WAGOMBEA WANAWAKE WACHONGWA UKALI

 

NA  FATMA  HAMAD,  PEMBA

 WANAWAKE ambao ni  wagombea kutoka vyama tofauti vya siasa wametakiwa  kuzisoma na kuzifahamu Sera na Seria za vyama vyao, ili waweze kuzungumza mambo yenye maana wakati watakaposimama katika majimbo na kunadi sera zao.

 Alisema ili waweze kusimama na kuzungungumza sera nzuri, ni vyema kurudi katika vyama vyao na kuzisoma sera zao ili waweze kuzitambua.

 Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake  wagombea kwa nafasi mbali mbali  Mkurugenzi wa mradi wa  kuwawezesha wanawake katika masuala ya  uongozi na Demokrasi kutoka Jumuia ya utetezi wa kimazingira na haki za wanawake (Pegao)  Hafidh Abdi Said  katika ukumbi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake  Tanzania Tamwa Zanzibar Mkanjuni  Chake chake mkoa wa Kusini  Pemba.

 Alisema  ni vyema kila mwanamke ahakikishe anafuata sera ya chama chake,  wakati anapokwenda kusimama na kunadi sera zake katika jamii yake.

 Alifafanua kuwa kila mmoja arudi kwenye chama chake ili kusoma sera na kuweza kuzitambua, kwani kutamfanya kuzungumzia mambo yenye maana ambayo yanaweza kuleta mabadiliko katika majimbo yao.

"Niwatakewanawake nyote mnaotarajiwa kuwa viongozi kwenda kuzungumza kero ambaozinawakwaza wanajamii, na sio kuzungumzia  yasikua na faida yoyote kwa wananchi,’’anafahamisha.

 Anasema endapo watasimama vyema na kuwa na sera nzuri zenye maslahi na umma, kutawafanya waweze kuchaguliwa na kusimama kwa wingi majimboni.

 Kwa upande wake Mratibu wa Program kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa  Zanzibar Sabrina Yussuf Mwintanga  alisema ni wajibu kwagombea  hao, kuhakikisha wanakwenda  kutekeleza vyema na kwa kujiamini  majukumu yao, na sio kuzungumza sera ambazo zitapelekea kuchafuana.

  "Nyinyi ni wanawake shida zilizomo za kwenyevijiji vyenu mnazijua, simameni na muwe karibu zaidi na wananchi wapate hamu ya kuja kuwachagua siku  ya kutia kura,’’aliwasisitiza.

 Mapema Mratibu  wa mradi  huo wa kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi na Demokrasia kutoka  Jumuia ya utetezi wa kimazingira na haki za wanawake Pemba  (Pegao)  Dina Juma   Makota alisema ni wakati kwa wagombea hao, kuweka tageti na malengo waliyoyakusudia katika  uongozi wao pindi wakichaguliwa.

 " Wanawake wenzangu niwatake kwenda kusimamia vyema majukumu yenu hakika nyinyi ni viongozi watarajiwa", alifafanua.

 Mkufunzi wa  mafunzo hayo Sabahi  Mussa Said alisema ni wajibu kwa watia nia hao, kufuata sheria, Sera  na maadili ya uchaguzi kwa wakati wote wanapokua wakinadi sera zao, ili kudumisha Amani na utulivu kabla na baada ya uchaguzi.

 Alisema suala la uchaguzi ni kipindi cha mpito, hivyo ni vyema kuwa wastaarabu, ili kulinda hadhi na heshima ya utu wao na Taifa lao.

 Kaimu Mratibu wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake  Tanzania Tamwa Zanzibar Ofisi ya Pemba Amina Ahmed Mohamed alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajenga vyema wagombea wanawake wawe  na uthubu kusimama na kuzungumza sera ambazo zitasaidia kupatikana kwa maendele, kwenye jamii zao.

 Baadhi ya wagombea  hao ambao  walisema mafunzo hayo yamewajenga vyema, na kuhakikisha wanafuata yote ambayo wameelekezwa.

 Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wagombea  hao yameandaliwa  na Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania  Tamwa Zanzibar  kwa ushirikiano wa  Pegao,  Zafela na Juwauza.

 


 


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO