Wandishi ibueni kero zinazowakwaza wanawake, kushindwa kutimiza ndoto zao za kua viongozi

 



Na Fatma Hamad-Pemba

CHAMA cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar kimewataka waandishi kisiwani Pemba kushirikiana  pamoja na  wahamasishaji jamii ( CBEES ) juu ya maswala ya wanawake na uongozi ili  kuongeza nguvu na kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake   na kuongeza ushiriki wao katika nafasi za uongozi.

Wandishi wa Habari wametakiwa kujikita Vijijini, ili waweze kuibua kero zinazowakwaza wanawake, ambazo zinawafanya washindwe kugombea nafasi mbalimbali katika uongozi.

Akizungumza na waandishi hao kutoka vyombo mbali mbali kisiwani Pemba Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka  (TAMWA) Mohamed Khatib Mohamed  waliofika katika mkutano maalum uliowakutanisha wahamasishaji jamii pamoja na waandishi hao uliofanyika katika ukumbi wa PEGAO Msingini Chake chake Amesema  katika miaka ya nyuma wanawake  walikua wako nyuma kushika nafasi za uongozi, kutokana changamoto mbalimbali ambazo zinakua zinawakabili, hivyo ni wakati kwa wandishi wa habari kuziibua kero hizo na kuzisemea, ziweze kusikika katika Mamlaka husika na kuweza kufanyiwa kazi,  ili waweze kupata  fursa za kushiriki kwenye uongozi.

‘’Wanawake wamekua wakikumbana na keronyingi ambazo zinawafanya wasiyape kipaombele masuala ya uongozi,mfano kukosekana huduma za mama na mtoto, Maji safi na salama, barabra,’amesema Afisa ufuatiliaji na tathmini

Anasema  lengo la mradi wa Swili kuhakikisha wandishi wa habari wanaielimisha  jamii waweze kubadilika, ili kuona wanawake wanashiriki nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya Shehia hadi ngazi za juu.

‘’Tunatamani  kuona wanawake wanashika nafasi za masheha, ubunge, uwakilishi pamoja na ngazi  tofauti tofauti,’’amesema.

Mapema Omar Mjaka Omar ambae ni miongoni mwa wahamasishaji jamii kutoka wilaya ya Micheweni anasema wandishi wa habari ndio sauti ya wanyonge, hivyo ipi haja kufanya majukumu yao  kwa uwadilifu ya hali ya juu, ili waweze kuwasaidia wananchi juu ya kero zinazowakwaza vijijini mwao.

‘’Nyinyi wandishi wa habari ni watu humimu katika jamii, hivyo msiweke mbele maslahi bali fanyeni kazi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi pamoja na Taifa kiujumla,’amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi wa Swil kisiwani Pemba Hafidh Abdi Said amesema  endapo wandishi wa habari watafanya kazi ipasavyo ya kuwahamasisha wanajamii juu ya masuala ya uongozi, wanawake wataweza kushawika na kuhakikisha wanaingia kwa wingi majimboni, ili lile lengo la hamsini kwa hamsini kwenye uongzi liweze kufikiwa.

Nao wandishi wa habari walioshiri kikao hicho wamesema ili kuona wananchi wamefikiwa na kupaza sauti zao, ipo haja ya kuepo na mashirikiano ya hali yaa juu kati yao na timu hiyo ya wahamasishaji jamii  (CBEES.

 Katika mradi huo wa kuwawezesha  wanawake waweze kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi, umefadhiliwa  NORWE ambao unatekelezwa na TAMWA, PEGAO, ZAFELA NA JUWAUZA.

 


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO