ADC YAAHIDI KUWAFUTIA MADENI WALIOKOPA ELIMU YA JUU
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tikati ya Chama cha Alliance
for Democratic Change ADC
Hamad Rashid Moh’d amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi na kuingia
madarakani atawalipia deni la mkopo wa Bodi ya Mikopo Zanzibar wale wote
waliokopeshwa kwa ajili ya kusomea, wafaidike na mishahara yao.
Mgombea huyo aliyasema hayo kwakati
akiwahutubia wananchi ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni
ulifanyika Mjimbini Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema
waajiriwa wengi wamekua wakiishi maisha duni, kutokana na mishahara yao kukatwa
na kulipa deni la mkopo hiyo.
Alisema
sera ya chama chake ni kuepo kwa elimu bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu,
hivyo akiingia madarakani atawalipia madeni kwa wote ambao wanadaiwa na Bodi ya
mikopo, waondokane na halingumu za maisha.
‘’Mishahara
yenyewe midogo haiwakidhii haja zao halafu unakatwa, naahidi nikichaguliwa nawalipia wote
wanaodaiwa, wafurahie maisha
yao,’’alisema.
Aidha
kwa upande mwengine alisema atawapeleka kufanya kazi nje ya nchi wafanyakazi wa
kada ya uuguzi, manesi na madaktari kwenda kupata ujuzi zaidi, ili kuja kuokoa
maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Mapema
Katibu mkuu wa chama cha ADC Mwalim Hamad Aziz alisema endapo wataingia
madarakani watajenga Chuo cha Uvuvi kisiwani Pemba, ili kuzalisha wataalamu
kupitia sekta hiyo.
‘’Tutakapoingia
madarakani tutaanzisha chuo cha uvuvi, vijana wa Pemba wasome na kupatikana kwa
wataalamu wa uvuvi na kupatikana ajira kwa wingi,’’alisema.
Kwa
upande wake Mratibu wa kampeni wa chama hicho Hafid Khamis Amour aliwataka
wananchi wa Mjimbini hususani wanawake, kukichagua chama cha ADC, ili kiwaletee
maendeleo.
‘’Wanawake
ni kundi ambalo limekua likikumbana na vikwazo kadhaa vya udhalilishaji, hivyo
nawaomba mkichague chama chetu, kije kuwa mkombozi wa shida zenu,’’alisema.
Aidha
amewataka wananchi hao kuwachagua
viongozi ambao wanauchungu na chi yao ambao watawaletea mabadiliko
majimbonimwao, na sio kuchagua kwa ajili ya chama Fulani.
Nao
baadhi ya wananchi wa Mjimbini walisema watahakikisha wanakiunga mkono chama
hicho, kwani kimeonesha matumaini makubwa kwa wananchi wake.
Comments
Post a Comment