujiajiri kwa kuekeza kutoa huduma za intanet hivyo inapokesakana kunarejesha nyuma nguvu za kujikwamua kiuchumi

 Sambamba na hayo ametoa wito kwa serikali kutatua vikwazo katika masuala ya mtandao ili kwenda sambamba na ulimwengu ulipo

 

Comments

Popular posts from this blog

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI