Ukata wa fedha unavyochangia wanawake kuyaogopa majimbo.


Na Fatma Hamad – Pemba

Nimewahi  kugombea  mara moja tu,  ila kila nikifiria  kurudi tena jimboni narudinyuma,  kwani sina uwezo kifedha

Simulizi ya Fatma Shaaban Mohamed (51) mkaazi wa Kiuyu minungwini Wilaya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,  inatuonesha  ukata wa fedha unavyomkatisha tamaa kuingia tena jimboni katika Uchaguzi wa 2025

Anasema amegombea Udiwani  mwaka 2010 Jimbo la Wingwi Shehia ya Njuguni  Wilaya  ya  Micheweni  Kaskazini Pemba, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Mama huyo ambae  amezaliwa katika kijiji cha Machengwe Ziwani,  wilaya  ya  Chakechake  Mkoa wa Kusini Pemba.

Anasema  amesomea  taaluma  ya  uwalimu  ngazi  ya  Cheti, katika  Chuo  cha  Ualimu  cha   Wiyat  kilichopo  Wete  Mkoa wa Kaskazini  Pemba,  na  ana familia ya watoto saba.

Anasema ameanza  harakati za siasa mwaka 2012  ameshawahi kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya matawi, na hata za kwenye Jumuia ya wanawake.

‘’Nimeshawahi kugombea nafasi nyingi kuanzia kwenye matawi, na hata nafasi ya ukatibu katika Jumuia ya akinamama  ya Chama changu,  ila  sikuwahi  kufanikiwa’’, anasema

Hakukata tamaa aliendelea kupambana na kukitumikia chama,  kwa vile alikua ana imani siku moja ataweza kufanikiwa.

Suala la kufikiria kugombea alipata ushawishi kutoka kwa walimu wenzake wa Skuli na akashawishika, kwani alikua na ndoto za kua kiongozi tokea zamani.

Mnamo  mwaka 2007  alianza kikamilifu kushuka tawini na kuanza kufanya shughuli ndogo ndogo za chama.

 Fatma anasema mwaka 2010 alijiingiza jimboni na kugombea nafasi ya Udiwani, na kupambana na wanaume bila ya kua na khofu yoyote.

Katika kundi la watu waliojitokeza kuchukua fomu katika Chama chao kwa nafasi hiyo ya Udiwani, yeye ndie alieibuka mshindi, na kuingia kwenye kinyan’ganyiro na kupambana na wapinzani wenzake wa vyama vyengine.

 licha ya kuwa jamii ilimkubali vya kutosha, ila mwisho wa siku alianguka hakuweza  kulikamata  jimbo.

‘’Asikudanganye mtu kama huna pesa kwenye Uchaguzi huwezi  ukashinda,  na mimi nasubutu kusema,  kilichoniangusha  ni pesa  tu  sio  kituchengine,’’anasimulia.

Kwakweli suala la pesa ni tatizokubwa  na linawafanya  wanawake  wengi  warudinyuma kuingia majimboni na shindwa  kugombea.

‘’Sasahivi  wanawake  tuliowengi tumekua na hamu ya kugombea, ingawa umasikini  unatufelisha,  kama huna pesa hakuna yoyote unaempiga kampeni akakuangalia,’’anaeleza.

Amegundua suala la pesa ni silaha kubwa kwenye Chaguzi, na ndio inayowafanya wenyepesa zao sikuzote kubakia wao kwa wao majimboni, na masikini kuishia kuwa wapiga debe tu.

Anatamani kurudi tena  jimboni, ila amekata tamaa, kwani ni masikini,  hana pesa zitakazomsaidia kufanya shughuli za kampeni katika kipindichote cha Uchaguzi

FAMILIA YAKE

Kombo  Khatib  Bakar  (60) mkaazi wa Kiuyu minungwini ni mume wa mwanamama huyo shujaa anasema baada ya mke wake kumpa wazo la kutaka  kugombea  hakumkatalia, alikua anamuamini ataweza, kwani alikua ni mpambanaji na mpenda maendele.

Alijitoa kihali na mali kumsaidia mke wake huyo kwa kila alichojaliwa nacho,  kuhakikisha anapata nafasi, ili aweze kuja kuwa  msaada kwa wanawake wenzake na hata kwa Taifa .

‘’Simkumzui  wala sikua na hisia mbaya nae,  bali nilimuunga mkono kwa kipindichote, kwani nilikua namini anaweza kupambana,’’anafahamisha.

Hivyo amewashauri wanaume wenzake kuwa  na uthubutu kama yeye,  wawaruhusu wenza wao kuingia kwenye  fursa mbalimbali za maendeleo ili walete mabadiliko kwenye jamii,’’anafahamisha.


Salma Kombo Khatib (28) ni mtoto wa Fatma Shaaban yeye anasema walimpa mashirikiano makubwa mamayao, kwani walikua wanamuamini.

Amefahamisha kua walikua wanaimani endapo akapata  jimbo ataleta maendeleo kwa wananchi wake, kupitia Nyanja mbalimbali ikiwemo Afya.

 ‘’Kiongozi mwanamke Tunakua na imani nae zaidi, kwani yeye pia ni mama, na siku zote anaejua utungu wa mwana ni mama mzazi,’’anaeleza.

JIRANI YAKE

Saumu Omar Hamad (40) mkaazi wa Kiuyu minungwini  anasema jirani yao huwa anaweza kua kiongozi nzuri, kwani ni mtu anaekua karibu na wenzake, amekua akiwashauri mambo mengi ya kimaendeleo.

‘’Kwa Kweli jirani yetu huyo tunamkubali kua kiongozi, ametuhamasisha tumejiunga katika vikundi vya hisa, ambapo tukiwa na shida zutu tunakwenda tukikopa,’’amemalizia Saumu.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wiala  ya Micheweni Khamis Juma Omar  anasema  wanachokifanya kwasasa  ni kuwasimamia  wanawake wa  Chama  chao  kupata  mikopo  serikalini, ambayo itawasaidia  kuendesha  shughuli zao  za  Uchaguzi.

‘’Tumekua tukiwasimamia na kuhakikisha wanapata mikopo ya  mfuko wa uwezeshwaji wanawake kiuchumi ili kumudu kuendesha shughuli zao, kwa kipinduchote cha kampeni,’’anafafanua.

WANAHARAKATI

Hidaya Mjaka Ali mwanaharakati wa masuala ya watuwenyeulemavu kisiwani Pemba anasema ipo haja kwa Serikali na vyama vya siasa, kuweka ruzuku maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wanaotaka kugombea, ili kuona wamejitokeza kwa wingi majimboni katika uchaguzi wa 2025.

Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania  TAMWA Zanzibar  kimesema kimekua kikifanya jitihada mbalimbali, kuona kumekua na mazingira rafiki kwa wagombea wanawake katika uchaguzi mkuu wa Octobar 2025.

‘’ Tunatamani kuona kumekua na uwezeshwaji wa kifadha kwa wagombea hususan wanawake, ili wawe na hamu ya kuingia majimboni na kugombea,’’ Amina Ahmed  Kaimu Mratibu Ofisi ya  TAMWA  Pemba  anashauri.

TAKWIMU

Kwa mujibu wa ripoti  ya Tume  ya  Taifa  ya  Uchaguzi  na Kamati ya  Kufuatilia  Uchaguzi  Tanzania  kuanzia  2015  hadi  2020  Idadi  ya  Madiwani wanawake  wa  kuchaguiwa  kutoka kwenye  kata  ni  204  ambao  ni sawa  na  asilimia  5  ya  Madiwani wote.

Kwa  Zanzibar  idadi  ya  waliojitokeza  kugombea  Udiwani katika Uchaguzi  wa  2020  wanaume  walikua  276  wanawake  74  Walioshinda wanaume ni 85 wanawake 25

Kwa mujibu wa Sensa  ya  watu  na  makazi  ya  mwaka  2022  Zanzibar  inawanawake wengi  ambao  ni  974,281  sawa  na  asilimia  51.6  kuliko  wanaume, ikiwa  wao  ni  915,492  sawa na  48.4 

Ambapo licha ya uwingi huo bado idadi kwenye ngazi za maamuzi ni kidogo, Kati ya hao, ni asilimia 21.14 tu kwa wanawake 71 waliojitokeza kugombea udiwani.

ILAANI YA UCHAGUZI YA WANAWAKE.

Ilani  ya  Uchaguzi  ya  wanawake, Uchaguzi wa Serikali za mitaa  ya  mwaka  2019  na  Uchaguzi  mkuu  wa  2020,  Madai  ya  mtandao  wa  wanawake  wameitaka  serikali kusimamia  matumizi  ya  rasilimali  fedha,  hususani ruzuku  zitokanazo  na  kodi  ya  Watanzania,  ili kuhakikisha  zinatumika  kwa  kuziba  mapengo  ya  jinsia wakati  wa  uchaguzi.

ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Moja  ya  mkakati  wa  Ilani  ya  Chama  cha Mapinduzi CCM  ya  mwaka  2024  imesema,  ni  kuwawezesha wanawake  kushiriki  katika  ngazi  mbalimbali  za  mamuzi.

 Hata katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 21 (1) kinaeleza  kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke  na Taifa lake. 

Mkataba wa kikanda wa Nchi za kusini mwa Afrika,  uliotiwa saini mwaka 2008 kupitia kifungu nambari 13 cha mkataba huo,  kinaelezea  kuwekwa  mikakati  madhubuti ya kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwashajiisha katika Nyanja mabali mbali za siasa.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO