TAMWA yatoa agizo kwa wandishi wa habari wa pemba
Na Fatma Hamad –Pemba
Wandishi wa habari wametakiwa
kujikita zaidi vijijini kuibua kero zinazowakwaza wananchi juu ya masuala ya Afya ya uzazi, ili kuona
zinajulikana na kupatiwa ufumbuzi.
Wito huo
umetolewa na Afisa ufuatiliaji na Tathmini kutoka Chama cha wandishi wa habari
wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar Mohamed Khatib Mohamed wakati akizungumza na
wandishi wa habari na wafanyakazi wa wizara ya afya huko ukumbi wa Tamwa
Chakechake Pemba.
Amesema bado
wananchi hususani wanaoishi vijijini wamekua wakikumbana na vikwazo kadhaa kama
vile kukosekana kwa vituo rafiki kwa
mama wajawzito pamoja na upatikananji wa huduma bora za afya.
Amesema wandishi
wa habari ndio mkombozi wa wasio na sauti, hivyo endapo watafanya kazi zao ipasavyo na wakaweza kuziibua kero
hizo ambazo ni kilio kwa wanajamii, kutasaidia kupatikana kwa huduma rafiki na kuepukana na athari
zitokanazo na masuala ya afya ya uzazi.
‘’Wandishi
wa habari nendeni vijijini mkandike shida za wananchi ili zipate kutatuliwa,’’amesema.
Amesema takwimu
zinaonesha kua wengi wanaopata mambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni vijana kuanzia miaka 15 hadi 35.
‘’Wengi
wanaoambukizwa Virusi vya ukimwi ni vijana, hivyo ni vyema vijana mkajitokeza
kwa wingi Hospitali kupima afya zenu,’’anashauri.
Comments
Post a Comment