WAJASIRIAMALI WAOMBA KUPATIWA ELIMU YA UTENGENEZAJI BIDHAA
NA FATMA HAMAD, PEMBA
WAJASIRIAMALI
kisiwani Pemba wameomba kupatiwa elimu ya usarifu wa bidhaa, ili waweze kutengeneza bidhaa zenye ubora na
zenye viwango, ambazo zitauzika katika Soko la ndani na nje ya Pemba.
Wajasiriamali hao walitoa ombi hilo katika mafunzo ya ujuzi
wa kidijitali yaliyofanyika kituo cha Uwalimu TC Wingwi wilaya ya Micheweni
mkoa wa Kaskazini Pemba.
Biamu Omar Mbrouk mwanakikundi cha Hapa kazi kutoka Wingwi,
ambacho kinajishughulisha na utengenezaji wa sabuni, mafuta, na unga wa mwani,
alisema wamekua wakitengeneza bidhaa nyingi lakini zinashindwa kuuzwa hata
Unguja, na huishia kuuzwa mitaani tu kutokana na kukosa ubora.
Alisema Mwani umebainika kuwa ni moja ya dawa inayotibu magonjwa mengi katika mwili wa mwanadamu,
hivyo ni vyema kupatiwa elimu, ili wawe
wazalishaji bora.
‘’Tunatamani siku moja kuona kwamba, na sisi tunaziuza
Tanzania bara na hadi Nchi za nje bidhaa zetu, kwani kutatuwezesha tuweze
kutambulika na pia kuinua uchumi wetu,’’alisema.
Ali Khatib Ali mjasiriamali wa kikundi cha Tumuombe Mola cha
Makangale kinachojishughulisha na ufugaji wa Majongoo ya baharini, alisema
wanahitaji kupatiwa elimu juu ya usarifu wa mazao hayo, ili waweze kuzalisha
kwa kuzingatia viwango na kiutaalamu.
Alisema kuna utaalamu wa kulima na kuchakata wakati
wanapovuna, ingawa wao bado wanafanya tu, jambo linalopelekea kukosa bei
wanayoihitaji.
‘’Mukisha kuwavua
wanautaalamu wake wa kuwachakata lakini sisi hatujui, bali tunawachemsha tu na badae
ndo tnawauza, kikukweli tunahitaji kupewa elimu,’’alisema.
Alisema endapo
watapatiwa elimu kutawasaidia kufuga kwa uwelewa, na kupata bei nzuri inayolingana
kilimo hicho, ambacho kitawawezesha kujikimu kimaisha.
Nae Abdala Salim Masoud mwanakikundi cha Ipo sababu ambacho
kinajishughulisha na ukulima wa mwanai alisema wanahitaji kupatiwa elimu ya
utengenezaji wa pagi za plastiki kwa ajili ya kufungia mwani wao, ili
waondokane na na changamoto ya upatikanaji wa pegi hizo.
‘’Tunapokata pegi za mikanda au mibura haturuhusiwi, kwani
tunaharibu mazingira, hivyo tunahitaji kupatiwa elimu tutengeneze pegi za
plastiki, ili tuondokane na usumbufu na tuzalishe mwani kwa wingi,’’alieleza,’’
Alisema Kampuni ya mwani ya Sewedi Coporation walishawahi
kwenda na kufanya utafiti wa kutengeneza pegi hizo, ingawa hadi sasa hawakurudi
tena kwa ajili ya kuwapatia elimu hiyo.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mratibu wa Fawe
Winnifred Yatuma Manawi Mjumbe wa bodi ya Fawe Zanzibar Biubwa Mohamed Mselem
aliwataka wajasiriamali hao, kuyatumia
mafunzo watakayopewa, ili waweze kuleta mabadiliko katika vikundi vyao.
‘’Nyinyi wajasiriamali ambao mmebahatika kushiriki kwenye
mafunzo haya, naomba muyachukue na muyafanyie kazi, ili muendeleze vikundi
vyemu na muweze kuzalisha kwa mazao kwa wingi na kujingizia kipato,’’alisema.
Alisema lengo la FAWE ni kuwakomboa wanawake na vijana
kiuchumi, hivyo ni vyema kuhakikisha wanayafanyia kazi, ili wawe wazalishaji na
watengenezaji wa zuri wa bidhaa.
Mafunzo hayo ya sikumbili kwa vikundi vya wajasiriamali
yameandaliwa na Jumuia inayoshughulikia na kutoa masuala ya wanawake na watoto,
vijana na watu wenye ulemavu (FAWE)chini ya ufadhili wa UN WOMEN.


Comments
Post a Comment