Aliniambia Ami Hakimu anaekaa kwa da Fatma ndie aliemfanya.

 


                          NA FATMA HAMAD-PEMBA

SHAHIDI NAMBA TANO ZUWENA HASSAN Mohamed ambae ni jirani   alieleza Mahkama ya Mkoa Chakechake kwamba, muathirika alimuambia kuwa aliemfanyia  kitendo hicho ambacho kilimpelekea kulazwa Hospitali,  ni ami Hakimu ambae anakaa  kwa da fatma.

 Shahidi huyo alidai kuwa  Julai 15 mwaka jana aliondoka nyumani kwake yeye na mtoto wake na  kwenda Hospitali ya Abdala Mzee  Mkoani kwa ajili ya matibabu yake ya Figo.

Alidai kuwa  baada ya kufika Mkoani mtoto wake alimuaga na kumwambia anakwenda msalani (chooni ) kujisaidia, nayeye  akabakia na kusubiri andike cheti kwa ajili ya kwenda kwa Daktari.

Aliporudi msalani yulele mtoto wake alimuambia kuwa alimkuta babayake  akiwa amekuja na mtoto wa shangazi yake Hospitali.

‘’Aliponiambia  babayake yuko na mtoto wa shangazi yake anamatatizo, nilipandisha  hadi ngazi ya juu  chumba wanacholazwa watoto nilimkuta huyo muathirika amelela kitandani,’’anaeleza.

Alieleza kuwa baada ya hapo aliondoka na kuwafuata wazazi wa mtoto  kituo cha Polisi Mkoani kwa ajili ya kwenda kusikiliza maelezo watakayopewa kituoni hapo.

Aliendelea kusemakuwa aliporudi kutuo cha Polisi alikwenda  moja kwa moja Hospitali alikolazwa mtoto, na kumuuliza amefanyiwa na nani kitendo, nakumjibu alifanyiwa na ami Hakimu anaekaa kwa da Fatma.

‘’Nilimuuliza nani aliekufanya kitendo hicho alinijibu kuwa ni ami Hakim anaekaa kwa da Fatma,’’aliniambia muathirika mwenyewe alida.

Baada ya kumaliza kutoa ushahidi  wake shahidi huyo Mwendesha Mashtaka wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka  DPP Asya Ibrahim aliiambia Mahkama hiyo ya Mkoa kwamba walikua wanashahidi  huyo mmoja, hivyo kesi ighairishwe na ipangiwe sikunyengine kwa ajili ya kusikilizwa.

‘’Mheshimiwa Hakimu kwa leo tulikua tunashahidi huyo mmoja tu, hivyo tunaomba tuipangie sikunyengine,’alidai.

Nae Hakimu wa Mahkama hiyo ya Mkao iliyopo Chake chake Pemba Taki  A. Habib ameighairisha kesi hiyo hadi Februari 18  huku akimtaka mwendesha mashtaka kuleta mashahidi wengine.

‘’Naighairisha  hadi Februari 18 naomba mulete mashahidi wengine, na mtuhumiwa utaendelea kukaa rumande hadi tarehe hiyo,’’lieleza.

Hakimu  Said Hakim (36) mkaazi wa Jondeni Pemba, Julai 14 mwakajana sa 4: 00 za usiku huko Jondeni wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, kwa kutumia nguvu na bila ya ridhaa yake alimbaka mtoto wa miaka Saba (7).

Ambapo kufanya jambo hilo ni kosa kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e)  na 109 (2) vya Sheria nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar.




Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI