RUSHWA BADO NI JINAMIZI LINALOWAKUMBA WANAWAKE
NA FATMA HAMAD, PEMBA
KUWEPO KWA rushwa
ya pesa imetajwa kwamba ni moja ya sababu inayowakosesha wanawake wanaogombea
nafasi za uongozi kushindwa kuyakamata majimbo.
Hayo
yamesema na baadhi ya viongozi wa vyama
vya siasa na wanaharakati wa wanawake na watoto wakati wakiwa katika
kikao cha tathmini juu ya Mradi wa SWIL, kilichofanyika Ofisi Tamwa Chakechake Pemba.
Walisema
licha ya mikakati mbalimbali inayochukuliwa na serikali na wadau wengine kuona
wanawake wanashika nafasi za uongozi, bado kunachangamoto ya rushwa ambayo inapelekea
wanawake kushindwa na kupelekea wenye pesa zao kuyahodhi majimbo.
Walisema
katika uchaguzi uliopita wa 2025 wanawake walionekana kujitokeza kwa wingi
kugombea,lakini kwenye majimbo walirudi ni kidogo.
‘’Jamani
tuseme ukweli uchaguzi sasahivi umekua kama ni biashara, kama huna pesa basi
huwezi kufanikiwa , wanarudi majimboni walewale viongozi wa zamani ama wenye
pesa zao,’’wanasema.
Mapema
Salma Omar kutoka chama cha Wanasheria
wanawake Zanziba (Zafela) anasema ili kupunguza malalamiko hayo ipo haja
kuwekwa sheria itakayomlinda mtoa
taarifa, sambamba na kuwekwa kwa dawati maalumu la upokeaji wa taarifa za
vitendo vya rushwa wakati inapofika
kipindi cha chaguzi.
‘’Ifike
wakati na sisi Zanzibar tuwe na sheria itakayo mlinda mtoa taarifa ya vitendo
vya rushwa, kwani itasaidia kupunguza rushwa na wanawake wanyonge wapate
nafasi,’alisema.
Kwa
upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali Hadid Rashid Hadid
alisema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ambazo wamekua wakizifanya zimeonesha
kwamba familia ambazo zinaongozwa na wanawake, ama wanawake wanashirikishwa juu
ya mambo yao, zinakua ziko juu kimaendeleo.
‘’Niseme
wanawake wakiondoshewa vikwazo na wakapata nafasi wanafanya viruzi, mfano
tafiti tunazo zifanya tunagundua kwamba familia ambazo wanawake wanakua na
maamuzi zinamaendeleo,’’alifahamisha.
Sabah
Ali Mzee Mkurugenzi mtendaji wa Jumuia ya wanawake wenye ulemavu upande wa
Unguja (JUWAUZ) alisema lengo la mradi wa Swil ni kuja kuwakomboa wanawake wote
waondokane na vizigiti mbalimbali ambavyo vitawazuia kuingia katika maamuzi.
‘’Tunawasaidia
vikundi vya wanawake hasa wenye ulemavu kuona wanafanya shughuli
zinazowaingizia kipato kitakachowasaidia kuingia kwenye kinya’nganyiro cha
uchaguzi,’’alisema.
Mkurugenzi
wa Chama cha Wandishi wa Habari wanawake TAMWA Zanzibar Nairat Ali alisema katika
Uchaguzi uliopita ilionekana idadi ya wanawake na hasa wenye ulemavu
walijitokeza kwa wingi ukilinganisha na miaka ya nyuma.
‘’Tumeona
Uchaguzi uliopita wanawake walijitokeza wengi, na ni mara ya kwanza kujitokeza
mgombea Uraisi mwanamke, hivyo japo kuna changamo, bado tuendeleeni kutetea,
ili kuona lile tunalolitaka la hamsini kwa hamsini katika uongozi limefikiwa,’’alishauri.
Nae
Afisa Programu kutoka Tamwa Zanzibar Sabrina Yussuf Mwintanga alisema lengo la
mradi wa SWIL ni kuwawezesha wanawake hata walioko vijijini kuhakikisha
wanashirika katika harakati za uchaguzi, na kuingia kwenye maamuzi.
Alisema
SWIL imeanza kuzaa kuleta mabadiliko kwani, katika serikali ya awamu ya nane,
imeonekana idadi ya madiwani wanawake imeongezeka kwani ni 27 ukilinganisha na
kipindi kilichopita, ilikua ni 25 kwa Zanzibar.
MWISHO.
Comments
Post a Comment