Zanzibar Hiro yawakaribisha kisiwa cha Pemba, Kilimanjaro Star
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar,(Zanzibar
Hiro) Ali Bakari Mgazija mara baada ya
kuichapa bao 1- 0 timu ya Kilimanjaro Star, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Michezo
Gombani, alisema ushindi huo unatokana na maandalizi mazuri walioyoyafanya.
Alisema
haukuwa rahisi kuwafunga wapinzani wao kutokana na ushindani uliokuwepo lakini anashukuru kwa Vijana wake kufuata maelekezo, jambo ambalo liliweza
kuchangia kupata ushindi huo.
Alisema bado
ni mwanzo wataendelea kujituma zaidi kuona kila mchezo wanashida, ili kuhakikisha ubingwa wa Kombe la Mapinduzi
katika msimu huu wa mwaka 2025 wanalibeba.
Alisema
anafahamu anakabiliwa na kibarua kizito katika mchezo dhidi ya Burkina Faso
utaopigwa Jaruary 6 anaamini, kwa kasi
walioyanayo Vijana wake wataweza kuondoka na alama tatu.
‘’Tunashukuru
kwa kumaliza salama niwapongeze wachezaji wangu wamecheza Vizuri kwa kufuata
maelekezo tuliyowapa, namini kwa mwendo huu utashinda na michezo mengine licha
ya ushindani uliopo’’alisema.
Kwa upande
wake Kocha Mkuu wa timu ya Kilimanjaro
Star,Ahmed Ali alisema kufungwa kwenye mchezo huo ni kama bahati walioipata
wapinzani wao, pamoja na juhudi
walizozifanya katika kupambana kusaka ushindi
lakini haikuwa bahati yao.
Alisema
tayari mapugufu yaliyojitokeza atakwenda kuyafanyia kazi na kujipanga na mchezo
mwengine, illi aweze kupata matokeo
mazuri, na kuwataka Mashabiki na Wapenzi
wa timu hiyo kutovunjika moyo watashinda mchezo ujao.
Alisema
watawasoma wanavocheza wapinzani wao watakaokutananao kwenye mchezo ujao dhidi ya Kenya, utakaopigwa
January 7 kwani itakuwa tayari wameshasoma mbinu zao .
‘’Tukubali
tumefungwa mchezo haukuwa mgumu kiasi hicho wala haukuwa rahisi ni matokeo ya
kimchezo, lakini tutayafanyia kazi mapungufu
yaliyojitokeza na tutawasoma wapinzani
wetu Kenya tutakao kutananao katika
mchezo ujao hata tukicheza nao itakuwa tumesha jipanga’’alisema.
Mkuu wa
Wilaya ya Chake Chake Mgeni Khatib Yahya alisema kufanyika kwa Michuano hiyo
Kisiwani Pemba,kunatoa fursa kwa Vijana
katika kuibua Vipaji Mbali Visiwani Zanzibar.
Alisema hata
hivyo Vijana watahamasika kujiingiza katika michezo baada ya kuona baadhi ya
Vijana wanavyonufaika na Fursa hiyo kama Feisal Salum kwa kuonesha umahiri
wake.
‘’Tunampongeza
Rais wa Zanzibar,Dk Husein Mwinyi kwa kuleta Mashindano hayo Kisiwani Pemba, Kwani yanalenga katika kuibua Vipaji
Visiwani humu, na Vijana kuhamasika
kujikita katika Sekta ya Michezo’’alisema Mgeni.
Katika Mchezo huo Bao Pekee liliwekwa kimiani na Mshambuliaji Feisal Salum Abdalla katika dakika 51.


Comments
Post a Comment