‘’Wandishi wa Habari msiandike habari, zenye kuleta migongano’’

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid amewataka wandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli na zenye kuzingatia maadili, ambazo hazitosababisha uvunjifu wa amani Nchini.

Mkuu huyo ameyasema hayo  wakati akifungua  Kongamano  la wadau wa Habari,  lililoandaliwa na Ofisi ya Rais Ikulu huko ukumbi wa ZRA Chakechake Pemba.

Alisema vyombo vya Habari ndivyo ambavyo vinaweza vikaiweka Nchi katika hali ya Amani, ama kwenye migogoro, hivyo ni vyema wandishi mkatumia maadili yenu na kuandika habari zenye ukweli na zenye kuleta maendeleo,ili kuibakisha Nchi katika hali Utulivu.

Alisema Serikali ya awamu ya nane imefanikiwa kuweka mambo mbalimbali ya maendeleo mjini na vijijini, hivyo ni jukumu lenu wandishi wa habari kuyandikia maendeleo hayo.

‘’Yapo mambo mengi ya maendeleo ambayo yamefanywa na Serikali yetu, hivyo yaandikeni hayo, ili yapate kufahamika, msiandike mambo ambayo yataleta uchochezi,’alieleza.



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja aliwasisitiza wandishi wa habari kuzingatia takwimu wakati wanapoandika habari zao.

‘’Ili uwe mwandishi mzuri na kazi zako ziwe zinavutia na zinasomwa na watu wengi, ni lazima uwe unatumia takwimu katika Makala yako ama kipindi chako,’’alisisitiza.

 Mapema  Afisamdhamini kutoka Tume ya Mipango Pemba Khamis Issa alisema wandishi wa Habari wananafasi kubwa, hivyo ipo haja kuibua kero na changamoto zilizoko, zieze kufahamika Ili Serikali iweze kuzitatua.

‘’Juzi wakati mheshimiwa Rais akiwa kule uwekezaji Micheweni alisema sasa ni zamu ya Pemba, jee kama wandishi wa habari mnafanyanini, kuona mnayaibua hayo maeneo ambayo bado  kuna changamoto ili mkaisaidia Serikali,’’alisema.

Nao wandishi wa Habari walioshiriki Kongamano hilo wamesema ni vyema kufanyiwa marekebisho baadhi ya Sheria ambazo zinakwaza uhuru wa utekelezaji wa majukumu yao.



Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO