WANAWAKE WAMUOMBA DOKTA SAMIA KUWAUNGA MKONO KENYE UONGOZI


NA FATMA HAMAD- PEMBA

WANAWAKE WA CHAMA CHA Wananchi CUF wamemuomba Raiswa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kulinda haki za wanawake wa vyama vya upinzani watakaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Oktaba mwakahuu,  ili nafasi za wanawake ziwenyingi zaidi.

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake ya CUF Taifa Anna Rioba Paul katika maadhimisho ya siku ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika huko Vikunguni, Wilaya ya ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema wanawake wengi wa vyama vya upinzani kikiwemo CUF wamekua na shauku ya kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, lakini wamekuwa wakienguliwa kwa kisingizio cha kuwepo makosa katika fomu za maombi za uteuzi, jambo ambalo ni tofauti na upande wa Chama Tawala CCM,

Alisema kuepo na changamoto hiyo imekua ikikatisha ndoto za  wanawake  wanaotaka kugombea, na kupelekea kubakia nyuma katika nafasi za uongozi.

 ‘’ Tunakuomba Rais wetu mpendwa mama Samia uwangalie wanawake watakaojitokeza kugombea nafasi za uongozi, kuondosha baadhi ya vikwazo ambavyo vimekua vikiwakwaza, ili kuona wanaingia kwa wingi katika maamuzi,’’alisema.

Aidha katibu huyo alisema ni vyema Serikali ikaweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanawalinda wagombea wanawake, juu ya vitendo vya udalilishaji, katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa mwakahuu, ili kuona wanaondokana na hofu na kuingia kwa wingi majimboni.

‘’Katika kipindi cha uchaguzi Wagombea wengi  wanawake wamekua wakikumbana na vitendo vya udhalilishaji, hivyo tunakuomba mamaetu kipenzi kwavile na ww ni mwanamke, utusikie kilio chetu uweke mkakati wa hali ya juu, ili kuepusha vitendo hivyo visitokee mwaka huu,’’alisisitiza.


Kwa upande wake  NaibuKatibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Zanzibar  Ali  Juma Khamis alitoa wito kwa wanawake wa Chama hicho kujiandaa ili waweze kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwakahuu wa 2025 utakaofanyika mwezi wa Oktoba, ili kufikia adhma ya hamsini kwa hamsini katika nafasi za  maamuzi.

Alisema wanawake wa chama hicho  hawapaswi  kuwanyuma katika kugombea nafasi za uongozi,  kwani wao ndio wenye uchungu mkubwa na chamachao na ndio wanapelekea chama hicho kupiga hatua kimaendeleo.

‘’Hakuna aliezaliwa na kujua, Wanawake msiwenyuma  kwani na nyinyi mnahaki sawa na wanaume, jitokezeni kuchukua fumo za uongozi, kwani nyinyi ndio wadau wakubwa mnaokifanya chama kisimame,’’alisema.

Nao baadhi ya wanawake ambao walishiriki kongamano hilo waliitaka Serikali kuondosha vikwazo katika upatikanaji wa mikopo, ili kuona wanawake wanawake wananufaika na mikopo hiyo, ambapo itawasaidia kumudu gharama za uchaguzi, wakati watakapokwenda kugombea.

‘’Kwa vile  lengo la Serikali yetu ni kutuinua sisi wanawake kiuchumi, tunaomba mikopo iendelee kutolewa na bila ya kuepo kwa masharti ambayo hayatukwazi, Ili  tuweze kunufaika nayo’’,walieleza.

Kaulimbiyu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni mwanamke akiwezeshwa anawez.




 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO