Jitihada za vyama vya sisa wanazozifanya kwa wanaume, juu ya uongozi kwa mwanamke

 

                   Na Salim Hamad-Pemba

Suala  la  uongozi    ni  haki  ya   raia   wote  na sio kwa    wanaumme  pekeo .

Kwani Haki ya uongozi imetajwa  katika Kifungu cha 21 (3)  cha Katiba ya Zanzibar   ya  mwaka 1984  kinasema  kila  Mzanzibari  anayohaki  ya kushika  nafasi  yoyote  ya  kazi  na  shughuli  yoyote  iliyoko  chini  ya Mamlaka  ya  Zanzibar.

Sera na Sheria mbalimbali za Zanzibar zimeelekeza kutambua haki ya mwanamke kushiriki katika demokrasia na uongozi.

Historia  inatuonesha kwamba uislamu unaruhusu mwanamke kuwa kiongozi, kwani wapo wanawake kadhaa ambao walishiriki  nafasi za mamuzi  wakati wa Mtume Muhammad (S.A. W).

Ambapo miongoni  mwa wanawake walioshika  uongozi ni Bi Khadija  mke wa Mtume  (S.A.W),  mtu wa mwanzo kuupokea Uislamu  kutoka kwa Mtume Muhammad.

Pia Bi Asma binti Abu Bakar ndie alieongoza kitengo cha utoaji wa tarifa na habari kwa Mtume ( S .A. W) wakati wa kuhamia Madina.

Hivyo ni wazi kwamba mwanamke anaruhusiwa kushika nyadhifa kwenye uongozi, ingawa  hadi leo  tumekua tukishuhudia wanawake kadhaa ambao hupewa  talaka  na waume zao, kwa sababu wameingia kwenye siasa.

Makala hii imewatafuta viongozi wa vyama vya siasa na kutaka kufahamu wanachukua jitihada gani kuwaeilimisha wafuasi wa vyama vyao pamoja na wananchi, kuona wanawashajiisha na kuwapafursa  wanawake,  waweze kujiingiza majimboni kwa  wingi  katika  uchaguzi  mkuu  wa  Zanzibar wa mwaka huu 2025.

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Katibu wa Chama cha ACT  -WAZALENDO Mmkoa wa Micheweni  kichama  Khatib  Hamad  Shehe anasema wanachokifanya ni kuwapa elimu jamii, ili wawape nafasi wanawake  waweze kushiriki kwenye kwenye masuala ya uongozi.

‘’Tunachokifanya kwa sasa tunawahamasisha wanajamii, wawaruhusu wanawake, waweze kuingia kwa wingi majimboni katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 ili kuepuka  talaka hizo za ovyo ovyo,’

Maryam  Saleh  Juma ni Mwenyekiti wa Mkoa Chakechake  Chama cha Ukombozi  Chauma  anasema katika Chama chao wamekua wakiwaelimisha  wanawake wanaotaka kugombea  kwanza  kujielewa, kulinda utu  wao na pia  kuheshimu maadili ya dini yao, ili waweze kujijengea uwaminifu kwa waume zao,  katika  kipindi  chote  cha uchaguzi.

 ‘’Tumekua  tukitoa elimu siku zote kwa wagombea wanawake  na waume zao, waweze kuaminiana na kuheshiniana, ili kubakia katika ndoa zao mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ,’’anaeleza.

Habib Ali Khamis katibu wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pemba anasema wanachokifanya  wao  ni  kuwapa  mafunzo wanawake  wanaotaka  kugombea  waweze  kujitambua,   na  kufahamu  wana nafasi gani katika dini yao,  ndoa  zao na pia kwenye chama chao.

‘’Tunawaelimisha wanawake kwanza waweze kujitambua na  vipi  anapata ruhusa kwa mume wake ya kujiingiza kwenye harakati za uongozi,’’anaeleza.

Anasema ikitokea kuna mwanamke wamempa elimu na mume wake  hakumpa ruhusa, wanawaita  wote wawili na kuwaelimisha, na kuona wanabakia kwenye ndoa yao endapo mwanamke  atagombea.

‘’Endapo  kama itatokea  kunamwanamke  anataka kugombea  mume wake hampi ruhusa, hatumuachi  tu akapoteza  ndoto yake, bali tunahakikisha  tunamuelimisha mwanamme  kufahamu  umuhimu  na faida  za  wa uongozi  kwa  mwanamke,’’anafahamisha.

Anasema watahakikisha wanatumia njia za busara kuwaelimisha  wanaume  wa Chama chao  kuwaruhusu wanawake  waweze  kujitokeza  kwa  wingi  majimboni katika  Uchaguzi  wa  mwaka  huu,  ili kuona  hakutokei vitendo  hivyo  vya  talaka  kwasababu  ya  mambo  ya kisiasa,  amemalizia  Habib.





SHUHUDA WA ALIEACHWA

Fatma Khamis Rashid (sio jina lake halisi)   mkaazi  wa  Kaskazini  Pemba   ni mmoja wa walioachwa,  na  mume  wake  kwa  sababu  tu aligombea ‘’Aliniacha mume wangu kisa niligombea,’’anasema.

 Uchaguzi ni mchezo wa kidunia  kusiwe na migogoro ya ndoa  kama hiyo, hivyo ni wakati  kwa wanaume  kubadilika  na badalayake  waweze   kuwaruhusau wake zao  waweze kugombea, ili waweze kuleta  mabadiliko  majimboni  mwao.

Ni vyema  kwa  vyama   vya siasa  pamoja na mashirika  kama  Chama  cha Wandishi wa  habari wanawake  Tanzania  TAMWA  Zanzibar  kuendelea  kutoa elimu  kwa  jamii  juu  ya  uongozi   kwa  mwanamke,  ili waweze  kutoa  fursa  kwa  wanawake.

WANAHARAKATI

Tatu Abdulla  Mselem  ni mwanaharakati wa masuala ya Utetezi kwa wanawake, watoto, mayatima  na  wanaoishi katika  mazingira  magumu Tujipe  Pemba  anasema sio jambo la busara  katika  ulimwengu huu wa uwatandawazi kusikia  kama  kuna  mwanamme amemuacha  mkewake  kwa  sababu  tu  ameingia  kwenye  kinyan’ganyiro  cha  uongozi.

Mwanamke  nayeye  anaweza kuwakiongozi na akaweza kuleta mabadiliko, hivyo ipo haja kwa viongozi wa vyama vya siasa kuwaelimisha wanachama wao kufahamu madhara ya kukosekana kiongozi mwanamke, ili waweze kuwapa ruhusa.

‘’Ili kuona wanawake wamekuwa na uthubutu wa kuingia kwa wingi majimboni katika uchguzi mkuu ujao, ni lazima vyama vya siasa kufanya  jitihada za makusudi kuwelimisha umma hususan wanaume, ili wawpe fursa wenza wao waingie kwenye mchakato wa uongozi bila ya vikwazo vyovyote,’’anasema .

Kaimu  Mratibu  wa  Chama  cha  wandishi  wa  habari wanawake  Tanzania  TAMWA - ZANZ   Ofisi ya Pemba Amina  Ahmed  Mohamed  anasema  moja ya mkakati walioufanya  wameanzisha  wanaume  mabadiliko,  kwa ajili  ya  kuwaelimisha  wanaume  wenzao, wafahamu  umuhimu wa  uwongozi kwa mwanamke.

‘’Tumeanzisha  timu ya wanaume  mabadiliko ,  ambao   watawahamasisha  wanaume  wenzao, waweze kuwaruhusu  wake  zao,  waweze  kuingia kwenye majimbo  na kugombania,’’naeleza.

Kombo Khatib Bakar  (60) mkaazi wa Kiuyu minungwini anasema ni vyema wanaume kuiga mfano wake,  kwani yeye baada ya mke wake kumpa wazo la kutaka  kugombea  hakumkatalia,  bali alimuunga mkono.

Anasema alijitoa kihali na mali na kumsaidia mke wake  ambae aligombea udiwani jimbo la Wingwi  kwa kipindi chote cha Uchaguzi,   ili wweze kupata nafasi ya Udiwani ambayo ndio aliyogombea.

 ‘’Simkumzui  wala sikua na hisia mbaya nae,  bali nilimuunga mkono kwa kipindichote, kwani nilikua namini anaweza kupambana,’’anafahamisha.

Hivyo amewashauri wanaume wenzake kuwa  na uthubutu kama yeye,  wawaruhusu wenza wao kuingia kwenye  fursa mbalimbali za maendeleo ili walete mabadiliko kwenye jamii,’’anafahamisha.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO