SHERIA ZA HABARI ZANZIBAR BADO KIZUNGUMKUTI
NA FATMA HAMAD - PEMBA
Katika
sheria ya usajili wa uwakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka
1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no 8 ya mwaka 1997 yapo maneno kadhaa yaliyotumika
ambayo yanaonekana kuwa na mapungufu na ambayo yanakwaza uhuru wa vyombo vya
habari.
Matumizi
hayo ya maneno yaliyotumika katika sheria hiyo yanaweza kuathiri uhuru wa habari pamoja na waandishi wa habari
ikiwa hayatofanyiwa marekebisho.
Katika makala hii tutaangalia sheria
ya usajili wa uwakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka
1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria
no 8 ya mwaka 1997 ina muda wa miaka 36 sasa, ambapo katika vifungu vyake inayo maneno
ambayo sio rafiki kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
Miongoni mwa maneno hayo yenye
kuleta ukakasi yanapatikana katika kifungu cha 30 cha Sheria ya usajili wa uwakala wa habari, magazeti na
vitabu namba 5 ya mwaka 1988 kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya
mwaka 1997 kwa mfano neno “endapo waziri ataona kuwa ni kwa manufaa ya umma au
kwa maslahi ya amani na utulivu anaweza kuamuru kufungiwa kwa gazeti.
Hivyo ni dhahiri kwamba Kifungu
hicho kimempa mamlaka makubwa Waziri wa habari, na kinaweza kumfanya akatumia
vibaya madaraka yake kwa kuwakandamiza
wengine kwa kutokana na chuki zake tu binafsi.
‘’Inawezekana waziri akawa wanaugomvi
tu na Muandishi wa habari au Muhariri, hapo inawezekana akapata mwanya na
kutumia mamlaka yake na kumfungia
mwandishi au chombo cha habari’’
Katika kifungu cha 27[2] kuna sentensi
isemayo: “hakimu yeyote anaweza kutoa hati na kumuidhinisha afisa yeyote wa
cheo cha inspekta kwa msaada au bila msaada kuingia na kupekua kazi yoyote ya
habari. Jambo hili wadau wa habari linawakosesha usingizi, kwani kinawanyan’ganya
haki ya kutoa habari kama ilivyoainishwa kikatiba.
Kutokana na hayo wandishi pamoja na wadau wa
habari wakapaza sauti zao kuipigia
kelele sheria hiyo ili iweze kuangaliwa tena upya kwa lengo la kuondoshewa baadhi ya maneno hayo ambayo imeonekana
hayaendani na uhuru wa habari na demokrasia.
WAANDISHI
WA HABARI
Said Abdulla kutoka Radio Istikama anasema neno endapo ni neno ambalo halina uhakika, na
linaingilia uhuru wa habari kwani mtu aliepewa mamlaka anaweza kumfungia
mwandishi wa habari kwa kutokana na utashi wake mwenyewe tu.
‘’ Neno akihisi au akidhani au endapo sio
maneno mazuri, kwani anaweza kumfungia mwandishi au chombo cha habari
akiwa na chuki zake tu binafsi, anasema
Said.
Mohamed
Khalfan mwandishi redio Nnur anasema
neono endapo, akidhani yeyote sio maneno rafiki hayaendani na mazingira, kwani
yanatoa mamlaka makubwa na yanaweza kumpelekea mwenye mamlaka aliepewa kuyatumia vibaya mamlaka hayo.
‘’Haiwezekani mtu mmoja tu akihisi,
akidhani, endapo akishuku tu chombo fulani sasa hivi kinaandika habari
mbaya aingie na kupekua, au afungie chombo cha habari, hilo ni tatizo kubwa
kwani yeye ni binadamu kama wengine ana mapungufu yake hebu hilo liangalieni
tena,anashauri.
Bakia Khamis Faki kutoka Zenji tv anasema maneno hayo yanaleta migongano na
hayaendani tena na mazingira ya kihabari, hivyo wakati umefika kwa wadau wa
masuala ya kisheria kukaa chini na kuipitia tena upya Sheria hiyo ya usajili wa
uwakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa
marekebisho na sheria no 8 ya mwaka 1997 ili kuondosha istilahi zinazoashiria
vikwazo.
WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI
Suleiman Said Ali mmiliki wa Jicho letu Oline
tv anasema maneno yaliotumika katika
Sheria ya Usajili wa Uwakala wa
Habari Vitabu na Magazeti namba 5 ya
mwaka 1988 yana ukakasi, kwa mfano kifungu cha 30 sentensi “endapo waziri ataona
kuwa ni kwa manufaa ya umma au kwa maslahi ya amani na utulivu anaweza kuamuru
kufungiwa kwa gazeti.”
Hata kifungu cha 27[2] kinachosema “hakimu yeyote anaweza kutoa hati
na kumuidhinisha afisa yeyote wa cheo cha inspekta kwa msaada au bila msaada
kuingia na kupekua kazi yoyote ya habari,” kifungu hiki sio rafiki kwa vyombo
vya habari na kinahitaji kufanyiwa marekebisho au kiondoshwe kabisa, kwani inaweza
ikapelekea wahusika kutumia mamlaka yao kwa utashi wao wenyewe.
Mgeni Kombo Khamis mmiliki wa Blog ya
Habariportal anasema maneno hayo yaliyotumika katika Sheria siyo rafiki
hayaendani tena na wakati wa sasa, na
yanawafanya waandishi wa habari kufanya majukumu yao wakiwa hawako huru.
‘’Kwa kweli maneno yaliyotumika katika Sheria
yetu hiyo ya habari yana ukakasi si ya
kidemokrasia, na hayawapi hamu wandishi kuandika habari zilizojificha na hata
sisi kumiliki vyombo vya habari,’’anamalizia Mgeni.
WADAU
WA HABARI
Mustapha Mohamed Moyo kutoka Tasaisi ya Moyo
media anasema endapo kama kutakuwa na Sheria ambayo ina maneno yenye ukakasi yatawatia
hofu baadhi ya watu ambao wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya habari.
‘’Kwa kweli ukisema mtu endapo, yeyote, atakapojisikia, atakapodhani,
sio maneno mazuri, na yanawatia hofu wawekezaji katika sekta ya habari hivy
wanarudi nyuma wanahisi hizo Sheria zipo kwa ajili ya maslahi ya wenye mamlaka,’’anafahamisha.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari
kisiwani Pemba (PPC) Bakar Mussa Juma anasema maneno hayo yaliyotumika katika Sheria hiyo
yanaathiri uhuru wa waandishi wa habari jambo linapolopelekea waandishi wa habari
pamoja na jamii kukosa haki yao ya
kikatiba ya kupata habari.
TAASISI
ZINAZOSIMAMIA WAANDISHI WA HABARI
Afisa program kutoka Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania TAMWA ZANZIBAR Zaina Abdala Mzee anasema Sheria ya habari imeshakua kongwe haiendani
tena na mazingira ya sasa, inahitaji kufanyiwa marekebisho.
‘’Tunatamani siku moja kuona nasisi Zanzibar
tumepata Sheria mpya ya habari ambayo haina maneno yenye kuleta mkanganyiko kwa
waandishi wa habari,’’anasema.
Anasema wamekua wakiwajengea uwezo waandishi
wa habari waweze kuipigia debe Sheria hiyo,
ili hatimaye kuona imefanyiwa marekebisho anasema Zaina.
WANASHERIA
Zahran Mohamed Yussuf ni wakili wa
kujitegemea kutoka Wilaya ya Chakechake anasema ipo haja ya kufanyiwa
marekebisho kwa Sheria hiyo ya habari, kwani inayo maneno/istilahi ambayo siyo rafiki kwa vyombo vya habari.
‘’Tujue
kwamba waandishi wa habari ndio wanaoifanya nchi kuwa na amani na maendeleo,
hivyo hivyo kama sheria zitakuwa na vipengele vinavyowabana kutekeleza kazi zao
kwa ufanisi tufahamu kwamba maendeleo hayo hayatafikiwa, kwani wao wenyewe
watakua na hofu katika utekelezaji wa kazi zao,’’ anasema Zahran.
Comments
Post a Comment