SARATANI YA SHINGO YA KIZAZAI ADUI MWINGINE MPYA KWA WANAWAKE, HUATHIRI MFUMO WA UZAZI
Kumbe kukosa mtoto, na magonjwa nyemelezi ni sehemu yake NA FATMA HAMAD, PEMBA SARATANI ya shingo ya kizazi ni ile ambayo, hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembe chembe au seli zilizomo katika shingo ya kizazi na wingine wakiita mlango wa kizazi. Saratani hii huathiri shingo ya kizazi, ambayo ni sehemu ya chini ya mfuko wa kizazi, ambapo kwa kawaida huonekana pale tu mwanamke, anapolala chali na inaweza kuonekana kupitia uke wake. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni ‘WHO’ inathibitisha kuwa, saratani hii, ni ya nne kwa kuathiri wanawake, ikiwa na wagonjwa wapya 604,000 mnamo mwaka 2020. Takriban asilimia 90 ya vifo 342,000 vilivyosababishwa na saratani ya shingo ya kizazi, vilitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Viwango vya juu zaidi vya saratani hiyo na vifo ni kutoka Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika ya Kati na kusini Mashariki mwa Asia. Tak...