NA
FATMA HAMAD, PEMBA
AKINAMAMA
wajawazito wamehimizwa kula vyakula vyenyelishe bora, ambavyo vinapelekea
kuongezeka kwa uzito miilini mwao, ili kulinda afya ya mama, kumfanya mtoto
azaliwe akiwa salama.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Chakechake Kaimu
Mratibu wa Kitengo cha Lishe kisiwani Pemba Said Abdi Said alisema lishe hupelekea kuongezeka kwa uzito kwa mama
mjamzito, na pia kunasababisha ukuaji kwa mtoto alie tumboni.
Alisema mjamzito
anatakiwa kuongezeka uzito wastani wa
kilo nane hadi 12, kwa kipindi chote cha ujauzito wake, hivyo ni vyema kutumia
lishe bora, ili kulinda afya na usalama kwa mama na mtoto.
‘’Kuongezeka kwa uzito kwa mjamzito ni muhimu, hivyo
jitahidini kutumia lishebora ili kuboresha afya ya mama na mtoto aliemo
tumboni,’’alisema.
Alisema mjamzito anatakiwa
kula mlo kamili wenyemchanganyiko wa vyakula kutoka katika mchanganyiko wa
makundi sita kama vile Mboga, Matunda, Samaki kila siku ili kuongeza uzito
katika kipindi hicho cha ujauzito.
Akitaja athari ya kutokuongezeka uzito kwa mama mjamzito
alisema ni kujifungua kwa mtoto mwenye uzito mdogo, ambapo huwa wako hatarini
kupata utapia mlo.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Sayansi
ya Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Tanzania Davis Gisuka anasema mtoto
anapokua tumboni anategemea zaidi chakula kutoka kwa mamayake, hivyo ni vyema
mama mjamzito kula vyakula vyenye lishe bora,
ili kujenga afya ya mama na mtoto.
‘’Tufahamu kwamba mtoto akiwa tumbona anategemea chakula kutoka
kwa mama yake tu, hivyo ni vizuri wajawazito kupendelea kula mlo
uliokamilika,’’alisema.
Mapema mwananchi Saida Ali Hamad mkaazi wa Chakechake anasema
upo umuhimu mkubwa kwa mjamzito kutumia lishe bora, kwani humsaidia kufikia
kiwango cha damu anachotakiwa kuwanacho
mjamzito,ambacho kitamuwezesha kujifungua salama.
‘’ Mama mjamzito anatakiwa awe na kiwango cha damu kisichopungua
uzito 12, hivyo endapo kama hatokula vyakula vya lishebora kutapelekea kutoakea
kwa athari hususani wakati anapojifungua,’’alieleza.
Hadia Kombo Ali ambae anaujauzito wa miezi sita mkaazi wa
Micheweni alisema kula vyakula vya lishe bora kwa mjamzito ni muhimu, kwani
hujenga afya ya mama na mtoto.
Alisema yeye mumewake amekua akimtafutia lishe bora, na kwa mara
ya mwisho alipokwenda Cliniki aliambiwa afya pamoja na uzito wake uko vizuri na
kwenye kiwango kinachotakiwa.
Mwananchi Sheha Ali Said aliwakumbusha wanaume wenzake
kuhakikisha wanawashughulikia wenza wao ipasavyo na kuwapa huduma muhimu
ikiwemo lishe bora, ili kuonesha upendo kwa mama na mtoto alie tumboni.
Nae Afisa Mdhamini wizara ya Afya Khamis Bilali Ali alisema ili
mtoto azaliwe akiwa salama ni vizuri kujengewa mazingira bora na salama tokea
akiwa tumboni kwa mama yake.
Alisema ni vyema wazazi wa kiume kuhakikisha wanakua karibu na
wenza wao na kuwapatia lishe bora hususani wakati wanapokua na ujauzito, ili
kumlinda mtoto na maradhi ya utapiamlo wakati atakapo zaliwa.
‘’Niwaombe wanaume wenzangu wakati wake zetu watakapokua na
ujauzito tupunguze pirika tuwe karibu nao, tuoneshe upendo kutamsaidia
ajifungue akiwa na hali nzuri,’’alishauri.
Alisema kwa mujibu wa kitaalamu ya Sayansi ya Makuzi, Malezi na
Maendeleo ya awali ya mtoto, mtoto anapokua tumboni anasikia kila kitu
kinachofanyika ulimwenguni, hivyo endapo kama wazazi watakua wanaishi kwa upendo na furaha, kunamjenga mtoto na
kujihisi yuko kwenye familia bora.
Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF ya mwaka 2021, ambayo ilifanyika
katika Mkoa wa Pwani, ilibaini kuwa ni asilimia 28 tu ya wanawake wajawazito
waliokula vyakula kutoka katika makundi
matano ya au zaidi.
Pia ulibaini kuwa kuna asilimia 18 tu wanawake wajawazito
waliokua na uwelewa wa kutosha kuhusu lishe bora, ambapo hali hiyo inachangia
ulaji usiofaa na hatimae husababisha matatizo kwa mama mjamzito.
Comments
Post a Comment