Tunahitaji kupatiwa maji, tuzalishe mazao kwa wingi ili tujikomboe na umaskini
NA FATMA HAMAD –PEMBA
KUKOSEKANA KWA HUDUMA za Maji safi na
salama imekua ni kero kubwa kwa wakulima
wanaolima kilimo msitu katika
Shehia za Mjini kiuyu, Kambini
kichokochwe, Mchanga mdogo na Chwale wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akizungmza na mwandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea
katika mashamba yao mkulima Fatma Sheha Juma kutoka Kiuyu minungwini anasema
wanahitaji kupatiwa maji katika mashamba yao, ili waweze kukuza vilimo vyao.
Alisema
wanapata shida kubeba maji majumbani kwao na kupeleka katika mashamba yao,
hivyo wanahitaji kupatiwa msaada wa kuchimbiwa visima karibu na maeneo yao
wanayolima, ili waweze kuzalisha mazao kwa wingi.
‘’Kwakweli
kubeba maji kwa vichwa kutoka majumbani
hadi mashambani kwetu tunakolima ni
shida tunaathirika, hivyo tunaomba
tuangaliwe,’’alisema Fatma.
Alisema ili
waweze kulima na kuzalisha mazao kwa
wingi kunahitajika kupatikana kwa maji ya kutosha kwa ajili ya kumwagilia mbegu zao.
Kwa upande
wake mkulima Fatma Mohamed Shaib alisema wameshaanza kuotesha miche, lakini
inakufa kutokana na kukosa maji.
‘’Tulitegemea
tuvune mazao mengi ili tuweze kuuza na kupata chakula cha kutosha, lakini mazao
yetu yanakufa tunachoka kubeba maji sehemu za mbali,’’alieleza.
Alisema wanahamu
ya kulima kilimo msitu lakini wanarudinyuma kutokana na kukosekana kwa maji ya
kumwagilia vipando vyao.
Mkulima
Kombo Bakari kutoka shehia ya Minugwini
amaeitaka Serikali pamoja na wadau wengine kuwafanyia msada wa kuwatilia
umeme ili waweze kujenga visima karibu na mashamba yao.
‘’Tunategemea
maji ya mvua, kwa kipindi hiki cha
kiangazi tunakosa maji ya kumwagilia, hivyo tunahitaji tuwekewe umeme,
ili tuweze kuchimba tusitegemee maji ya
mvua tu,’’anasema.
Afisa
uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa Ofisi ya Pemba Suleimana Anass
Masoud alisema Mamlaka ya Maji inangalia
matumizi ya nyumbani kwanza na sio kwa shughuli za umwagiliaji.
Alisema
Wakulima wanaouwezo wa kuchimba visima vyao
wenyewe, isipokua wafuate masharti
kutoka kwa Mamlaka husika ya Maji
safi na salama.
‘’Walio na
jukumu la kusaidia maji kwa ajili ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo wadogo ni
wizara ya kilimo, sisi tunaangali kwanza mahitajio ya wananchi,’’alieleza.
Aidha
aliwasisitiza wakulima kutumia maji kwa
uwangalifu ili kuepuka kutokea kwa uharibifu wa miundombinu ya maji, jambo
litalosbabisha kukosekana kwa maji kwa wananchi.
Afisa
mdhamini wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi, Idirisa Abdulla Hassan
alisema katika wizara yake wameweka mkakati maalumu wa kuwasaidia wakulima
hususan wadogo wadogo, ili kuona
wanaondokana na changamoto zinazorudisha nyuma vilimo vyao.
‘’Tunahakikisha
tunawasaidia wakulima wa vikundi mbalimbali, ili kuona wanaondokana na changamoto na kuhakikisha
wanazalisha mazao kwa wingi.
Nae Mkurugenzi
wa Tasisi ya upandaji wa misitu
Pemba CFP Mbarouk Mussa Omar
alisema tayari wameshaomba ufadhili kutoka kwa Serikali ya Kanada CFI wa
kuchimbiwa visima wakulima hao ili waweze kuondokana na kero hiyo.
‘’Tayari
tumeshaomba ufadhili kutoka kwa wenzetu kutoka Kanada, kuchimbiwa visima ili
kuona wakulima hao waweze kupata maji, na kuzalisha mazao ya kutosha.
Comments
Post a Comment