TIMU ZA WANAWAKE ZA PEMBA ZAOMBA KUSHIRIKISHWA KWENYE MASHINDANO YA KITAIFA
NA FATMA HAMAD-PEMBA Kukosekana kwa uwanzishwaji wa ligi maalumu kwa wachezaji wanawake, imekua ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha Timu ya Mpira wa pete iliyopo Mchangamdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Hayo yamesemwa na Amina Kudra Ali Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Wete wakati wakizungumza na wandishi wa habari ikiwa ni ufuatiliaji wa tathmini ya mafanikio wa mradi wa michezo kwa maendeleo uliokua ukitekelezwa na Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA), Chama cha wanasheria wanawake (ZAFELA) na CYD. Anasema anahamu ya kua mchezaji mkubwa duniani, lakini anarudinyuma kwasababu tangu walipoanzisha timu hiyo hawajashirikishwapo mashindano ya ligi za aina yoyote na kuweza kukuza vipaji vyao. ‘’Huu ni mwaka wa tano tokea kuanzisha timu yetu hii ya mpira wa pete pamoja na Netball, lakini tunakata tama hatujashirikiswapo hata siku mo...