Suhaila Omar: ni mwanamke anaepambana kuiheshimisha wadi ya Mtambwe baharini
Jee ni vipi Suhaila anapambana kuingia kwenye maamuzi
NA
FATMA HAMAD, PEMBA
Nilipabana
na wanaume saba nashukuru nimewaangusha, licha ya kuwa walinibeza kwa sababu ya
uwanawake wangu.
Hiyo
ni kauli ya Bi Suhaila Omar Hamad
mgombea wa Udiwani wadi ya Mtambwe Baharini kwa chama cha ACT Wazalendo, mwenye
tunu ya kutaka kuingia kwenye maamuzi.
Bi
suhaila ni mama wa watoto 5 ana umri wa (34), ni mzali wa mtambwe, anaishi
kijiji cha Uondo, ambacho kinawakaazi wapatao 4220 ameanza harakati za kisiasa
tangu mwaka 2017.
Suhaila anaonekana kuwa miongoni mwa wanawake waliojitokeza kuingia kwa kishindo kwenye siasa za ngazi ya chini mwaka huu,
kipindi ambacho wananchi wengi na wadau wa jinsia wametoa msukumo kwa
uwezeshaji wa wanawake.
Kutokana na hilo ndipo akanza kujitoa, ambapo uchguzi wa mwaka
huu 2025, ni mara yake ya kwanza kuingia kwenye kinyan’ganyiro cha kuwania uongozi
katika wadi ya mtambwe baharini.
Hata Takwimu na ripoti zinaonyesha ongezeko la ushiriki wa
wanawake kwenye uchaguzi wa 2025 nchini Tanzania, ikijumuisha Zanzibar.
Suhaila ameanza kujihusisha na harakati za siasa tokea mdogo, ameanza
kushika nafasi ndogo ndogo za kwenye tawi, jimbo, mkoa na hadi amefikia hatua
mara hii kujiingiza katika kinyan’ganyiro cha kugombea nafasi hiyo ya Udiani
wadi ya Mtambwe Bsharini.
Anasema baada ya wenzake na viongozi wake kumuona anauwezo mzuri
wa kuongoza ndipo walipomshawishi aingie kwenye nafasi kubwa, aweze kusimama na
kutetea shida za wanamtambwe akiwa kwenye maamuzi.
Hivyo mwaka huu 2025 ndipo aliposimama rasmi na kuchukua fomu ya
kugombea Udiwani wa Wadi ya Mtambwe baharini kupitia tiketi ya chama cha ACT
Wazalendo,ili
kuboresha huduma za msingi ikiwemo maji, afya, elimu na kutetea
maslahi ya kina mama na vijana wa Mtambwe Baharini.
Suhaila anatokea ACT
Wazalendo, chama kinachojivunia msimamo wa demokrasia, uwajibikaji na
uwazi.
Anasema ACT ni chama kilichopewa usajili wa kudumu na
kinaonekana kuwa mchezaji mkubwa wa upinzani na siasa za mrengo wa vyama
pinzani, na kinachojali wanawake.
Mipango ya chama kuhusu uwakilishi
wa wanawake katika maamuzi imekuwa
ikisaidiwa na ngome za wanawake na mashirika ya kiraia.
Vikwazo anavyokutana
navyo
Suhaila anasema moja ya
changamoto anayokumbana nayo ni maneno ya baadhi ya watu wasiomtakia ambao
wamekua wakimuwambia hawaezi kushinda kwa vile amegombea na wanaume na tena
wenye uwezo wao kifedha.
Anasema amepata pesa
kidogo na amefanikiwa kufanya mikutano kidogo ya kampeni, ingawa maranyingi
anafanya za nyumba kwa nyumba.
Anasema changamoto nyengine inayomkabili ni
kukosa pesa za kuchapishia mabango
pamoja na vipeperushi kwa ajili ya kuvisambaza na kuweza kufahamika na wananchi.
‘’Suala la kukosa rasilimali pesa bado ni tatizo kwangu,nashindwa
kufanya mikutano ya hadhara, na kuchapisha vipeperushi ambavyo vingeniwezesha
kujitangaza kwa wananchi,’’anasema.
Anasema hata mabadiliko ya sheria za uchaguzi ya mwaka 2024
yanayoweka masharti mapya, usajili wa vyama na taratibu za kusajili wagombea
pia umekuwa changamoto kwa baadhi ya vyama na wanawake wagombea.
VIPAUMBELE VYAKE
Mwanamama huyo anasema vipaumbele vyake ni kuwakaribu na wanawake
wenzake na kuwasaidia kero zao ambazo zimekuwa zinawatokezea katika vjiji vyao.
Anasema kipaumbele chengine ni kuvisaidia vikundi vya
wajasiriamali wanawake kwa kuvipa mikopo vianzishe biashara ambazo zitawazesha
kuinua kipato chao,
Kipaumbele chake chengine pia anasema ni kusimamia nifuko ya Wabunge na Wawakilishi inayotolewa kwa ajili ya wananchi, na kuona inawanufaisha kweli wahusika wenyewe.
FAMILIA YAKE
Anasema familia yake
ikiwa ni pamoja na ndugu zake watoto, na
majirani zake wamekuwa wakimuunga mkono tokea mwanzo wa kutia nia ya kwenda
kuchukua fomu yakuingia kwenye kinyan’ganyiro hicho.
‘’Nashukuru familia yangu
inaniunga mkono, iko bega kwa bega na mimi, na wamekua wakiwahamasisha wapiga
kura waweze kunichagua,’’anaeleza.
Anasema kwa upande wa
mume wake ambae anafhamika kwa jina la Omar Hamad, amekua msaada mkubwa kwake,
kampeni zake za nyumba kwa nyumba amekua akimpeleka na kumsadia kuwaomba
wananchi wamuunge mkono mwanamke mwenzao huyo.
KIONGOZI WA CHAMA CHAKE
Juma Khamis Ali mwenyekiti
wa ACT Wazalendo Mkoa wa Wete kichama anasema chama chao kinasera maalumu ya
kuwasaidia wanawake washiriki harakati za uchaguzi na kuingia kwenye maamuzi.
Anasema Suhaila amekuepo
chamani kwa muda mrefu, amekua akijitolea kukisaidia chama kuhakikisha kinapiga
hatu, hivyo hata akipata nafasi katika wadi yake mabadiliko yatapatikana.
‘’Suhaila ni mmoja wa
wanawake mwenye kujituma na mpambanaji, naamini akichaguliwa na kiongoza wadi
ya mtambwe naamini anaweza kuleta mapinduzi makubwa ndani ya wadi na hata katika
chama,’’anaeleza.
Takwimu
Kwa
mujibu wa Chama cha Wandishi wa Habari WAnawake Tanzania Tamwa Zanzibar kupitia
ripoti iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanziba mwaka 2020, kupitia nafasi ya
Uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar wanawake waliojitokeza ni 61
walioshinda ni 8 na wabunge wanawake waliowakilisha Zanziba ni wane.
Takwimu
kutoka Tume huru ya Uchaguzi Tanzania kwa upande wa wabunge walikua 141
walioshinda wanawake ni wane tu.
Kwa
Uchaguzi wa mwaka huu 2025, unaweka historia mpya, kwani ni mara ya kwanza
wanawake kujitokeza kwa wingi
kuwania
nafasi mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.
Kwa
vile suasa la uchaguzi ni haki ya kila mtu kama katiba Katiba yetu mama ya nchi
ya mwaka 1984 inavyoeleza katika kifungu cha 21,(2) kinaeleza mzanzibari yoyote
anahaki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia maamuzijuu ya mambo
yanayo muhusu yeye, maisha yake au yanayohusu Taifa lake.
Hata
Mikataba ya kimataifa ya haki za kiraia na haki za kisiasa ya mwaka 1966
kifungu cha 25, kila raia ana haki ya kupiga kura na kuchaguliwa katika
uchaguzi wa kweli, wa haki na wa mara kwa mara, uliofanywa kwa kura ya siri na
kuhakikisha uhuru wa wapiga kura.
Ripoti za vyombo vya habari na mashirika ya jinsia
zinaripoti ongezeko la wanawake wanaogombea
mwaka 2025 ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.
Zanzibar pia imeona
wanawake wakichukua nafasi kubwa katika kuingia kwenye nafasi za juu za
uongozi,ikiwa ni sehemu ya mwelekeo wa kitaifa wa kuhamasisha ushiriki wa
wanawake katika siasa.
Hata kwa upande wa Bunge, ziko taratibu za viti maalum za
wanawake na hii imekuwa moja ya njia za kuimarisha uwakilishi wa kijinsia,
ingawa juhudi za kuongezeka kwa wagombea wa kiti cha uwakilishi wa moja kwa
moja zinaendelea.
Comments
Post a Comment