AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 7

 


                            NA FATMA HAMAD, PEMBA

 MAHAKAMA ya Mkoa chake chake imemuhukumu kutumikia chuo cha mafunzo  kwa muda wa miaka 30,pamoja na kulipa fidia shilingi Milioni tatu Hakim  Said Hakim mwenye umri wa miaka 36 Mshirazi  wa Jondeni wilaya ya Mkoani , baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka  mtoto mwenye umri wa miaka 7.

 Hukumu ya kijana huyo  kutumikia chuo cha mafunzo kwa kosa hilo la kubaka ambalo ni kinyume na  vifungu vya 108,(1)(2) n 109 (2) Vya sharia namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar ,imetolewa October 21 2025  chini ya Hakimu dhamana  Taki Abdalla Habibu  mbele ya mwendesha Mashataka  wa serikali Kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma Ali Juma .

 Juma Ali Juma  mwendesha wa mashtaka wa serikali   kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka  alisema kuwa hukumu hiyo iwe fundisho kwa wengine  walioko katika jamii ambao wanaendelea na  vitendo vya udhalilishaji  kwa watoto ,na kuonesha utendaji wa haki  na msaada wa serikali katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji .

 Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo siku ya tarehe 14 july 2024 majira ya saa 4.00 usiku huko mkoani  mkoa wa kusini pemba  kwa kutumia nguvu na bila ya ridhaa yake, alimbaka mtoto  wa kike mwenye umri wa miaka 7 Jambo ambalo ni kosa kisheria.

 Ikumbukwe kuwa kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifunguliwa Mahakamani hapo tarehe 3\12\2024 na jumla ya mashahidi 7 walitoa ushahidi ulioiwezesha Mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.

 Hakimu huyo alimuamuru kijana huyo kutumikia Chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30 sambamba na kulipa  fidia ya shilingi 3 ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hizo. 

 


 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO