BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT ) LATOA SOMO KWA WANDISHI WA HABARI PEMBA KUELEKEA UCHAGUZI
NA FATMA HAMAD, PEMBA BARAZA la Habari Tanzania (MCT) Ofisi ya Zanzibar , limewataka Waandishi wa Habari kuzingatia miiko, kanuni na maadili yao wakati wanapoandika habari zao hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu, ili kuepusha nchi kuingia kwenye migogoro. Ametoa nasaha hizo kwa Viongozi wa klabu ya Wandishi wa Habari kisiwani Pemba (PPC), pamoja na baadhi ya wanachama wao Mratibu mstaafu wa Baraza la habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar,Bishifaa Said Hassan katika kikao maalumu cha kuwatembelea wanachama wake. Alisema kuwa Baraza la habari linajukumu kubwa la kuzungumza na Waandishi wa habari sambamba na kuwakumbusha wajibu wao kwani sauti na kalamu zao zikitumika vibaya vinaweza kupelekea machafuko yasio ya kutegemewa hasa katika kipindi hichi cha kuelekea Uchaguzi mkuu. Alieleza kuwa Baraza la habari Tanzania (MCT) Ofisi ya Zanzibar imeamuwa kuwatembelea wanachama wake ikiwem...