Wakulima wa kilimo msitu waomba kupatiwa Pembejeo.
WAKULIMA WANAOLIMA KILIMO MSITU katika Shehia za Mjini kiuyu, Kambini kichokochwe, Mchanga mdogo na Chwale wilaya ya Wete Pemba, waomba kupatiwa vitendea kazi ikiwemo Miche ili waweze kuendeleza kilimo chao hicho.
Wakizungmza na mwandishi wa habari hizi huko vijijini kwao mwananchi Maryam Khamis Bakar na Anu Omar Juma , walisema tayari wamesha tayarisha mashamba yao, ila wameshindwa kupanda kutokana na kukosa miche kwa ajili ya kuotesha.
‘’Tayari tumesha tayarisha mashamba yetu vya kutosha, ila tumeshindwa na Miche,’’walisema.
Hivyo waliwataka wizara ya Kilimo maliasili, Mifugo na Uvuvi pamoja Jumuia ya upandaji wa Misitu Pemba CFP kuhakikisha wanawapatia miche ya aina mbalimbali ili waweze kuotesha katika mashamba yao hayo.
Kwa upande wao wakulima Aisha Khamis na Suleiman Abdala Hamad wanasema kilimo msitu kitawafanya wanawake kupiga hatua kiuchumi, kwani wataweza kulima mazao tofauti yakiwemo ya biashara na ya chakula.
‘’Kilimo msitu kitatusaidia kuinua uchumi wetu, hivyo ni vyema tukawezeshwa ili tukaweza kupiga hatua kupitia kilimo msitu,’’walisema.
Mapema Afisa mdhamini wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi, anasema kama wizara wamekua wakitoa elimu kwa vikundi mbalimbali ya utunzaji mazingira ili kuona wanawake wanapiga hatua kupitia kilimo msitu.
Rehema Abrahman Alawi Afisa misitu kutoka Tasisi ya upandaji misitu Pemba CFP Anasema wamekuwa wakiwapatia elimu pamoja na miche wanawake, waweze kulima kilimo msitu kwa ajili ya kujiinua kiuchumi, pamoja na kuepuka kutokea kwa mmon’gonyoko wa ardhi.
‘’Tumekua tukiwahamasisha wanawake wapande miti ya misitu katika mashamba yao, ili waweze kujipatia mahitaji yao muhimu kama vile kuni, miti ya kujengea, na kufahamu athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.


Comments
Post a Comment