Yafahamu madhara anayopata mwanamke wakati akijiwekea vitu katika sehemu zake za siri

 

                   NA FATMA HAMAD - PEMBA

 Wanawake wametakiwa kuacha tabia ya kuweka vitu kwenye sehemu za siri, kwani wanaweza kuathiri mfumo mzima wa viungo vya uzazi.

 Hayo yamesemwa na Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba (ZAC) Ali Mbarouk Omar  wakati Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) ZANZIBAR Ofisi  Pemba, alisema, wapo baadhi ya wanawake huweka vitu katika sehemu zao za siri, jambo ambalo ni hatari kwa afya ya uzazi.

 Alisema kuwa, ni vyema wakaenda  hospitalini na vituo vya afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mara kwa mara, endapo wamepata matatizo waweze ili waweze  kupatiwa matibabu na sio kuweka vitu ambavyo vinaweza kuwapatia madhara zaidi.

 "Kuna baadhi yao huweka vitu kama wanajitibu baada ya kupata magonjwa ya kujamiiana na kuna wengine wanaweka vitu hivyo kwa urembo, haya yote hayafai kwa sababu wanaweza kuathirika katika mfumo wa kizazi," alisema Katibu huyo.

 Aidha, akielezea kuhusu maambukizi ya magonjwa ya kujamiiana alisema, pia yanasababisha kuathiri kizazi cha mama na kupeleka mtoto anaezaliwa kupata madhara mbali mbali.

 "Maradhi ya kuambukiza ikiwemo ukimwi, saratani ya shingo ya kizazi, gonoria, pangusa, kisonono cha usaha ni hatari katika kuharibu mfumo mzima wa uzazi kwa mwanamke, hivyo waache tabia ya kufanya ngono zembe kuepuka magonjwa hayo," alieleza.


Akifungua mkutano huo Afisa Mawasiliano kutoka TAMWA Zanzibar Khairat Haji Ali alisema kuwa, elimu ya afya ya Uzazi ni muhimu  na inahitajika iwafikie wanajamii, hivyo ipo haja kwa waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuielimisha jamii.

 Alisema kuwa, wameamua kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kusudi waelewe masuali ya afya ya uzazi, jambo ambalo litawasaidia kutoa elimu kwa jamii wakiwa na ujuzi wa hali ya juu.

 "Wanawake wanapata shida kubwa kwenye mfumo wa uzazi bila kujijua, hivyo iwapo waandishi tutaweza kutoa elimu, jamii itaelewa na watakuwa ni wenye kupima afya zao na kuacha Yale ambayo yatawasababishia matatizo," alisema.


Akitaja baadhi ya dalili za maradhi ya kujamiiana  Mratibu wa kituo cha Tiba na Kinga  Rahila Salim Omar, ni  maumivu chini ya kitovu, majeraha sehemu za siri, kuharibika kwa mimba, kutokwa na maji maji mazito sehemu za siri yenye rangi na harufu.

 "Kuweka vitu sehemu za siri pia kunasababisha saratani ya shingo ya kizazi, hivyo waandishi nijitahidi kuielimisha jamii yetu," alifahamisha.


Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo walisema kuwa, watahalikisha wanaibadilisha jamii kwa kuwapa elimu ya afya ya uzazi, ili kuondosha madhara yanayowapata wanawake na watoto.

 "Tumejifunza mambo mengi ya afya ya uzazi, hivyo kupitia elimu hii, itatusaidia kuielewesha jamii ili wajitunze na kuepuka madhara mbali mbali," anaeleza.


Mafunzo hayo ya siku mbili  waandishi wa vyombo vya habari mbali mbali kisiwani Pemba  yameandaliwa na Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania  TAMWA   Zanzibar.

 

                       

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI